Mdahalo wa Katiba Mpya (The Way Forward)

Mdahalo wa Katiba Mpya (The Way Forward)

Wadau, tunawashukuru sana na kufuatilia kwa karibu ushauri wenu, tutashukuru pia kama mtaweza hata kujadili hapa maeneo ambayo yapewe kipaumbele kwenye mjadala huo. Tunataka tuwe wasikivu kwenu ili mjadala huu uwe wa kitaifa ili kuelekea kule tunakotaka, 'The Tanzania We Want'!
Asanteni.

Rosemary Mwakitwange

Kazi nzuri sana Rose na wadau wengine mlio andaa hii kitu.Tulikukosa kwa kweli. Nitapenda kuhudhuria.
 
Mdahalo mzuri sana kwa ajili ya mustakabali mwema wa nchi yetu. Katiba ni msingi wa Taifa lo lote.


Bwana Aweda, umekuwa ukiripoti matukio mengi in detail na sisi tulioko mbali hasa huku Ulaya tunafaidika sana na nyie! Nikuombe siku ya mdahalo huo shirikiana na MAKAMANDA kurekodi hata kama si video basi sauti mtutupie humu ili na sisi tulioko mbali msituache kwenye mchakato wa KATIBA YETU! "

NGUVU YA UMMA ndiyo msingi wa TAIFA"
 
View attachment 118040



Jumapili hii live kupitia ITV, kuanzia saa 9 - 12 jioni EABMTI itakuletea Mdahalo wa Katiba Mpya 'tunakoelekea'. wazunmgumzaji kwenye mdahalo huu watakuwa:


Mh. Angela Kairuki
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania;

Mh. Tundu Lissu (MB)
Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni

Hon. Aboubakar Khamis Bakari
Mjumbe wa Baraza La wawakilishi, Jimbo la Mgogoni Pemba,
Waziri wa Sheria na Katiba Serikali ya Umoja Zanzibar

Mwenyekiti wa Mdahalo huu: Rosemary Mwakitwange Muongozaji wa Kipindi cha TV cha Tanzania Tunayoitaka' The Tanzania We Want'

Jumapili Oktoba 27, 2013, Muda: Saa 10 - 12 Jioni
Mahali: Ukumbi wa Kivukoni, Hoteli ya Serena DSM.

Mdahalo huu utarushwa ‘live' kupitia Kituo cha Television cha ITV na Radio one
MDAHALO HUU UNALETWA KWENU NA EABMTI, School of Journalism and Broadcasting na washirika Wake.

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu.
East Africa Business & Media Training Institute | Center of Excellence
Kwa kununua meza ya matangazo wasiliana nasi kwa simu namba.

Kama una swali ungependa liulizwe tafadhali litume kupitia info@eabmti.co.tz
Kama unataka kushiriki tafadhali wasiliana nasi kwa ajili ya kupata kadi ya mwaliko.

WAANDAAJI!! Chondechonde fanyeni mfanyavyo na sisi wa ughaibuni tulioko nje ya nchi tuone kama si kusikiliza. Tunaomba mu-attach humu kama si video basi audio na sisi tujuie kinachoendelea kwenye mchakato mzima wa KATIBA YETU.

Naomba kuwasilisha.
 
WAANDAAJI!! Chondechonde fanyeni mfanyavyo na sisi wa ughaibuni tulioko nje ya nchi tuone kama si kusikiliza. Tunaomba mu-attach humu kama si video basi audio na sisi tujuie kinachoendelea kwenye mchakato mzima wa KATIBA YETU.

Naomba kuwasilisha.

MFUKUZI, asante kwa ushauri, tutajitahidi kutimiza hilo ili tusiwaache nyuma.
 
Mimi naomba niulize swali hili;

Kama katiba mpya itapatikana kutokana na rasimu ilivyo sasa, serikali tatu. Je katiba ya Tanganyika itapatikana vipi na kwa muda gani? Tukizingatia muda uliobaki kuelekea chaguzi za serikali za mitaa 2014 na uchaguzi mkuu 2015.

Kura ya maoni ya katiba mpya itapigwa kwa kutumia daftari la wapiga kura lililohakikiwa sasa au litakuwa lile la zamani 2010?
 
Asante kwa maoni mkuu, unatumia haki yako ya kikatiba.

Mimi nilikuwa naomba aulizwe Waziri wa Sheria wa Zanzibar kuwa amesema Zanzibar haikushitikishwa Katika kutoa maoni hivi karibuni wakati Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewahakikishia Wabunge kuwa Zanzibar imeshirikishwa. Sasa suali nani ni Mkweli na kwa ushahidi ipi?
 
Mh, sidhani kama huyo wa kutoka ugambani atashiriki huo mdahalo, kwa sababu hawa jamaa na midahalo havichangamani kabisa. Hata ukiwa mzuri kichwani ukiwa ugambani akili zote huwa zinabaki mtaa wa elfu saba.
 
Tunawashukuru waandaaji kwa kujua kiu ya watanzania yaani mnatupa microphone tunasema kama si kuuliza, raha iliyoje.
Ndani ya "the Tanzania we want" tunajisikia huru sana.

ninaota siku moja mtatuletea makatibu wakuu wa vyama vikubwa vya siasa nchini tuzungumze nao kwa maswali.
Big up Rosemary Mwakitwange na crew nzima.
 
Tunawashukuru waandaaji kwa kujua kiu ya watanzania yaani mnatupa microphone tunasema kama si kuuliza, raha iliyoje.
Ndani ya "the Tanzania we want" tunajisikia huru sana.

ninaota siku moja mtatuletea makatibu wakuu wa vyama vikubwa vya siasa nchini tuzungumze nao kwa maswali.
Big up Rosemary Mwakitwange na crew nzima.

Makatibu wa vyama vyote hawawezi kupatikana wote,lazima tu yule wa magambani asitokee coz atakuwa na wasiwasi wa kuulizwa maswali magumu yahusuyo tembo wetu.
 
Mbona Naibu Waziri Anjela Kairuki kaingia mitini?
 
Kairuki kaingia mitini. Chezeya Lissu weye! MiCCM inaudhi! Nape ndo asingesogea kabisaa hapo alivyo mweupe kichwani.
 
Back
Top Bottom