Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Peter Msigwa, amewataka wananchi wa Wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara, kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na chama hicho tawala, akieleza kuwa mafanikio ya sekta ya korosho ni ushahidi tosha wa uongozi imara na wenye mwelekeo sahihi.
Akizungumza Jumanne kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla, uliofanyika Tandahimba, Msigwa amesema Wilaya hiyo inaongoza kwa uzalishaji wa korosho kuliko hata mkoa wa Lindi jambo ambalo limeiwezesha Tanzania kupata zaidi ya Dola milioni 500 msimu uliopita wa mauzo.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha, amewataka wananchi kutoyumbishwa na vyama vya upinzani ambavyo amedai havina mwelekeo, wala uwezo wa kusimamia haki au demokrasia wanayoihubiri.
“Hao wanaosema haki, kwao hakuna haki. Wanaosema demokrasia, kwao hakuna demokrasia. Tanzania iko salama mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi,” amesema Msigwa.