Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
"CCM naiona inaondoka madarakani. Kama mmenisikiliza vizuri hayo mambo ninayoyazungumza ni ya msingi sana. Eh, nimesema labda sikusema mwanzoni, Roman Empire ilikuwa na jeshi kubwa sana lilikuwa litifu sana, lakini Roman Empire haikuanguka kwa sababu ya kushambuliwa kutoka nje. Ilianguka yenyewe kwa sababu ikionekana vyombo zile taasisi za msingi zinatumika kwa baadhi ya watu, hata ndani ya CCM wenyewe wataanza kugombana. Kwa hiyo as a result itadondoka kama haitarekebisha haya mambo.
Lakini ukija kwenye hiyo ya kwamba fedha na nini, tawala nyingine zilikuwa na fedha, sio kwamba... Gaddafi alikuwa hana tatizo la hela, walikuwa na pesa nyingi. Sasa ukiangalia mikutano ya CCM ya hadhara yoyote inayofanyika haiko organic.
CHADEMA wanaweza wakatuma message tu, watu wanakimbia. "Palipo na mzoga ndipo wanapokusanyika tai." Katika katika life, vision attracts money. Unaweza ukawa na hela lakini huna vision. Unaweza ukawa na hela lakini hauko kwenye mioyo ya watu. Swala ni kwamba unabeba kile ambacho watu wanakitaka."
