Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Hii wadau ilikaaje? Mch. Christopher Mtikila. Msomi wa juu wa Sheria, mtu mwenye akili na ujasiri. Alisema wazi bila kuuma uma maneno. Kuwa aliyekuwa Rais wa Tanzania kipindi hicho ndugu kikwete ni gaidi.
Sielewi ile kesi alishindaje shindaje. Je ilithibitishwa kweli ikafunikwa au ilikuaje? Ni mwanasiasa pekee ambaye ameshawekwa sana ndani na kushinda kesi nyingi sana Tz.
Pia soma > Tupige kidogo ‘mastori’ ya Mchungaji Christopher Reuben Mtikila
----
Ni kwamba Mtikila alidaiwa kutoa maneno ya uchochezi na kashfa dhidi ya Rais Kikwete kwa kumuita gaidi kwa madai kuwa serikali anayoiongoza inataka kuanzisha mahakama ya kadhi, jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977
Ilidaiwa kuwa kati ya Januari mwaka 2009 na Aprili 17, mwaka 2010 jijini Dar es Salaam, kwa nia ya uchochezi mshitakiwa alisambaza kwa umma nyaraka zilizosema 'Kikwete kuuangamiza ukristo', 'wakristo waungane kuweka mtu Ikulu'
Shitaka la pili likadai kuwa
Aprili 16, mwaka 2010 eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka wenye uchochezi kwa jamii.
Nakumbuka polisi walivamia nyumbani kwa Mtikila kusaka waraka huu
Katika kesi hii Mtikila hana wakili wa kumtetea na anajitetea mwenyewe.
Kesi hiyo ilisikilizwa na mahakimu watatu tofauti ambao ni Waliarwande Lema, Sundi Fimbo
Mahakimu wawili walilazimika wajitoe baada ya Mtikila kuwakataa kwani anaamini hawana hadhi na hawawezi kumtendea haki.
Mwisho wa siku, kesi hiyo akapangiwa hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo (kwa wakati huo Elvin Mugeta) ambaye aliisikiliza Kesi hiyo na Septemba 25 Mwaka 2012 ,alitoa hukumu ya kumuachilia huru Mtikila baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha kesi yao.
Nakumbuka siku Mtikila alipotoa utetezi wake katika Kesi hii nilikuwepo.
Mtikila Kama kawaida alikanusha madai ya jamhuri uwa ule waraka wake uliokuwa na kichwa cha Habari kisemacho (KIKWETE KUANGAMIZA UKRISTO) kuwa ni wa uchochezi.
Mtikila alikubali kuwa ule waraka ni wake na aliundaa yeye na siyo wa uchochezi na kwamba hawezi Kuukana waraka ule kwasababu Kuukana walaka ule ni sawa na kumkana YESU KRISTO"
Baada ya kuachiliwa huru Mtikila akasikika akisema Haleluya!
Huku polisi wakijiandaa kumkamata tena
Kule nje polisi walipomsogelea kwa lengo la kumkamata, Mtikila akawaambia
"Nyie Polisi hamna uwezo wa kunikamata kwanza mnavyeo vya chini sana....Kama mnataka kanifungulia kesi nyingine nitakwenda Mwenyewe Kituo cha polisi kuripoti"
Mtikila akaendelea
"Hata boss wenu IGP- Said Mwema ananiita kwa heshima kwa kunipigia simu naenda mwenyewe Polisi,ebu toeni Ujinga wenu hapa"
Mtikila alisema na kusababisha watu kuangua vicheko na Polisi wale waliokuwa wamepanga kumkamata kumuacha Mtikila aende zake nyumbani.
Credit: Fortunatus Buyobe