Pre GE2025 Mchungaji Msigwa kuongea na Waandishi wa Habari baada ya kushindwa Uchaguzi wa Uenyekiti Kanda ya Nyasa

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa kuongea na Waandishi wa Habari baada ya kushindwa Uchaguzi wa Uenyekiti Kanda ya Nyasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama heading inavyojieleza mpaka muda huu mgombea aliyeshindwa kanda ya nyasa amegoma kusema lolote, ameahidi kuita press na kuongea yote yaliyojiri kwenye huo uchaguzi kifupi hajaridhirika.

Hizi habari ni za ndani sana kaeni tayari kwa mvurugano!

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa

- Kuelekea 2025 - Kumekucha: Mchungaji Msigwa amkataa John Mrema kuwa Msimamizi wa Uchaguzi Kanda ya Nyasa

=======

Sasisho

Mchungaji Peter Msigwa amezungumza na waandishi wa habari na Kuwapongeza walioshinda uchaguzi akiwemo Joseph Mbilinyi, pia kasema hakwenda CHADEMA kufata vyeo bali kuwatumikia wananchi, amesema ataendelea kukitumikia chama japo hana cheo chochote na yupo tayari kwenda jimbo lolote watakalomuhitaji.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa: Sikuingia CHADEMA kutafuta Vyeo bali Kuwatumikia Wananchi, nitaendelea kukitumikia chama Katika Jimbo lolote mtakalonihitaji!
Aibu yako Kipara kipya.
 
Wacha uwongo,Msigwa ametoa hotuba baada ya matokeo na kumpongeza sugu kwa ushindi. Wewe unasema amegoma kusema neno lolote. Moderators kwa nini mnaendekeza wazushi kama huyu kiparangoto,ushahidi wa hotuba ya Msigwa uko humu. Au na nyie mna interest na huu uzushi?
Je ameongea na wanahabari au hakuongea?
 
Sugu kura 54

Msigwa kura 52

Mchuano ulikuwa mkali sana kama sio Sugu kuhonga, najua Mchungaji Msigwa angeendelea kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa..!!

CHADEMA rushwa iko wazi wazi na chama chenye zero democracy and zero maendeleo, SACCOS ya Mbowe hii shida sana
 
kipara kipya. najua ndani ya CCM neno maadili limefutika katika kamusi yao lakini kwa huu umbeya mnashusha hadhi ya JF. Hili hapa chini ndilo tamko rasmi la Msigwa baada ya matokeo ya uchaguzi.

View attachment 3003182
Hakika Chadema imetoa somo kubwa kwa chama cha mafisadi, mambuzi na wezi wa kura wa jinsi upigaji wa kura unavyotakiwa kufanyika katika nchi ya demokrasia. Komeni kuleta ujinga wenu humu.
Tamko rasmi ametoa leo!
 
Msambatavangu atakuwa anachekea.

6208957_square.jpg

Lakini ajue kicheko chake ni cha muda tu Kiama chake 2025.
 
Aongee tu tujue madudu ya hiyo saccos toka moshi.
 
kipara kipya. najua ndani ya CCM neno maadili limefutika katika kamusi yao lakini kwa huu umbeya mnashusha hadhi ya JF. Hili hapa chini ndilo tamko rasmi la Msigwa baada ya matokeo ya uchaguzi.

View attachment 3003182
Hakika Chadema imetoa somo kubwa kwa chama cha mafisadi, mambuzi na wezi wa kura wa jinsi upigaji wa kura unavyotakiwa kufanyika katika nchi ya demokrasia. Komeni kuleta ujinga wenu humu.
Ni msemo tu ukiwa muongo uwe na kumbu kumbu leo kimbukizi ya nyerere!
 
Back
Top Bottom