Mkuu Pasco, Nashukuru sana kwa mchango wako mzuri.
Tangu uhuru mpaka hapa tulipofikia, CCM ndio imetifikisha hapa, na hapa ndio mwisho wa uwezo wa CCM!, nikimaanisha "CCM CAN NOT DO ANYTHING MORE THAT WHAT IT CAN"!, kwa maana hiyo ninamaanisha ili taifa liweze kusonga mbele, CHANGES are innevatible, unless tunaendelea kukubali kupiga mark time hapa tulipo!
Nakubaliana na proverb kwamba:
A Man Can Do No More Than What He Can pamoja na application yako Ki- CCM. Lakini Je, na wewe unakubaliana na Mimi kwamba
CCM Does What It Can, and Chadema Can Do What CCM Will?
. kwa maana hiyo ninamaanisha ili taifa liweze kusonga mbele, CHANGES are innevatible, unless tunaendelea kukubali kupiga mark time hapa tulipo!
Nakubaliana na wewe kwamba Changes are INEVITABLE, ndio maana vuguvugu la M4C kwa mtazamo wangu lazima litazamwe kwa umakini sana kwani linaweza kuzaa mabadiliko ya aina mbalimbali, mengine ambayo pengine hayakutegemewa lakini yote itategemeana na maamuzi ya UMMA juu ya aina ya Mabadiliko wanayotaka na Mbinu sahihi za kuwafikisha huko. Kwa mtazamo wangu, M4C ni amsha amsha ili wananchi wajue nini kinaendelea katika maisha yanayowazunguka huku ikiamini kwamba Once wakitambua hilo, Aina ya Mabadiliko Na Mbinu sahihi za mabadiliko, yatabaki kuwa Chaguo lao UMMA wenyewe. Ndio maana napenda kusisitiza tena kwamba kwenye mdahalo huu, sina maana kwamba Chadema inataka kuleta mapinduzi ingawa kama tunakubaliana na Aristotle kwamba Mzazi wa Mapinduzi ni Ufukara na Uhalifu, na pia kama maneno ya Mwalimu Nyerere kuhusu nchi kufikia hatua kama VOLCANO inayochemka, yanatuingia vizuri, basi tusije shangaa kuona siku moja M4C inageuzwa na UMMA kuwa daraja la kuleta mabadiliko Very Radical.
CCM inayo nafasi ya ku proove kwa umma wa Watanzania kuwa bado inao uwezo wa kuleta reforms kwa njia ya change for the better, ikiwa na something in the hand to show kuwa I did, this, I did that, such that if elected again, I can do this and that!. "a bird in the hand, woth two in the bush"!. Yaani kwa CCM "moja shika sii kumi nenda rudi"!. CCM ndio huyo ndege mmoja, anacho cha kuonyesha!, Chadema haina kitu cha kuonyesha isipokuwa ahadi kuwa nikipewa nchi, nitafanya hili na kile!, but with nothing to show, hivyo CCM hapa ndio yenye advantage!.
Chadema nayo kwa upande wake, kupitia M4C, inao mtihani mgumu, wa kuwa convince Watanzania kuwa kwa kipindi cha miaka 50, CCM imeshindwa kuondoa wale maadui wetu watatu wa ujinga, umasikini na maradhi, on top of that, imeongeza maadui wengine wawili, rushwa na ufisadi, hivyo CCM hata ikipewa miaka 100 mingine ya kuendelea kutawala, haitaweza kubadili chochote kwa sababu hapo ilipofika, ndio mwisho wa uwezo wake!. "CCM CAN DO NO MORE THAN WHAT IT CAN"!.
Nakubaliana na wewe kwamba CCM ina advantage kwa sababu inaa mambo mengi ambayo inaweza yaweka mezani na kuwaambia wananchi kwamba tumefanya hiki na kile huku Chadema wakiwa hawana kitu. Nadhani huu ni ujumbe muhimu kwa Chadema na wanaufahamu vizuri lakini hawaufanyii kazi ipasavyo. Chadema inatakiwa waanze kutumia studies na research zilizojaa chungu nzima za wataalam mbali mbali wa ndani na nje ya nchi zinazoelezea kwa ufasaha juu ya nini kifanyike kutokomeza umaskini Tanzania. Vile vile Chadema pia ni muhimu waunde idara ya utafiti na takwimu ili isimamie kazi hii kwa ufasaha. Vinginevyo kutegemea Ilani zinazotengenezwa Board Room kwa wiki moja haisaidii kitu, ndio maana ilani za kila chaguzi zinapishana. Vinginevyo umaskini wa wananchi upo persistent for 50 years same enemies wa Maendeleo Ujinga, Maradhi, Umaskini, hivyo ideas to resolve this predicament ought to be consistent, sio flip flaps kila chaguzi kupitia Ilani. This is where research comes handy.
Kitu kingine muhimu pia ni kwa Chadema waanze kutumia M4C kama FACT FINDING MISSION, kama vile Mwalimu alivyofanya katika ziara zake vijijini mara tu baada ya uhuru - alipomuachia Kawawa uongozi wa nchi; Aliyoyasikia na kuyakuta huko vijijini yalichangia sana kuanzishwa kwa sera ya Ujamaa; Chadema waendelee kutumia M4C kuamsha wananchi ili waelewe mazingira yao na haki zao za kisiasa, kiuchumi na kijamii, lakini pia watumie fursa hiyo kutambulisha potential candidate (s) wa 2015 kwani muda wa kutembeza mgombea hautatosha;
Lakini muhimu zaidi, ni suala la Fact Finding Mission, na wawe wanarudi kila mara kwenye drawing board na kuchanganya uhalisia wa mambo on the ground na tafiti nyingine mbalimbali kuhusu hali za maisha ya wananchi mkoa kwa mkoa/kanda kwa kanda, na mapendekezo mbali mbali ya wataalam jinsi gani umaskini unaweza punguzwa iin PRACTICE, kwani mawazo haya Watawala wengi chini ya CCM wanayapuuza; Chadema wakifanya haya na wakirudi kwenye Kampeni na kuuza sera zao na mipango yao mbadala, wata connect vizuri sana na UMMA, kwani Umma utagundua kwamba kumbe Chadema wanajua matatizo yetu na wana mapendekezo mengi ya kitaalam ambayo yamejaribiwa kwenye jamii zinazofanana na sisi huko Latin America au South Asia, na majaribio haya yamezaa matunda huko;
2010 Taanzania ikiwa na population ya watu milioni 40, eligible voters were 25 milions. Waliojindikisha ni 20 milions. Waliopiga kura ni 8 milions, walioichagua CCM ni 6 milions!. Ukisoma website ya CCM, wanajitapa wana wanachama milioni 6!, hivyo CCM ilichaguliwa na wale wana CCM milioni 6 suppose wote walijiandikisha na kupiga kura!. 2015 tutakuwa milioni 50, eligible voters milioni 30!. Nimewashauri Chadema, kuwa M4C iachane kabisa na CCM!, ijikite kuzitafuta zile kura milioni 20 ambazo CCM haiwezi kuzivuna ili tupate mabadiliko kwa njia ya amani kupitia ballot box!.
Upo sahihi katika hili; Mdau mwenzetu Mkandara pia aliwahi jadili suala hili vizuri sana pale alipohimiza kwamba
Operesheni ya Vua Gamba Vaa Gwanda ina mapungufu kwani inalenga wanachama wa CCM, badala ya Wapiga Kura. Na mimi naomba niongezee kwamba:
Chadema inatakiwa kufahamu kwamba watanzania wengi zaidi (voters) bado wapo in the swing column in terms of kuunga mkono between Chadema na CCM, kwani jumla ya wanachama HAI wa vyama vyote vya siasa kumi na tisa (19) Tanzania sidhani kama inafika hata milioni kumi. Tukirudi kwenye hoja ya Mkandara, nakubaliana nae kwani - wanachama wa CCM ni kama milioni saba, wakati wapiga kura kwa mujibu wa database ya 2010 wapo milioni kumi na nane. Hii ina maana kwamba katika Operesheni Vua Gamba, Vaa Gwanda, Chadema inalenga less than one third ya wapiga kura Tanzania i.e. about 27% - kwani inalenga wanachama wa CCM zaidi au pengine inaamini kwamba hakuna Wapiga Kura huru wengi, badala yake ni lazima mpiga kura kwanza awe na mapenzi na CCM hata kama sio mwanachama wakati hii si kweli kwani kwa Tanzania ya leo, Utambulisho wa Watanzania wengi kwanza ni
Wapiga Kura, suala la uanachama wa vyama vya siasa ni secondary;
Kwa mwenendo wa demographics za sasa Tanzania, haitakuwa ajabu wapiga kura mwaka 2015 wakafikia hata milioni 22. Pia ni dhahiri kwamba by 2015, wanachama wa CCM watapungua pengine kufikia milioni tano, nne or less kutokana na ukweli kwamba CCM inazidi kupoteza mvuto kadri siku za kuelekea 2015 zinavyozidi kuyoyoma. Sasa tuseme kwamba wanachama hawa wa CCM by 2015 wapungue kufikia milioni nne kati ya jumla ya watanzania wapiga kura tuseme milioni 22, ina maana Vua Gamba, Vaa Gwanda itakuwa inalenga only 18% ya wapiga kura kuelekea mwaka 2015.
Tuseme Chadema manages to secure wapiga kura wake wa uchaguzi mkuu uliopita (2010) i.e about 2.5 million; na tuseme kwamba Chadema inafanikiwa kuvuna 25% ya wanachama wa CCM ambao tusema watabakia Milioni nne (2015) ambao ni sawa na wanachama milioni moja; na tuseme Chadema inafanikiwa kuongeza wanachama wengine milioni mbili kutoka katika column ya independent voters katika kipindi hiki cha miaka mitatu heading towards 2015, ina maana Chadema itaingia 2015 ikiwa na supporters wa uhakika between 5 and 6 million.
Je Kura hizi zinatosha? HAPANA. Idadi hii itakuwa ni less than one third ya wapiga kura wa 2015 i.e only 27%. Je, ikitokea CCM ikaweka mgombea 2015 ambae ataleta mvuto kwa wapiga kura kama ilivyotokea 2005, Chadema itavuka? HAPANA.
Hata CCM ikiweka mgombea mwenye mvuto wa wastani tu, ili mradi UMMA umeshalisikia jina lake, kwa kanuni ya mshindi ni mshindi, CCM kupata ushindi wa 50.1% dhidi ya Chadema 49.9% ni kitu kirahisi sana, hivyo CCM kuwa mshindi wa kiti cha Urais 2015. Ushindi wa Chadema sana sana, May Be
(MAY BE), itakuwa ni kualikwa na CCM kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutokana na godo performance huko majimboni, suala ambalo litakuwa ni msiba kwa Chadema Kisiasa kwani Chadema wameshalitolea msimamo suala hili rejea ndoa baina ya CUF na CCM 2010 Zanzibar. Mbaya zaidi ni jeraha linaloweza kutokea kwenye demokrasia yetu kwamba Chadema wakikataa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Propaganda dhidi ya Chadema kwamba kimekataa ridhaa ya 49.9% ya wananchi itakuwa ni mzigo mkubwa sana kwa Chadema kisiasa; Hii ni changamoto kubwa sana kwa Chadema, na inaingia katika hoja yako kwamba Njia kwa Chadema 2015 ni Nyeupe lakini HAWAJAJIPANGA.
Zile singles za "list of Shame", ufisadi, rushwa, etc, by 2015, zitakuwa zimeisha shuka kwenye chart ya top of the pops. 2015 Wanzania wanahitaji hit single za Tukiichagua Chadema, tutapata nini tofauti na hiki tunachopewa na CCM, concentrations isiwe just change and replace CCM with Chadema, bali lets replace CCM with Chadema because CCM imeshindwa kufanya ABCD kwa sababu ya sera zake mbovu (failed policies),ABCD na Chadema wao wakiingia, watafanya ABCD kwa kutumia policies ABCD na resources from ABCD!.
Nakubaliana na wewe katika hili ingawa kila ninaposema kwamba Suala la Ufisadi ni suala la Mpito, tafsiri inayotolewa ni mbaya. Lakini naomba hapa nipingane na wewe pale ulipowahi kusema kwamba Hoja ya Ufisadi sio Hoja ya Kuwakomboa Watanzania; Mimi nadhani ni hoja ya kuwakomboa watanzania lakini isijitegemee na badala yake izungumziwe katika mazingira uliyoainisha hapo juu in blue.
Kwa mliongalia mjadala wa jana US, sisi pia tutatamani kuwapima vagombea wetu kwa utaratibu huu, na tuweke mecchanisim lazima wagombea washiriki debate, sio options bali a compulsory ili kuwapima, tupate kiongozi bora na sio bora kiongozi!.
Nilitazama debate na Obama didnt perform well, lakini huo ni mjadala mwingine. Suala la msingi hapa ni umuhimu wa midahalo katika kampeni/chaguzi zetu; Kwa sababu fulani fulani, CCM ni waoga wa midahalo, na hii ni weakness kubwa sana ambayo itakuja kuimaliza CCM mchana kweupe. Tatizo la CCM ni kwamba wameamua kuingia Siasa za ushindani Defensively, wakati wakiamua kujipanga vizuri kuna ya ku Attack kihoja (sio kiviroja). Suala la midahalo kukataliwa na chama lipo hata katika chaguzi za ndani - kuteua wagombea ubunge na udiwani, midahalo au mijadala inayohusu uwezo, mapugufu, na mitazamo ya wagombea haipewi nafasi kwa hoja kwamba Wote Mle ni wana CCM hivyo wakianza kutofautiana, upinzani utapata hoja za kutumia majukwaani. CCM sio chama kinachoheshimu mawazo huru na demokrasia kama wengi wanavyofikiri, na ndio maana kuelekea 2015, kinajijengea mazingira ya kuwa Chama cha WAFU.
Mwisho mkuu Pasco, nashukuru kwa kunipa compliment kuhusu michango yangu yenye value ya shilingi laki Tano; Serioudly, kama una sehemu ambazo unajua wanapenda mijadala kama hii, na nikienda kuzungumza watanilipa hizo hela, nitashukuru kwani itakuwa ni jasho langu (sio ufisadi au ujanja ujanja wa kihujuma), lakini muhimu zaidi yaliyomo yatalenga zaidi maslahi kwa umma/taifa, sio wagombea fulani fulani au chama fulani fulani.