Pre GE2025 Mdahalo wa wagombea Urais wa TLS ulikuwa "fantastic". Wagombea Urais Uchaguzi Mkuu 2025 waige mfano huo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Unasema Kwenye nchi yetu, midahalo hiyo bado sana, hivi unadhani lini midahalo hiyo itakuwa muda muafaka, Kwa nchi yetu??

Ni chama Cha CCM pekee, ndicho "kinachokacha" midahalo hiyo😀
Siasa zetu zimetawaliwa na mambo yasiyo na maana Wala tija Kwa ustawi na utangamano wa kitaifa ndiyo maana nasema hivyo.
Ukitaka kuhakikisha pitia hoja zinazotolewa na wanasiasa wengi utaona ni kama aina fulani ya mipasho hivi.
 
..tatizo lingine ni kwamba hatuna waandishi au watangazaji wenye uwezo wa kuendesha midahalo ktk VIWANGO vinavyotakiwa.
 
Mgombea gani wa CCM mwenye gut ya kuongea kwenye midahalo ya akina kiasi?
 
..tatizo lingine ni kwamba hatuna waandishi au watangazaji wenye uwezo wa kuendesha midahalo ktk VIWANGO vinavyotakiwa.
Chifu Odemba wa Star TV, ni mwandishi nguli, anayeweza kuendesha kipindi kama hicho Cha mdahalo.

CCM msitafute sababu za kuukumbia mdahalo huo😀
 
Chifu Odemba wa Star TV, ni mwandishi nguli, anayeweza kuendesha kipindi kama hicho Cha mdahalo.

CCM msitafute sababu za kuukumbia mdahalo huo😀

..Odemba ana viwango ukimlinganisha na wachovu na chawa walioko ktk vyombo vyetu vya habari. Lakini ukimuangalia kimataifa utaona kwamba bado ana safari ndefu mnooo.
 
Je, unataka kumdhalilisha mgombea wetu asiyejua kuongea na kujenga hoja?? Utakuwa unatumika na mabeberu wewe, siyo bure hata kidogo.!!
 
..Odemba ana viwango ukimlinganisha na wachovu na chawa walioko ktk vyombo vyetu vya habari. Lakini ukimuangalia kimataifa utaona kwamba bado ana safari ndefu mnooo.
Kwani huo ni mdahalo wa kimataifa au wa kitaifa? madiwani, wabunge na Rais kuna shida gani kuwa na mdahalo?
 
Ni vizuri kuanza kupractice hata kama ccm watakataa, ila wengine wakishiriki itawaongezea imani kwa wapiga kura, na alikacha imani kwake itapungua. Hii ni mojawapo ya mbinu itakayowalazimisha ccm washiriki.
Iwekwe kwenye sheria
 
Naskitika chama chakavu ni weupe sana kichwani itakuwa ni aibu ya kimataifa.
 
Kikwete aliweka mpira kwapani na CCM ikapiga marufuku wagombea wake kushiriki midahalo, hiki ndicho chanzo cha nchi kupata marais wasiokidhi viwango vya juu.
 
Wakati hilo linafanyiwa kazi, njia pekee ni midahalo kuanza ktk uchaguzi mkuu wa 2025. Itachangamsha siasa pia vyama watalazimika kuwachagua watu sahihi kuviwakilisha vyama vyao, mtazamo wangu tu.
Bado tuna muda wa kutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…