Mch. Mwanjale ana wakati mgumu bado yuko ICU! Nguvu ya Sambwee Shitambala bado ni kubwa, wale wananhi wa Mbeya Vijijini wamekataa kudanganywa na mfano hapa juzi alipokuja Mgombea Mwenza wa CCM, Dr Bilali, wananchi wa Ilembo waligoma kusombwa kwenye malori kwenda kumsikiliza, waliendelea na shughuli zao.
Mpaka sasa kwa Mbeya, CCM wameshapoteza Majimbo ya Mbeya Vijijini na Mbozi Magharibi, labda itokee miujiza. Hayo ni majimbo ambayo CHADEMA wanao uhakika wa asilimia 80, wanachotakiwa kufanya viongozi wa CHADEMA ni kuwekeza kwenye majimbo hayo kwa kuwasaidia wagombea wao ili waweze kuwafikia wapiga kura kila kona ya majimbo hayo.