Niuseme Ukweli sasa haha Yule ambaye alikuwa anaimba kuleta serikali ya viwanda ameona kwamba isingewezekana na haitawezekana
Tumekosea wapi
1.Tumeingiza siasa kwenye taaluma na Utaalamu, walipaswa wawe na mpango mkakati wa kuwashirikisha hasa wenye viwanda vilivyopo kuona ni wapi paboreshwe, lakin kinyume serikali imekuwa against Private sectors na kuona kama maadui , lazima viwanda vifungwe
2.Hakukuwa na maandalizi Thabiti ya Viwanda vyenyewe
Tulilileta kisiasa
Ilibidi kwanza tuhakikishe haya
A.Tuna nini kama Malighafi
B.Tunataka kuzalisha nini kutokana na Malighafi hizo
C.Nani awekeze katika uzalishaji huo
D.Ni nini mahitaji muhim katika uzalishaji hio na yanakidhi viwango? Yaan Umeme, Miundombinu na vingine
E.Muda tuliojipa unatosha kuyakamilisha?
F.Elimu vijana wanayopata itakidhi mahitaji ya soko la wataalamu ndani ya viwanda hivyo?
Tatizo tuna copy na Ku paste, kama Singapore na Indonesia bila kujua leo wamefikaje
Viwanda vitafungwa sana
Britannica