Mchungaji wa kanisa la eagt jijini mbeya ahukumiwa kifungo cha miaka 30 na viboko 12 baada ya kubaka

Mchungaji wa kanisa la eagt jijini mbeya ahukumiwa kifungo cha miaka 30 na viboko 12 baada ya kubaka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT JIJINI MBEYA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 NA VIBOKO 12 BAADA YA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI WA MIAKA 19..!!

1.jpg

MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.



Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemtia hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).


Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.


Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shitaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.


Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana na mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.


Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimharibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani , hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha.


Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kuhusu kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.


Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.


Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.


MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.
dd.jpg

Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi
DSC00003.JPG


DSC00004.JPG


DSC00005.JPG


DSC00006.JPG

MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela


7.jpg

Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo
9.jpg

Mtoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika
10.jpg

Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika

11.jpg

Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30

x.jpg
Binti anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha



MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT JIJINI MBEYA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 NA VIBOKO 12 BAADA YA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI WA MIAKA 19..!! - GUMZO LA JIJI
 
DSC00062.JPG


Pole sana mchungaji. Utubu na Mungu atakusamehe.

Tukio hili litukumbushe kuwa tatizo la maadili lipo kwa viongozi wa dini. Wengi, hasa hawa wa Assemblies of God ni wepesi kunyoosha vidole kwa mapadre, pale Padre anapokuwa amepotoka hukimbilia kusema eti ni kwa kuwa hawaoi.

Huyu mchungaji ameoa na ni mtu mzima wa kutosha, na binti yake ni mkubwa kuliko hata huyo aliyefanyiwa kitendo hicho.
 
Huyo mchungaji tabia ya uharibifu anayo sana mwaka 1995 alimtorosha classmate wangu shule ya msingi aliyeitwa vivian
 
Hawa wapumbavu wanaojiita manabii/wachungaji/mitume wa kisasa wengi wao ni majini watu, wako tu pale kwa ajili ya utapeli na kufanya maovu kujuwa serikali haitawafuatilia. Kama tu ------- hawa na kuwanyonga. Tena huyu kwa kuwa ni kiongozi wa dini, yaani ilibidi akamatwe na kukatwa dushelele lake ili iwe fundisho kwa kina Mwingira na Mama Rwakatare pamoja na majini watu wenzao.
 
Na mzee wa upako aache kudanganya mabinti atawafungulia saloon bab kubwa akishawatumia anawaacha
 
kama wewe ni msafi, uwe wa kwanza kurusha jiwe au kumnyoshea kidole huyu mtumishi. yeye si malaika, kama kila mtu akikosea angekuwa anasemwa hivyo, hakuna ambaye angelisimama bila kusemwa. kama Mungu angehesabu maovu yetu, nani angelisimama, Mungu atusaidie tu.Mungu amsaidie huyu mchungaji jamani.
 
Huyo mchungaji tabia ya uharibifu anayo sana mwaka 1995 alimtorosha classmate wangu shule ya msingi aliyeitwa vivian

MMH, MAJANGA!!!KUMBE NI MZOEFU.AENDE JELA AKAJIFUNZE NAMNA YA KUCHUNGA KONDOO WA BWANA!!!:A S-alert1:
 
Roho inaniuma jamaniii
Hata simjui ila binti wa miaka 19 kisheria ni mtu mzima.
Mchungaji jamani,ulianzaje na unake nyumbani?
Unauchafua ukristo
 
Na mafisad wangekuwa wanafungwa hivi Tz tungekuwa kama ulaya...Mchungaji kaanzishe kanisa gerezani na utubu
 
Ni nafasi nyingine Bwana kakupatia ili ukahubiri Injili yake Gerezani..

Pole mchungaji...

Hivi hivyo viboko ni wakati wa kuingia na kutoka...? I cant wait to see anavyo charazwa duhh!!"
 
hivi hawa WACHUNGAJI WANA LAANA YA AINA GANI??

Majitu YANAPENDA KUBAKA KULIKO CHAKULA??

Duhh!

cc Ritz wabara faby Polite
 
Last edited by a moderator:
DSC00062.JPG


Pole sana mchungaji. Utubu na Mungu atakusamehe.

Tukio hili litukumbushe kuwa tatizo la maadili lipo kwa viongozi wa dini. Wengi, hasa hawa wa Assemblies of God ni wepesi kunyoosha vidole kwa mapadre, pale Padre anapokuwa amepotoka hukimbilia kusema eti ni kwa kuwa hawaoi.

Huyu mchungaji ameoa na ni mtu mzima wa kutosha, na binti yake ni mkubwa kuliko hata huyo aliyefanyiwa kitendo hicho.


we badala ya kumpa pole aliyebakwa! unampa pole MBAKAJI?

AMA KWELI WE KONDOO KWELI
 
Back
Top Bottom