Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Wanaosema msitoke CHADEMA kwakuwa kuna future ni uongo mtupu, wao wenyewe hawana hiyo future

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

..hii sio hoja ngumu kujibu.

..Msigwa alipoingia Cdm alikuwa muuza mitumba.

..Cdm walimpa platform na akapanda mpaka akawa mbunge vipindi viwili.

..Msigwa alipogombea ubunge kipindi cha tatu, Ccm walimpora ushindi wake.

..Ccm ni chama cha wenye fedha. Sio rahisi mtu wa chini kujiunga nao, na kufikia ngazi, na umaarufu, aliopata Msigwa alipokuwa Cdm.

..kwa hiyo, kwa kijana anayechipukia ktk siasa, ambaye hana fedha, lakini amewiwa kutetea nchi yake, Cdm ndio chama kinachomfaa.

..kwa mtu wa makamo, mwenye fedha, anayetaka kulinda utajiri wake, au kuongeza utajiri, chama kinachomfaa ni Ccm.

..Cdm, na Ccm, vyote ni vyama sahihi, lakini sahihi kwa watu wa matabaka tofauti.

Cc Nguruvi3
 
Msigwa wewe ni kama mwanamke uliyepewa talaka na mume wako, sasa kuendelea kumzungumzia vibaya aliyekuwa mume wako maana yake bado ulikuwa unampemda na huko ulipoenda kuna vitu ambavyo huvipati.

Nakushauri tuliza akili bado safari ni ndefu sana hii, jaribu kujifunza kutoka kwa waliokutangulia, wewe siyo wa kwanza kuondoka CHADEMA.
 
Mbowe sio mpinzani kama hamuelewi basi shauri yenu ila kwa kuwa uongo, ghiliba na utapeli vina mwisho mtakuja kujua hilo.

Mbowe sio mpinzani nchi hii ni ya kuhurumia sana na Chadema kamwe haitafanya siasa yeyote au kuchukua nchi kama Mbowe akiwa pale.
Mbowe ni Mamluki anareport kila kitu.
 

..kama Mbowe ni mamluki na agent wa Ccm, kwanini Ccm haiishi kumshambulia? Si wangemuacha ili aendelee kuiharibu Chadema?
 
Tunaposema amejumaliza kisiasa ni kama hivi kubebeshwa sanamu na watoto wa uvccm hata sura yake anaonyesha amelazimishwa
 

Attachments

  • dac25c6b-05ab-4329-af3b-0497d13d1c20~2.jpeg
    47.3 KB · Views: 4
  • dac25c6b-05ab-4329-af3b-0497d13d1c20.jpeg
    151.5 KB · Views: 4
  • Screenshot_2024-07-21-09-14-46-163_com.whatsapp~2.jpg
    244.5 KB · Views: 4
Msigwa kama hujui ni kwamba ushachokwa na watanzania kwa vimaneno vyako vya kuungaunga, ww si usharudi CCM haya fanya kazi kuwaletea maendeleo wananchi. Kama hujui hicho ndicho chama kinachokusanya ma billion ya kodi kila siku, tunasubiri hoja za namna ya kutukwamua sisi watanzania katika lindi la umaskini.

Sababu tangu urudi CCM hatujawahi kusikia HOJA hata moja ya namna ya kuboresha maisha yetu sisi watanzania ambayo yapo hoi bin taaban.

CDM haiongozi dola achana nayo inakupotezea muda.
 
Hivi matatzo ya taifa hli na watanzania ni chadema? Ndiyo waliofilisi mashrika ya umma, kuua viwanda, ukosefu wa ajira, mikataba ya hovyo ya raslimali zetu nk je bwana msigwa hayo na mengneyo chanzo n chadema?
 
Ahadi yake ilikua akihama CHADEMA anahama na "rundo" la watu kutoka huko.Haikua hivyo.Kaanza kutumia mbinu nyingine ya uchonganishi?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™
 
Mimi ninavyo jua Msigwa ameenda CCM kufuata maslahi yake binafsi kwa hiyo msiwe na kazi ya kumjibu yeye asubiri mda wake ukifika apate utezi wake basi, akichapata uteuzi kama wakina katambi atanyamaza mwenyewe
 
Mimi ninavyo jua Msigwa ameenda CCM kufuata maslahi yake binafsi kwa hiyo msiwe na kazi ya kumjibu yeye asubiri mda wake ukifika apate utezi wake basi, akichapata uteuzi kama wakina katambi atanyamaza mwenyewe
Msigwa alipitiwa na dollar za Abdul, asijifanye mjanja yeye amenunuliwa kama bidhaa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…