Mdahalo wa rasimu ya katiba mpya

Joined
Oct 23, 2013
Posts
23
Reaction score
1
Leo tena wadau wa siasa tupo Serena hotel mdahalo kujadili rasimu ya katiba mpya. Mdahalo karibu utaanza angalia ITV ama fuatilia kwenye jf washiriki Masoud Kombo,raisi wa chama cha wanasheria Zanzibar na wakili msomi. Francis Stola rais wa chama cha wanasheria Tanganyika na wakili wa mahakama kuu endelea kufuatilia karibu tunaanza

Maandalizi yamekamilika, wageni waalikwa wameshakaa kwwnye viti vyao, tunasubiri wachokoza mada ambao ni Masoud Kombo ambaye ni Rais wa chama cha wanasheria Zanzibar pia ni wakili msomi, Francis Stola ambaye ni rais wa chama cha wanasheria Tanganyika pia ni wakili wa mahakama kuu.

kama kawaida mdahalo huu unaletwa kwenu na EABMTI school of jounalism and broadcasting na washirika wake.

Mwongozaji wa mdahalo huu ni Rosemary Mwakitwange.

tafadhali fuatana nasi.
 
asanteni sana kwa kutuletea huu mdaharo bila shaka pumba na mahindi vitajulikana kabla ya kupata katiba mpya...
 
Tumechelewa kuanza bado wageni rasmi hawajafika nitawapa kinachoendelea hapa Serena Hotel ukumbi wa Kivukoni tuko pamoja
 
Maoni yangu kama mtaweza kuyafikisha huko yafikisheni kuwa: kama kweli watanzania tuna nia ya Dhati ya Muungano basi tuwe na NCHI MOJA TU na SERIKALI MOJA kinyume na hapo ni kiinimacho tu.
 
Maoni yangu kama mtaweza kuyafikisha huko yafikisheni kuwa: kama kweli watanzania tuna nia ya Dhati ya Muungano basi tuwe na NCHI MOJA TU na SERIKALI MOJA kinyume na hapo ni kiinimacho tu.
Nikipata nafasi ya kuchangia nitalifikisha wazo lako ni zuri sana hata mimi nasema bila kujadili muungano kwanza hatuta pata katiba bora kwani tunajadili katiba wakati chini kwa chini kuna mpasuko mkubwa wa muungano tuko pamoja mdahalo umeanza
 
Rose:-
leo tutaangalia rasimu kuanzia ibara ya pili kwani ibara ya kwanza tuliijadili kwenye mdahalo uliopita
 
Stola:-
ni kweli kuwa katiba ni waraka wa kisiasa, lakini katiba si ya wanasiasa, ananukuu katiba "sisi watanzania" hakuna sisi wanasiasa.

viongozi huwekwa madarakani na wananchi ili kuongoza kwa kufuata makubaliano ya wananchi (katiba)
 
Mchangiaji wa kwanza Franci Tola afafanua kuhusu katiba kwamba ni makubaliano ya wananchi wote nae Masoud aunga mkono
 
Kombo:-
katiba ni kitu muhimu sana. ni nyaraka inayopaswa kuheshimiwa sana, historia ya katiba zilizopita ni zao la viongozi wa juu, lakini sasa tumepata bahati ya kwamba lile neno "sisi watanzania" tutalifanyia kazi.
 
Hongera Dada Rosemary Mwakitwange na timu yako kwa kazi nzuri ya kizalendo.
May God bless you for that !
... Maoni yangu ni kuwa mchakato wa katiba isihodhiwe na wanasiasa au kikundi fulani cha watu kwa kutumia dhamana walizonazo.
... Katiba ni ya Tanzania kwa ajili ya Watanzania wa leo na kesho.
 
Kazi ya kutunga katiba ni kazi ya bunge maalumu la katiba ila kazi ya kutunga sheria ni kazi ya bunge hayo yamesemwa na francis Stola
 
Nashauri tuachane tu-pack tujadili muungano wakati mwingine else tutapoyeza kujadili mambo mengi matamu yaliyoko kwenye rasimu!
 
Stola:-
kazi ya kutunga katiba ya nchi ni kazi ya bunge maalum la katiba, kazi ya bunge la kawaida ni kutunga sheria.

wabunge wameapa kuitii katiba ya zamani ikiwa ni sehemu ya utendaji wa kazi zao ambazo ni pamoja na kutunga sheria ya kuandika katiba mpya.
 
Kombo:-
sheria yoyote ambayo haijapingwa mahakamani na kupata tafsiri ya ubatili, itabakia kuwa sheria halali.

changamoto za wingi wa wabunge kuathiri mchakato wa upitishaji wa katiba husika.
 
Swali:-
miiko ya uongozi wa umma, je rasimu hii inatibu jeraha la manung'uniko ya jamii kwa viongozi?
 
Kombo:-
Ni kweli maadili ya baadhi ya viongozi inanyooshewa kidole, na rasimu inaonekana inaweza kukidhi kwa kiwango fulani.
lakini hakuna vifungu vinazuia wabunge hata wakitamani kuvibadilisha wasijaribu.
iwe ni lazima kwa viongozi wa umma kuitii katiba.
ibara ya 20:2 kiongongozi wa uma hapaswi kutoa siri za serikali
kutoa au kupokea rushwa,
kusema uongo ama kutoa taarifa zisizo za kweli
n.k.
 
Tuko kwenye ibara ya pili MIIKO YA UONGOZI WA UMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…