Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,324
Kwa faida ya wengi Ningependa niweke maneno mazito sana yaliyoongewa na Kijana wa BINO, aliyelelewa kwa kulishwa Kitei na Chui lililokuwa linapikwa na Mzee Lukumay na kijana wake Erasto. Huyo Ni TUNDU LISU.
``Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya Rasimu ya Muswada hayakubaliki kwa sababu yanaweka mchakato wa Katiba Mpya kwenye huruma na/au fadhila ya Rais wa Zanzibar na siasa za Zanzibar kwa ujumla. Kwa mapendekezo haya, Rais wa Zanzibar asipokubaliana na jambo lolote linalohitaji ridhaa yake basi mchakato mzima utasimama au kusitishwa. Aidha, endapo katika kura ya maoni inayopendekezwa, theluthi mbili ya Wazanzibari hawatakubaliana na Katiba Mpya basi Katiba hiyo haitapitishwa hata kama inakubaliwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Tanzania Bara.
Mustakbala wa taifa letu hauwezi kuwekwa tena rehani kwenye siasa za Zanzibar na kwenye matakwa ya Wazanzibari kwa kiasi hicho. Kuhusiana na jambo hili, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba Rais wa Zanzibar ahusishwe tu katika masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Nje ya masuala hayo, Rais wa Zanzibar hana sababu yoyote ya kuhusishwa na mchakato wa kikatiba unaohusu mambo ya Tanzania Bara."
Aidha, wajumbe wa Tume ya Mapitio ya Katiba ambao watatoka Zanzibar wahusike tu katika mchakato wa masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Vile vile, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza wananchi wa Zanzibar washiriki katika kura ya maoni inayohusu mfumo mpya wa Muungano tu. Hii ndio kusema kwamba, kama vile ambavyo viongozi, wawakilishi na wananchi wa Tanzania Bara hawajashirikishwa katika mchakato wa kikatiba wa Zanzibar kwa sababu ulihusu mambo yasiyokuwa ya Muungano, vivyo hivyo viongozi, wawakilishi na wananchi wa Zanzibar wasishiriki katika mchakato wa kikatiba wa mambo yasiyokuwa ya kikatiba kwa upande wa Tanzania Bara.``