Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Licha ya Serikali kulifungia Kanisa la Christian Life (CLC), lililoongozwa na Dominique Dibwe maarufu kama ‘Kiboko ya Wachawi’, imebainika kiongozi huyo wa dini anaendelea kutoa huduma hiyo, huku akiomba mamilioni ya fedha kwa waumini wake.
Tofauti na awali, Dibwe ambaye ni raia wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo (DRC) kwa sasa anatoa huduma ya maombezi na kile anachokiita uponyaji kwa njia ya simu, akiomba kulipwa mamilioni hayo kwa waumini wenye matatizo.
Kwa sababu hiyo hiyo ya kutoza fedha kuanzia Sh500,000 kwa waumini wake ili awape huduma ya uponyaji wa kiroho, ndiyo iliyoifanya Serikali ilifutie usajili wa kanisa lake, Julai 25, 2024.