Mchuzi wa mayai!

hahahaa...... Kaizer mumuwache mume wangu, ananenepa kwasababu namtunza, ukiona umeoa halafu huna mabadiliko kimwili bora uvunje ndoa!

Cc: DEMBA, Arushaone beibi wakuwache nakupenda jinsi ulivyo atii!

atapasuka huyoo afu sijui kama unaijua theory ya unene na size jamani.
 
Last edited by a moderator:
hii tamu sana amu
ila mie napenda mayai niyavurugie humohumo kwenye sosi...weeee na mkate banaa
 
Last edited by a moderator:
Huo mchuzi umenikumbusha zamani mama alikua akitupikia. Ila mayai hukata vipande viwili kwa kila yai. Si Unajua tena mambo ya bajeti. Apo alikua akikosa nyama au samaki ndo hutupikia ivo. Ni kweli mtamu hata kwa wali unaenda poa.

Hata soup ya nyama ukiweka na mayai ya kuchemsha pia inakua poa, unaweka na njegere kdg ni safi sana pia. Tena kama utapata mbuzi ndo inakua tasty
 

hata pilau la mayai ni tamu sana
 
hii tamu sana amu
ila mie napenda mayai niyavurugie humohumo kwenye sosi...weeee na mkate banaa

mpenzi ya kuvuruga nlidowea kwa jirani jumapili ila akantibua hakuyatendea haki loo jamani kupika kazi tena shurti utulize akili na makalio
 
Last edited by a moderator:
Hii simple sana napika weekend hii ila mi takula na biriani sio mkate kama ww.
 
mmh jamani amu hebu poooo kwanza pilau la mayai ndo linakuwaje hilo?

siku nkipika ntakuwekea uone mpenzi yaani ni kawaida tu hauweki nyama we unapika pilau bubu bila nyama ile ukitaka kufunikia unaweka mayai ya kuchemsha katikati daaaamn tamu balaa afu upate na juice ya chungwa au mixer mango na passion mweee umpikie Kaizer usisahau kudondoshe yale maji yetu
 
Last edited by a moderator:
unatutesa wengi sana
cc amu
 
Last edited by a moderator:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…