Mchungaji Msigwa: Niliishauri CCM imuachie Lissu haikunisikiliza

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kada wa CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa, ametoa wito wa kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akidai kuwa hana hatia na kwamba amekuwa akizuiliwa kutokana na misimamo na uwezo wake wa kujenga hoja.

Akizungumza na waandishi wa habari, Julai 14, 2026, Msigwa amesema Lissu amekaa gerezani kwa zaidi ya siku 400, akisisitiza kuwa si mhalifu wala msaliti wa nchi.

Msigwa amedai kuwa viongozi wa dini, wanasiasa kutoka vyama mbalimbali, baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na jumuiya za kimataifa, wameendelea kutoa wito wa kutaka Lissu aachiwe huru.

Soma Pia: John Heche: Tusiposikilizwa, tutaitikisa nchi kwa maandamano; Lissu aachiwe huru

Msigwa amesema wakati alipokuwa mwanachama wa CCM aliwahi kushauri Tundu Lissu aachiwe huru akiamini kuwa uwepo wa upinzani imara unasaidia kuifanya hata serikali iliyoko madarakani kuwa imara zaidi.

Aidha, alisema Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola (Commonwealth) zimeendelea kuishinikiza Serikali ya Tanzania kumuachia huru Tundu Lissu.

Your browser is not able to display this video.
Via: Nuru FM
 
Peter Msigwa
 
Chura Kiziwi kwani huwana ni msikivu sasa?
 
Apo kwanza anawavuta CDM ili awe nao kwenye mfumo ikipita miez mitano anaenda kuwauza wote uko mjin ccm nayeye ataenda kustafia uko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…