Mdahalo wa wagombea uenyekiti Chadema Taifa utafanyika tarehe 18/01/2025

Mdahalo wa wagombea uenyekiti Chadema Taifa utafanyika tarehe 18/01/2025

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Edwin Odemba: Mdahalo wa wagombea uenyekiti Chadema Taifa utafanyika tarehe 18/01/2025, siku ya jumamosi kuanzia saa 3:30 Usiku hadi saa 6:00 Usiku, mahali mtajulishwa. Mpaka sasa wagombea wawili wamethibitisha kushiriki mdahalo huo, tunaendelea na jitihada za kuhakikisha wote wanashiriki katika mdahalo, Asante.
 
Midahalo anzieni huko CCM,wenye serikali na wanaotuibia fedha zetu
 
Edwin Odemba: Mdahalo wa wagombea uenyekiti Chadema Taifa utafanyika tarehe 18/01/2025, siku ya jumamosi kuanzia saa 3:30 Usiku hadi saa 6:00 Usiku, mahali mtajulishwa. Mpaka sasa wagombea wawili wamethibitisha kushiriki mdahalo huo, tunaendelea na jitihada za kuhakikisha wote wanashiriki katika mdahalo, Asante.
Lissu atakubali ila Mbowe lazima achomoe maana mbele ya Lissu ...kigugumizi kitamtesa sana Mzee wetu Mbowe.
 
watu wameshaanza kutukanana muweke mdahalo mnataka wavuane nguo hadharani hatutaki kuona mbupu za watu wazima kama hao hazarani sisi
Mdahalo ni njia nzuri ya mgombea kuuza sera zake lkn nina wasiwasi kama utafanikiwa kwa sababu Lissu sio muungwana ni mpenda sifa.
 
Yaani Mbowe kung'ang'ania tu utawala ndani ya chama tayari ameshakuwa kama Ccm hata siku moja hawezi akakubali kushiriki kwenye mdahalo.

Ndiyo maana huu uchaguzi wa Chadema ni kati ya Ccm Mbowe na mpinzani Lissu. Mbowe kwenye huu uchaguzi anaenda kufanya fitina zote zinazofanywa na Ccm. Kura zitaibiwa, kura feki, polisi wa Ccm watamsaidia kwa kiasi kikubwa.
 
Edwin Odemba: Mdahalo wa wagombea uenyekiti Chadema Taifa utafanyika tarehe 18/01/2025, siku ya jumamosi kuanzia saa 3:30 Usiku hadi saa 6:00 Usiku, mahali mtajulishwa. Mpaka sasa wagombea wawili wamethibitisha kushiriki mdahalo huo, tunaendelea na jitihada za kuhakikisha wote wanashiriki katika mdahalo, Asante.
Vizuri sana, Binafsi sina wasiwasi na Simba Tundu lissu, atawachachafya vizuri mno.
 
Huyo jamaa ni dikteta sugu. amehodhi chama kama kampuni yake, hataki kuachia.
Hiyo hoja ya 'hataki kuachia' hata Lissu anakwepa kuitumia maana anajua kuwapo madarakani kwa Mbowe na kutaka kuendelea kuwapo madarakani, kupo kisheria, wala hajalazimisha kama ambavyo watu wengi wa vijiweni wanavyotaka ionekane. Njia pekee ya kuonyesha kwamba Mbowe 'hataki kuachia' madaraka ni kubadilisha katiba ya chama au kumshinda kwa kura. By the way Mbowe hajajiweka pale, ila amechaguliwa na hao hao CHADEMA. Kama wewe si mjumbe wa mkutano wa uchaguzi, usijihesabu sana kwamba na wewe ni mwenye CHADEMA, wenye CHADEMA ni wale watakaopiga kura
 
Huyu jamaa sio raia wa Tanzania na uhamiaji wanamuangalia tu
 
Mdahalo ni njia nzuri ya mgombea kuuza sera zake lkn nina wasiwasi kama utafanikiwa kwa sababu Lissu sio muungwana ni mpenda sifa.
Kwamba uungwana unaupima wewe na mme wako mbowe au umetumia kihezo gani kusema lissu sio muungwana.
 
Back
Top Bottom