Mdada, ukiachwa achika!!

Mdada, ukiachwa achika!!

Wadada wengine aibu hawana. Umemuacha mwanaume wakati amepoteza kipato na haitoshi ukamsaliti tena wazi wazi kila mtu anaona!

Kaka wa watu amejipiga ameinuka tena, unarudi na blah blah eti nakupenda sijawahi kukutana na mtu mwenye mapenzi ya kweli mvumilivu mpole kama wewe. Wakati unamsaliti unamuacha ulikua huyajui hayo?!!

Mwanaume amekublock sehem zote bado unatumia rafiki zake wakuombee msamaha! Kuna wanawake hawana aibu!!

Unaambiwa mwenzako anaoa mwezi wa nne na tarehe ya harusi umeambiwa lakini bado huchoki kutuma watu wakuombee msamaha!! Mbaya zaidi meseji unazotuma zinamfikia mke wake mtarajiwa!! Kwani wanaume wameisha mpaka uwe king'ang'anizi namna hii?

Ulisema wa nini wezako wamemchukua, wahuni wamekuchezea wamekuacha solemba unarudi na gia ya kulia lia eti haikua akili yako ulilogwa 🤣🤣 muwe na aibu ukiachwa achika maisha yaendelee mbona wanaume wapo wengi tu!!
Mwandiko wa mke mtarajiwa huu, ila dada king'ang'anizi, hebu achika basi.
 
Mnaambiwa kaane mbali na watoto wakike waliolelewa na single mother hamuelewi acha yawakute!
 
Back
Top Bottom