SI KWELI PreGE2025 Mchungaji Peter Msigwa ameandika kwenye mtandao wa X kuwa Wana CCM wanapitia wakati mgumu

SI KWELI PreGE2025 Mchungaji Peter Msigwa ameandika kwenye mtandao wa X kuwa Wana CCM wanapitia wakati mgumu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
MSIGWA.24.JUL2025.jpg
 
Tunachokijua
Peter Msigwa ni mwanasiasa ambaye aliwahi kuchaguliwa kuwa mbungi wa jimbo la Iringa mjini kuanzia mwaka 2010 hadi 2020 kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mnamo Mwezi Juni 30, 2024 Msigwa alijiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM NEC kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan. Msigwa pia ni miongoni mwa watia nia wa ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM.

Awali Mwezi Mei 30, 2024 Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu, alimshinda Peter Msigwa kwenye nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa.

Ipo picha ya ujumbe iliyochapishwa katika mtandao wa Facebook ukidaiwa kuchapishwa na Peter Msigwa kwenye mtandao wa X ukisema,

"Wana CCM tunapitia wakati mgumu sana wakati huu muda wa mama kushika kiti cha uraisi kwa muda baada ya Magufuli kufa umekwisha na kikatiba makamu wa Raisi haruhusiwi kabisa kugombea uraisi ila mama amegoma kutoka madarakani"


Je, ni upi uhalisia wa ujumbe huo?


Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa ujumbe huo si wa kweli ni wa kutengenezwa na wapotoshaji kwani haujachapishwa katika ukurasa rasmi wa Peter Msigwa kwenye mtandao wa X.

Aidha yamebainika mapungufu kadhaa yanayoonesha kuwa ujumbe huo ni wa kutengenezwa, mathalani katika picha hiyo haioneshi muda wa kuchapishwa, alama ya Grok, pamoja na nukta tatu upande wa juu wa kulia wa andiko husika.​
Back
Top Bottom