Mchungaji Msigwa na Joseph Mbilinyi wafungua kesi ya Kikatiba dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupinga unyanyasaji Magerezani

Ndugu yangu,
Mitazamo yako yaoneka wazi kuwa mitazamo yako ni ya ki CCM ambayo inadhani kuwa ina milki ya dola.
CHADEMA wanafahamu wazi kuwa CCM inaogopa na kuchukia harakati kwa vile (hizi) ndio huwafumbua macho wananchi wanaofanyiwa ghiliba na kukandamizwa/kunyonywa/kunyanyaswa.
Aidha, wanafahamu kuwa hakuna chama kinachoweza kuja kufanikiwa kushika dola kwa bidii za kuifurahisha CCM, kwa KUKUBALI kuchezeshwa ngoma na kuimbishwa nyimbo za kichawi/mapambio ya CCM. Wafanyao hivyo wanajidanganya na wataishia kuwa vichekesho tu hata kwako.
Uhuru, Haki na Maendeleo ya kweli.
 
tatizo hao wanaofanya hiyo shughuri ya kufungua kesi hakuna mtu atawasikiliza wataonekana wanaleta fujo tu mahakamani
Ukombozi huwa hauji wenyewe, wala kuletewa kwenye sahani.
Ukombozi hutafutwa, tena mara nyingi kwa gharama.
AMEN
 
We huna akiri kabisa. Hujui hata wewe umatetewa. Hujui kama we ni mgungwa wa kesho. Dhulma zikizidi unaweza bamvikwa kesi yoyote kama akina mdude na manji

..kuna utafiti umefanyika kujua kwamba hili ni hitaji la WAPIGA KURA walio wengi?
 

..naunga mkono harakati.

..lakini ziwe harakati zitakazoleta kura ktk uchaguzi.

..masuala ya wafungwa siyo kero au hitaji kuu la wapigakura waliowengi.

..wangetetea wakulima, wafugaji, kinamama, vijana wasio na ajira, siyo wafungwa.
 
Leo ndiyo wanakumbuka hilo baada ya Mwendazake kuondoka?
 
Mwanzo mzuri.

Tukafungie nyingine sasa ya kuzuia DEDs na staff wake kupora kazi za Tume ya Uchaguzi.
 
Magereza hayana camera za CCTV?
 
Propaganda zako, uongo ni asili yako, na hutaacha! Labda hujui kusoma, “Nikiri kuna maeneo mengi tulikuwa na wagombea sahihi, lakini kuna maeneo kadhaa tulikuwa na wagombea dhaifu, huo ni ukweli na haupingiki kwa sababu waswahili wanasema wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani," amesema Mbowe. Tunga uongo mwingine, sukumagang, mfiwa wewe!
 
..naunga mkono harakati.

..lakini ziwe harakati zitakazoleta kura ktk uchaguzi.

..masuala ya wafungwa siyo kero au hitaji kuu la wapigakura waliowengi.

..wangetetea wakulima, wafugaji, kinamama, vijana wasio na ajira, siyo wafungwa.
JokaKuu,
Walicho fanya ni sahihi kwa sababu, pamoja kwamba Labda ni wachache na Labda hawapigi kura, lakini kila mtu ana haki mbele ya sheria! Zingatia pia kuwa, hawatetei Wafungwa VS Wakulima au hao wengine! Wafungwa wakitetewa haiondowi chochote kwenye haki za hao unao taka watetewe! Pia, huyo mkulima, ama mtu yeyote ambaye leo ni mpiga kura, anaweza kujikuta gerezani kesho, baada kupigia CHADEMA kura leo!
 
Hili jambo linafahamika na wala hakuna siri, ushahidi wake uko wazi na maofisa magereza wamekiri mara kadhaa kwamba linafanyika.
Washaurini wawe wanaleta matokeo ya hukumu na sio wanapopeleka shauri kwasababu mna taarifa nyingi za kufungua kesi lakini hatupati mrejesho. Mfano, Kesi ya Amsterdam na Maria Sarungi Tsehai za The Hague zimefikia wapi?
 
Inasikitisha kwakweli
 
AMEN
 
..naunga mkono harakati.

..lakini ziwe harakati zitakazoleta kura ktk uchaguzi.

..masuala ya wafungwa siyo kero au hitaji kuu la wapigakura waliowengi.

..wangetetea wakulima, wafugaji, kinamama, vijana wasio na ajira, siyo wafungwa.
Wote watakuja fikiwa
 
..je hilo ni hitaji la watz?

..muda na resources wanazotumia kutetea wafungwa kwanini wasiutumie kutetea wakulima, wafugaji, vijana wasio na ajira, wastaafu,..

..nadhani wangetumia muda huu kujipendekeza kwa wapiga kura.
Mkuu think big,kila mtu ni mfungwa,mababu zetu wangekuwa na mawazo ya namna hii kwamba wapambane kwa masrahi yao Leo hii tusingerithi hata ngozi toka kwao.

Kama ni swala la kutetewa kwa wakulima sio lazima akina msigwa wawatetee,watetezi tunao wengi Sana,hata Mimi ninaweza watetea wakulima,na kila mtu ana kipaumbele chake ,kwa msigwa sasa ni wafungwa Kwanza

Swala la haki kwa kila mtu ni muhimu,binafsi nakubaliana na akina msigwa ,mungu awatangulie .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…