Elections 2010 Mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Bukoba mjini unaendelea

Elections 2010 Mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Bukoba mjini unaendelea

swali kwamba uliwahi kutuita wananchi na kutuambia umetuletea cheki ya pesa ulizopewa Japan sh 200 milioni na ukassema unazikabidhi kwa mkurugenzi manispaa je hizo pesa zilitumikaje?
 
Swali za bei kuwa juu sana toka kwa wafanya biashara. Je utasaidiaje kuhakikisha bei hazipandi sana?
 
Swali miji mingine vipanya vimepunguzwa na kuletwa coaster ili kuongeza kasi ya usafiri. Je kwa hapa Bukoba utatusaidiaje?
 
Mchukia Fisadi I hope na majibu utatuja ahsante in advance
 
Anajibu. Kuhusu pesa aliyoileta kutokana na kuandika write up na kupata pesa toka Japan 200 milioni. Anasema aliikabidhi manispaa na kwa kuwa kipindi chake kilikuwa mwishoni hajui zilitumika vipi lakini ana taarifa zililiwa na hakuna ripoti iliyotumwa kwa wafadhili kama walivyokuwa wamekubaliana nao hawakuna kilichoendelea. anatoa ahadi kuwa akichaguliwa ataendeleza juhudi za kupata ufadhili zaidi.
Kuhusu ufadhili anasema inahitaji kupanuka kwa mji ili tu masuala yasiwe ya mjini tu bali mji uchangamke kibiashara pia. Kwa hiyo ametoa ahadi ya kulishughulikia ili kuhakikisha mji unakuwa kiuchumi tokana na usafirishaji.
Kuhusu viwanda analaumu kwamba juhudi zake za kuendeleza viwanda zilikufa. Anashukuru Mayawa kwa kujiongezea uzalishaji wa kiviwanda.
Kuhusu bei anaeleza kuwa ni sera za Chadema kupunguza bei za vitu muhimu kama vya ujenzi. Anatoa mfano wa wanajeshi ambao wamepewa punguzo katika bidhaa zao na serikali inalipia kiwango kilichobaki, kwa hiyo ni kitu kinawezekana.
 
Naona anaambiwa waliowapa nafasi redioni wanaelekea kuondoka hivyo anawashukuru sana. Kumbe mdahalo umetayarishwa na vyombo vyote vya Bukoba mjini.
Mdahalo umekatwa katika redio lakini bado wanazo dakika 15 kumalizia offline
 
Back
Top Bottom