Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Akizungumza na wanahabari Disemba 09, 2024; Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa adai kuwa CHADEMA ni Chama ambacho kimepoteza mvuto hivyo hakistahili tena kujiita Chama kikuu cha upinzani.
"Wamepoteza dira, wamepoteza misingi ya chama chao, wamepoteza mvuto na kujiita chama cha upinzani kikuu ningewasihi watanzania mnaonisikiliza ni vizuri mkawauliza uhalali wa kujiita ni chama kikuu cha upinzani haupo.
Kwa sababu unapokuwa chama kikuu cha upinzani maana yake una wabunge wengi ndani ya bunge CHADEMA wana mbunge mmoja uhalali wa kuitwa chama kikuu cha upinzani wanautoa wapi.
Wana Mbunge mmoja Aida Kenani, ACT ndiyo wana wabunge wengi ndani ya bunge kwa hiyo chadema kujiita ni chama kikuu cha upinzani hilo jina ni linapaswa watanzania tujitafakari hawana sifa ya kujiita chama kikuu cha upinzani.
Lakini niwaase ndugu zangu wa Chadema watanzania ni watu wenye akili sana watanzania wanaweza kufikiri ukisema chadema ni chama kikubwa nayo hiyo ni dhana tu ambayo wamejikusha upepo ndani ya vichwa vyao."