Elections 2010 Mdahalo - TBC Mchakato - Jimbo la Arumeru (Video)

Elections 2010 Mdahalo - TBC Mchakato - Jimbo la Arumeru (Video)

CCM wamekimbia....
Jamaa wa CHADEMA ni soo....
Anamwaga vitu vya uhakika sana kwa kila muda mfupi anaopewa
 
Utapigwa marufuku muda sio mrefu kwani unashusha hadhi ya chama. Namaanisha TBC wataacha kudahalo wagombea wa vyama
 
Duh!
huyu jamaa wa CHADEMA ni noma..amenifurahisha jinsi alivyosababisha kadamnasi kulipuka! Nadhani watu wake tayari wanamwelewa vizuri. Mungu ampe hekima, busara na uwezo zaidi..Inshallah
 
Huyu MC amemkatiza nini, maana jamaa amepeleka mashambilizi ya kumtoa mtu KO..Kumbe ndiyo sababu sisi m wako mitini!
 
Hivi jamani hawa CCM kwanini wanakimbia midaharo jamani?
Hivi kweli kwa ulimwengu huu wa sasa ni sahihi, mtu kuogoba kwenda kwenye midaharo kama hiyo jamani
Ebu wananchi jioneeni wenyewe type ya viongozi wa CCM wanatoka IFM
alafu naomba kama inawezekana tuwaadhibu kwa maamuzi yao
eeeh Mungu baba saidia jamani hawa watu wakose jamani.

Samahani, ni 'mdahalo.'
 
Kura zenu zote wananchi wa arumeru mashariki mpeni mbunge wa chadema,kwa sababu hizi ni makini,smart,analielewa jimbo na matatizo yake.huyo ni mkiongozi makini
 
Wananchi wa arumeru mashariki kura zenu pelekeni chadema kwani sababu mnazo
 
hizi thread zinahang tuuu.... huweki sababu, unadhani kila mtu anaishi arumeru na anajua kinachojiri??

please be fair to the forum
 
Kura zenu zote wananchi wa arumeru mashariki mpeni mbunge wa chadema,kwa sababu hizi ni makini,smart,analielewa jimbo na matatizo yake.huyo ni mkiongozi makini

Broda,

Ungewarahisishia sana wananchi wa Arumeru na sisi wasomaji hapa kama ungeweka na jina lake huyo mgombea wa hicho chama!

Lakini yaonyesha we bado ni mgeni hapa....karibu sana!....usiogope tutafika tu!
 
hizi thread zinahang tuuu.... huweki sababu, unadhani kila mtu anaishi arumeru na anajua kinachojiri??

please be fair to the forum
Akikua ataacha!
 
Aisee, huyo dogo wa Chadema ni noma! Namtakia kila la kheri. Nadhani tunahitaji vijana kama hawa bungeni wapiganie haki zetu.
 
The content of the video is enough material to lead a discussion. Video hii ni ya kipekee ndio maana nikaiweka. Tazama then changia. Mkitaka synopsis ningeweka text kutoka gazetini.
 
Uamuzi wa makamba kuwakataza wabunge wasishiriki kwenye mdahalo unaweza kuwaangamiza kwa maana
ccm aikuweka wananchi kufadika kwao na mdahalo wamefikiria zaidi wakasahau wananchi ambao wangependa kuskia
kutoka kwao mfano mzuri huu hapa wananchi wanamaswali ambayo wangependa kumuuliza mbunge hayupo hii ni dharau kubwa sana kwa mpiga kura na that has nothing to do with opposition parties. Wabunge wa ccm ndio walikuwa madarakani kwahiyo wanawajibika kujibu maswali ya wananchi waliowatumikia na siyo kuwakimbia.
 
Swala la CCM kukimbia mdahalo silishangai hata kidogo. Wanajua makosa waliyoyafanya, wanajua kuwa wana wabunge ambao sio competent enough kusurvive kwenye midahalo. We angalia huyo dogo anavyochana, ingekuwa kuna mtu wa CCM hapo nahisi angerushiwa viti au angeomba udhuru as if anaenda msalani na kutokomea mazima.

Kuhusu huyu jamaa wa Chadema, hata kama ni wa jimbo jingine na mtu uko Mbeya vijijini, bado unaweza toa ushauri kwa wana Arumeru. Nimeicheki clip na nilipata habari kutoka kwa wadau walioangalia live kipindi, jamaa wa Chadema alifunika.

Tuache ushabiki wa kichama na twende kwenye ushabiki wa uwezo wa mgombea. Tukiishia kuangalia bendera za vyama vyetu tutachagua wataalamu wa kulala bungeni na kuuza nchi na kuishia kujaza vichwa vya vyuu vya magazeti kwa masaga kibao; mara EPA, mara Richmond n.k. Tutaishia kujaza viongozi wasioweza hata ku-analyse maswala muhimu ya nchi na kuishia kutuaibisha kwenye vyombo vya habari vya dunia.
 
Ukiona nzi wanakuandama ujue unanuka.......m, ndio maana hawataki watu watu wajue uozo uliopo. Mdahalo una mantiki kubwa kwani watu wanapokuwa kwenye pilikapilika za maisha mara pengine wanakosa muda wakuhudhuria mikutano hiyo, lakini baada ya kazi mtu anaweza kupata fursa ya kusikiliza sera za wagombea wote kwa pamoja. Shilingi imeshuka, mfumuko wa bei juu, sasa mara pengingine unakosa hiyo fursa. Pili wanawaonyesha wapigakura kuwa ni jinsi gani wasivyo wanyenyekevu kwa waajiri wao watarajiwa.
 
Broda,

Ungewarahisishia sana wananchi wa Arumeru na sisi wasomaji hapa kama ungeweka na jina lake huyo mgombea wa hicho chama!

Lakini yaonyesha we bado ni mgeni hapa....karibu sana!....usiogope tutafika tu!

Kijana anaitwa Nassari Pallangyo.
 
Mbowe, Mnyika, Mdee, Nyimbo, Lema, Nasare, Shibuda, Zitto, Ntagazwa, Lisu, Mwikwabe na wengine.... YESU WANGU! Bunge lijalo limepata wenyewe
 
Back
Top Bottom