Mchungaji Msigwa: Hatuwezi kuwa na wachoyo wachache wanaoona ng'ombe wao na biashara zao muhimu kuliko Ngorongoro yenye maslahi ya Taifa

Mchungaji Msigwa: Hatuwezi kuwa na wachoyo wachache wanaoona ng'ombe wao na biashara zao muhimu kuliko Ngorongoro yenye maslahi ya Taifa

Kufukuza/kuhamisha watu zaidi ya laki moja ambao wameishi hapo toka kuzaliwa kwao, takriban nusu karne! sio jambo jepesi..labda kama ku-depopulate kwa kuwawekea by-laws za ukomo wa idadi ya mifugo kwa kila household..lakn ukifanya hamisha-hamisha ya kimabavu italeta shida.
Nyerere aligamisha watu karibu nusu ya Tanganyika na kuwapeleka kwenye vijiji vya ujamaa kando ya barabara
 
Nyerere aligamisha watu karibu nusu ya Tanganyika na kuwapeleka kwenye vijiji vya ujamaa kando ya barabara
Kipindi hicho tunasimuliwa nchi ilikuwa tupu.halaf watu wake walikuwa scattered..yaan kaya X kwenda Y ilikuwa distance hadi ya nusu saa kutembea..ilikuwa ngumu huwahudumia watu waliotawanyika
 
Kipindi hicho tunasimuliwa nchi ilikuwa tupu.halaf watu wake walikuwa scattered..yaan kaya X kwenda Y ilikuwa distance hadi ya nusu saa kutembea..ilikuwa ngumu huwahudumia watu waliotawanyika
Lakini si iliwezekana mkuu? Na maisha yakaendelea
Kinacho shindikana kwa hao wamasai ni nini haswaa

Tuamue moja, Wamasai waondoke au tuachane na hifadhi ipotee wamasai waendelee na maisha na waruhusiwe sasa maisha kamili na sio kuwabana na na sheria za hifadhi inayozidi kupotea kila leo kwa idadi ya watu, mifugo na shughuli za kibinaadamu

Zamani walikua wachache na wanyama walikua wengi
Lakini sasa ni kinyume chake
Muingiliano wao HAUWEZEKANI tena lazima tuchague moja
A
 


Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa zamani wa Iringa mjini na waziri kivuli wa maliasili na utalii ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Nyasa amesema kuwa pamoja na Tofauti zao za kisiasa na kupishana kwa mambo kadhaa ya hapa na pale, jambo moja muhimu ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anapaswa kuwafanyia WATANZANIA na likabaki kama LEGACY kwake basi ni kuiokoa Hifadhi hii ya NGORONGORO ambayo inazidi kuteketea kutokana na ongezeko kubwa la watu, ongezeko kubwa la mifugo, ongezeko kubwa la Nyumba zisizoendana na uhifadhi ikiwemo ujenzi wa Maghorofa, ujenzi holela na hali mbaya ya maisha inayowakuta wananchi wanaoishi eneo hilo huku wale wanaojinasibu kuwatetea wakiishi maeneo nyeti na mazuri yenye huduma zote za msingi jijini Dar es salaam

"Hatuwezi kuwa na wachoyo wachache, ambao ng'ombe zao, biashara zao ziwe muhimu kuliko Ngorongoro inayoingizia mabilioni ya fedha zinazosaidia kupeleka huduma kwa jamii" amesema Mchungaji Msigwa

Mwalimu Nyerere alituachia urithi huu, ni wajibu wetu kuutunza, Serikali ya CCM imeshindwa kuutunza, na ndio maana tunaipinga na tunataka kuiondoa madarakani, haiwezekani watu wanajenga majumba hifadhini, wanazidisha mifugo nakadharika na CCM WAPO TU aliongeza Msigwa.

OKOA NGORONGORO
mwehu msigwa
 
Back
Top Bottom