Anajibu. Kuhusu pesa aliyoileta kutokana na kuandika write up na kupata pesa toka Japan 200 milioni. Anasema aliikabidhi manispaa na kwa kuwa kipindi chake kilikuwa mwishoni hajui zilitumika vipi lakini ana taarifa zililiwa na hakuna ripoti iliyotumwa kwa wafadhili kama walivyokuwa wamekubaliana nao hawakuna kilichoendelea. anatoa ahadi kuwa akichaguliwa ataendeleza juhudi za kupata ufadhili zaidi.
Kuhusu ufadhili anasema inahitaji kupanuka kwa mji ili tu masuala yasiwe ya mjini tu bali mji uchangamke kibiashara pia. Kwa hiyo ametoa ahadi ya kulishughulikia ili kuhakikisha mji unakuwa kiuchumi tokana na usafirishaji.
Kuhusu viwanda analaumu kwamba juhudi zake za kuendeleza viwanda zilikufa. Anashukuru Mayawa kwa kujiongezea uzalishaji wa kiviwanda.
Kuhusu bei anaeleza kuwa ni sera za Chadema kupunguza bei za vitu muhimu kama vya ujenzi. Anatoa mfano wa wanajeshi ambao wamepewa punguzo katika bidhaa zao na serikali inalipia kiwango kilichobaki, kwa hiyo ni kitu kinawezekana.