Elections 2010 Mdahalo - TBC Mchakato - Jimbo la Arumeru (Video)

Elections 2010 Mdahalo - TBC Mchakato - Jimbo la Arumeru (Video)

Du! demokrasia nayo ina mambo sasa hao wagombea wengine mbona kama hawako tayari hata kukampeni? Wht about ubunge wenyewe???
 
Kwakuwa hata mie nilisikia, basi tusubiri wanaomfahamu kiuhakika watatuhakikishia jina la ubini.
Mkuu kwenye hiyo video ametambulishwa kama Nasare (Nassary ???) Joshua Samwel ila hapa wanasema hivi-

MKOA WA ARUSHA
ARUMERU MASHARIKI
1. JEREMIA SUMARI - ----------------------------CCM
2. JOSHUA NASARE - ---------------------------- CHADEMA
3. JOHN PALANGYO ----------------------------- CUF
4. LINDA PENIEL - ------------------------------- JAHAZI ASILIA
5. FANUEL PALANGYO -------------------------- TLP
6. CHARLES MSUYA ----------------------------- UPDP

Source.. Home
 
Mbowe, Mnyika, Mdee, Nyimbo, Lema, Palangyo, Shibuda, Zitto, Ntagazwa, Lisu, Mwikwabe na wengine.... YESU WANGU! Bunge lijalo limepata wenyewe

Mkuu hapo kwenye red nimecheka sana. Huna tena hidden Identity kwenye upande wa kabila.
 
Huyu dogo wa CHADEMA anaonekana ni mdogo wa umbile na umri lakini ana moyo mkubwa sana. Nina maanisha ana uhakika na anachokizungumza na hakika ni kada wa CHADEMA ambaye baadaye atakuwa ni nyenzo kwa chama cha CHADEMA. Hii ndiyo aina ya viongozi tunaowataka,viongozi wenye vision ya kuona mbele na kuweka mikakati ya kuleta mabadiliko kwa faida ya Watanzania wote.

Hakikka siyo sawa na CCM inayoandaa watoto wote wa vigogo kwenda bungeni na maeneo au sehemu nyingine nyeti serikalini kwa ajili YA KULINDA MASLAHI NA MADHAMBI WALIYOYAFANYA BABA ZAO. Wapo tunawaona kina Dk.Hussein Mwinyi, Ridhiwani Kikwete,Januari Makamba na wengineo. Huu ni upuuzi ambao lazima ukomeshwe siku moja.

CHADEMA wana vijana ambao hakika wameiva kifikra na kisiasa na wako tayari kuleta mabadiliko katika nchi hii. Aina ya vijana hawa ndani ya CHADEMA(kina Zitto Kabwe, Halima Mdee,Mnyika na wengineo) inaleta challenge kali sana kwa chama tawala kiasi kwamba CCM wameamua kuingia mitini kwa kuhofia challenge kama hizi.

Nawapa pole sana CCM kwa kukimbia mijadala hii tena inayoendeshwa na chombo cha Serikali TBC.
Wajue kuwa hapa hawajawatendea haki Watanzania hata kidogo. Hapa hakuna Demokrasia ya kweli. Huu ni woga wa kukimbia kujibu maswali kuhusu madhambi yao na ufisadi walioufanya huko nyuma.

Mwanzo nilifikiri kuwa kwa vile CCM wamekimbia midahalo basi TBC wangefuta kipindi hiki cha MCHAKATO MAJIMBONI lakini haikuwa hivyo. Naamini Tido Mhando aliliona hili bila shaka kwa kurejea matukio ya nyuma kama yale ya Jangwani la kwanza likiwa kugeuza Camera kuwaelekea Watazamaji ili kuficha aibu ya KUANGUKA kwa KIkwete jukwaani na siku ya CHADEMA ilipoanza Kampeni kwa kuzima Kamera kwa madai kuwa CHADEMAwalikuwa wakitukana viongozi wa CCM. Umma uliokuwepo Jangwani ulitaka kumsulubu mtangazi wa TBC Mareen Hassan Mareen kwa kuzima camera. Hakikuwa kitendo cha kiungwana na alikuwa hana sababu yoyote ya kuzima kamera kwasababu walichokuwa wanakiongea CHADEMA ni ufisadi uliofanywa na vigogo wa CCM. Hakuna mtu alitukanwa pale ulikuwa ni ukweli mtupu.
 
Back
Top Bottom