Mchunguzeni huyu kwanini anaharibu maisha ya watu. Rais ikikupendeza unaweza ukamhamisha hapo TAMISEMI

Mchunguzeni huyu kwanini anaharibu maisha ya watu. Rais ikikupendeza unaweza ukamhamisha hapo TAMISEMI

Songwe Yetu

Member
Joined
Nov 22, 2021
Posts
84
Reaction score
99
Katika vitu ambavyo Katibu Mkuu wa TAMISEMI anakosea kulifanya suala la uhamisho wa wafanyakazi kwa matakwa yake amekuwa hatoi uhamisho majina ya wanaohama kwa wakati.

Mfano sasa hivi kigezo cha mtumishi kuhama ni kwa kubadilishana lakini hata hivyo amekuwa akitoa majina ya uhamisho pindi anavyojisikia.

Mpaka sasa hajatoa majina ya waalimu wanaohama nadhani umekuwa ni utaratibu wake(shemdoe) Amekuwa mkiritimba kila kitu anataka afanye yeye wenzake wanamlalamikia.

Aruhusu wafanye kazi wabadilishane vituo kwani utaratibu huu ni wa kawaida anatoka mtu anaingia mtu. Sasa yeye ndo amekuwa tamisemi master.

Wa kila kitu kuanzia mchakato unapoanza mpk mwisho, kuna wakati wa jafo watu walipiga kelele chuo kimoja cha Tanga(ekenford) na Moshi(MAMIRE TC) majina yao kuonekana sana katika ajira kwa nadhania alipoingia huyu katibu mkuu alirekebisha na alijitahidi sana katika hilo lakini suala la uhamisho nadhania analiendesha kama anaendesha familia yake maaana haiwezeka mda wa miezi 6 unatoa majina machache .

Rais Samia shugulika na huyu
 
Tatizo hamtaki kufanya kazi popote Tanzania mnataka Dar ws salaam.ukiwa mwepesi ndio ubaki Pwani na Morogoro.
Fanyeni kazi nchi yetu sote sio kila mtu abaki dar.
Nanj kakwambia anataka kufanyia kazi Dar, utaratibu wa uhamisho ni kubadilishana sasa hataki kutoa majina kila siku kutoa sababu wenzake wanamlalamikia
 
Tatizo hamtaki kufanya kazi popote Tanzania mnataka Dar ws salaam.ukiwa mwepesi ndio ubaki Pwani na Morogoro.
Fanyeni kazi nchi yetu sote sio kila mtu abaki dar.
Utadhani popote unapajua. Hii nchi ni ngumu sana kuishi sehemu ambazo huduma za kijamii ni shida
 
Katika vitu ambavyo Katibu Mkuu wa TAMISEMI anakosea kulifanya suala la uhamisho wa wafanyakazi kwa matakwa yake amekuwa hatoi uhamisho majina ya wanaohama kwa wakati.

Mfano sasa hivi kigezo cha mtumishi kuhama ni kwa kubadilishana lakini hata hivyo amekuwa akitoa majina ya uhamisho pindi anavyojisikia.

Mpaka sasa hajatoa majina ya waalimu wanaohama nadhani umekuwa ni utaratibu wake(shemdoe) Amekuwa mkiritimba kila kitu anataka afanye yeye wenzake wanamlalamikia.

Aruhusu wafanye kazi wabadilishane vituo kwani utaratibu huu ni wa kawaida anatoka mtu anaingia mtu. Sasa yeye ndo amekuwa tamisemi master.

Wa kila kitu kuanzia mchakato unapoanza mpk mwisho, kuna wakati wa jafo watu walipiga kelele chuo kimoja cha Tanga(ekenford) na Moshi(MAMIRE TC) majina yao kuonekana sana katika ajira kwa nadhania alipoingia huyu katibu mkuu alirekebisha na alijitahidi sana katika hilo lakini suala la uhamisho nadhania analiendesha kama anaendesha familia yake maaana haiwezeka mda wa miezi 6 unatoa majina machache .

Rais Samia shugulika na huyu
Utaratibu huu ukome, unajenga ukabila tu, watu wanarudi maeneo ya makabila yao ya asili, watumishi wanakuwa restless, wanasumbua viongozi Kila mara kutaka kuhama, wanapunguza juhudi za kazi
 
Katibu Mkuu TAMISEMI yupo Vizuri, LAKINI hawezi kumridhisha kila mtu kulingana na Matakwa yake
 
Mimi nilikua sina mpango wa kusoma nje ya Dar.

Nikapelekwa Makete kijiji kinaitwa Mwakauta wageni tukawa tunatamka Mwakavuta. Nikawa nalalamika, Baba akaniambia kwamba kuhamisha wanafunzi kutoka sehemu A mpaka Z ni mpango ulioasisiwa na Mwl. Nyerere ili kufanya muingiliano uwepo miongoni mwetu.

Nikapendezwa na maelezo nikaona nitapambana.

Nikafika Mwakavuta, walimu 6 walioripoti pale ndani ya wiki wote waliondoka. Hapa namaanisha walitoroka, tangazo kwenye redio linasikika kila jioni likiwaambia wasiporudi ndani ya wiki na kazi watakua wamekosa kabisa.

Mwalimu wa somo la kiingereza nilimuona mara moja miezi 2 ya kwanza alikua anashinda Mbeya.

Huduma za kijamii ni za hovyo au hakuna.

Baridi ni kali mno mpaka theluji na mabarafu yanaanguka.

Hospitali nzuri ni Ikonda, ipo umbali wa masaa mawili mpaka matatu.

Pamoja na kwamba nilihama ila hii tabia ya kubadilishana inaua idea ya umoja na kukomaza ukabila. Serikali ijaribu kuweka huduma katika viwango vya kuridhisha kabla haijawa inawapost watu maporini.
 
Shemdoe utakuwa unamuonea tuu ni mtu mmoja poa sana.

P

Brother pascal uyu shemdoe hakuna kitu majuzi kati hapa ofisi yake ilitoa agizo kuwa halmashauri ambazo zimechukua walimu mashuleni nakuwapeleka ofisi za halmashauri kufanya majukumu mengine warudi Mara moja kwenye vituo vyao vya kazi ili kuziba gape la upungufu wa walimu mpaka mda huu nakwambia Kuna baadhi ya halmashauri wametii agizo Hilo kwa ubaguzi wale walimu ambao hawana connection wamerudi kufundisha wale wenye connection wamebakia maofisini unajiukiza hivi tamisemi hawafutilii agizo lao limetekelezwa kiasi gani yani Kuna vitu unaona unasema ukija kuandika humu itaonekana unataka mchona mtu

Kupitia Uzi huu wafanye ufutiliaji woane Kuna watu wamekomaa ofisi za halmashauri uku watoto mashuleni hawana walimu
 
Private kwenyewe watu hawahami hami hovyo.
Hutaki kaishi unapotaka bila ajira waachie wanaoweza kufanya kazi hapo.
 
Huyu jamaa hata ajira bado kuna shida wanaachwa wahitimu wa nyuma wanachukuliwa wa mwaka Jana masomo hayohayo
 
Tatizo hamtaki kufanya kazi popote Tanzania mnataka Dar ws salaam.ukiwa mwepesi ndio ubaki Pwani na Morogoro.
Fanyeni kazi nchi yetu sote sio kila mtu abaki dar.
Hilo ndilo tatizo kubwa. Akienda kuomba kazi anaweka mikono nyuma na kusema atafanya kazi kokote ndani ya Jamhuri ya Muungano. Akipangiwa Namanyere ama Mtambaswala, anaenda kuripoti anachukua hela kisha anasingizia anaumwa figo na daktari wake yupo Muhimbili hivyo ahamishiwe Muhimbili!
Wanataka KM awe anatoa majina kila siku? Nadhani anafanya vyema ili kwanza aangalie idadi ya wanataka kuhama kwa kubadilishana ili atoe majina mengi kwa wakati mmoja badala ya kutoa majina kila siku.
 
Tatizo hamtaki kufanya kazi popote Tanzania mnataka Dar ws salaam.ukiwa mwepesi ndio ubaki Pwani na Morogoro.
Fanyeni kazi nchi yetu sote sio kila mtu abaki dar.
Waambie hivyo viongozi wako wanao wekeza kila kitu dsm kama ndio tanzania pekee..kwahiyo watumishi wenyewe ndio mafala wakake huko maporini.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom