Mchuzi wa yai: Hufaa kuliwa na wali, mabachela unawahusu

Mchuzi wa yai: Hufaa kuliwa na wali, mabachela unawahusu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Vyuma vimekaza, hii ni njia rahisi ya kupata balanced diet yenye protein. Ni mlo wa mayai mawili. Mods si kuona jukwaa la mapishi.

Kata kitunguu, nyanya, hoho, uviweke sehem tofauti kwenye sahani.

kaanga kitunguu mpaka kuwe na rangi ya hudhurungi, weka nyanya acha ziive, weka hoho usiiache iive, ni nzuri kuliwa ikiwa crunch.

Vunja mayai uyamimine kwenye mchanganyiko huu bila kuyapiga. Acha yaive bila kukoroga mpaka ya settle.

Ukiyapiga au kukoroga yana kuwa kama matapishi. Unaweza kuweka maggi na chumvi kidogo kuleta ladha.

Nilifundishwa na shost m-Ghana enzi za mchacho wa shule na tulikula mboga hii na wali.
 
HHaha,jana dem,wangu huko yaan analalamika,et kajisahau kuzima jiko la gas alikua anachemsha maj ya kunywa had maj yame evaporate yamebak nusu.hahaha,yaan kalalamika,had anataka kulia,hahahah
 
HHaha,jana dem,wangu huko yaan analalamika,et kajisahau kuzima jiko la gas alikua anachemsha maj ya kunywa had maj yame evaporate yamebak nusu.hahaha,yaan kalalamika,had anataka kulia,hahahah
Ninaelewa pale unapojua budget ya gas iko sorted.

Ingekuwa dada wakuu amefanya hayo?😳
 
Umenikumbusha mbaali sana mkuu , huu msosi nimeila sana enzi hizo
 
Yaani kweli mTanzania umeenda kufundishwa hii mboga na mGhana?

Anyways social status matters, coz watu wengi wenye background ya kawaida na ile ya chini hii mboga ni lazima uijue, hii na dagaa wa kukaanga
 
Mie nilifundishwa pishi hili na dada furani hivi alikuwa best wangu mno... Ni mboga simpo sana kuiandaa.
 
Kichuo chuo.
Nilikuwa nanunua trei moja.
Na superget tatu..
Napiga mvurugo wa mayai na tambi kifuko nusu..inatosha breakfast mpaka dinner ..
Uvunguni nina dagaa wamejaa rambo, pembeni kuna dona nusu kiroba.

Hapo nikirudi home shavu dodo.
 
Kipindi hki ugali na wali maharage vinakuaga na ladha moja tamu kuliko ukivila December au November..hapa naona madamu kaongezea vionjo yan grisi ikizid kupotea ndio utagundua aliesema innovation is life alikua anatusema.
 
maggi...inapatikana wapi hapa dar, nishazunguka sana natafuta, ndo kwanza naulizwa ndio nini hicho
 
Na ile ya kuyachemsha kwanza alafu unayamenya , unaweka sufuria jikon ,mafuta ,nyanya ,kitunguu, unaacha viive alafu unayaweka Yale mayai ulikua umeyachemsha unaacha hadi viive vyote
Unaweza kula na wali tamu sana
 
Back
Top Bottom