ACT Wazalendo wamefanya jambo zuri sana katika siasa. Mdahalo ni sehemu muhimu ya shughuli za siasa
Kuna mapungufu makubwa yaliyotokana ima na mwendesha mdahalo au kamati ya maandalizi.
Vijana ndio viongozi wa vyama katika miaka michache ijayo, tunayo mifano mingi hai na mmoja ni Zitto
Tulitegemea mdahalo uongelee mambo kwa upana ili kujua uelewa wa viongozi hao.
1. Sera za nchi kitaifa- ni kipi kifanyike , kipi kizuri au kipi kinahitaji maboresho
2. Kimataifa- nini mtazamo wa vijana hao kwa jicho la Dunia
3. Uchumi- nini mtazamo wa sera za uchumi
4. Siasa- nini mtazamo wao kuhusu mambo mazito ya siasa nchini kama Muungano
Kulitakiwa uwanda wa majadiliano uwe mpana tofauti na nilivyoona. Ulikuwa kama mjadala wa highschool
Nadhani kwa mijadala inayofauta ya chama hicho au vingine ni muhimu wawepo waongozaji wenye mitazamo mipana ya masuala anuai katika jamii.
Nadhani muongozaji alipwaya sana na kamati hhaikumsaidia kuufanya mdahaho uwe moto na wenye tija
Pascal Mayalla una uwezo wa kuongoza shughuli hizi najua, na hapa nakupigia chapuo kwa weledi.
JokaKuu Zitto Kabwe