Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akizungumzia umuhimu wa kuwa na Watu wanaohusika na suala la uhakiki wa taarifa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema “Uwepo wa Wadau kama JamiiAfrica unahitajika kutumika kusaidia kutoa elimu ya Uhakiki wa Taarifa kama ambavyo wamekuwa wakifanya (kupitia JamiiCheck.com).”
Ameongeza “Tunahitaji Wadau aina ya JamiiAfrica waongezeke kusaidia kukabiliana na Taarifa Potishi hasa wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, kwani kupotosha Sera, Ilani au Taarifa za Watu wakati huu tunapoelekea katika kampeni kunaweza kuwa na madhara makubwa.”
Amesema hayo wakati akizungumzia ujio wa Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Habari Afrika unaoandaliwa na MCT kwa kushirikiana na Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA), Umoja wa Mabaraza ya Habari ya Afrika Mashariki (EAPC) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Pia soma ~ Rais Samia aalikwa kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Habari Afrika utakaofanyika Julai 14 – 17, 2025