MkikiMkiki2015
Member
- Jul 2, 2015
- 20
- 23
Shiriki kwa kutuma swali lako hapa JamiiForums kwa ajili ya kuwatumia viongozi watakao shiriki mdahalo hapo kesho Tarehe 20, September 2015.
Mkikimkiki‬ iko Zanzibar wiki hii na wamealika wagombea urais wa vyama vitano ambavyo ni CCM, CUF, ADC, CHAUMMA na ACT-Wazalendo Kushiriki ni kwa mwaliko tu!
Wakti huo huo, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la Twaweza, kuna ongezeko kubwa zaidi la Wazanzibari kupatiwa huduma ya umeme kati ya mwaka 2002 na mwaka 2012 pia huduma ya maji ya bomba imeongezeka kwa kiasi kidogo sana kati ya miaka kumi ya 2002 na 2012.
Utafiti huo unaonyesha kwamba Wazanzibari wanapedelea kuona ongezeko la Uhuru wa kujitawala wa Zanzibar na uwepo wa serikali tatu na pia asilimia 5 ya Wazanzibari wanajiona kuwa wao ni Wazanzibari zaidi kuliko kuwa Watanzania.
Tarehe: Jumapili Septemba 20 2015
Muda: 7:00 – 10:00am (Saa saba mchana hadi saa kumi jioni)
Mahali: Hoteli ya Double Tree Hoteli Zanzibar
Midahalo hii inalenga kuvipa vyama vyote fursa ya kunadi Ilani zao na kwa wananchi kuuliza maswali muhimu yatakayo pelekea maamuzi yao katika uchaguzi. Vyama vinavyoshiriki ni vile vyenye wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na wagombea Ubunge angalau majimbo 65.
- Midahalo hii itarushwa moja kwa moja na Star TV na Redio RFA. Vyombo vya habari vinakaribishwa kushiriki lakini lazima wajiandikishe kabla.
- Kupata nafasi ya swali lako kuulizwa kwenye mdahalo, tuma neno KUULIZA acha nafasi, andika swali lako na tuma kwenda namba 15678.
- Kama unapenda kuwa mmoja wa watazamaji ukumbini tuma neno KUSHIRIKI acha nafasi tuma jina na kazi yako kwenda 15678.
- Utatozwa bei ya kawaida ya ujumbe wa simu (SMS). Hakuna gharama ya ziada.
TUWAHOJI, TUWACHAMBUE, TUWAPIME!!
Karibuni!
===============
Update: Maandalizi ya kuanza kwa Mdahalo wa Wagombea Urais Zanzibar utakaofanyika Double Tree Hotel yanaendelea..

Washiriki Mdahalo leo ni Dk. Ali Shein (CCM), Seif Hamad (CUF), Hamad Rashid (ADC), Mohamed Rashid (CHAUMA), Khamis Lila (ACT).
Mdahalo wa #MkikiMkiki unakaribia kuanza. Kati ya wawakilishi watano wa vyama waliothibitisha kuwepo katika mdahalo, wawili wametoa udhuru.
Wawakilishi wawili waliotoa udhuru wa kutokuwepo kwenye mdahalo ni Dk. Shein (CCM) na Maalim Seif (CUF).
CCM hawajahudhuria Mdahalo huu kwa sababu wanazodai ni za 'kiitifaki'; CUF waliweka sharti kuwa watashiriki kama CCM watakuja.
Muongozaji anatoa taarifa kwa hadhira na anaeleza kwamba mdahalo utaendelea na wawakilishi waliopata fursa ya kuhudhuria.
================
Swali: Ni namna gani vyama vitaendelea kuulinda Muungano wa Tanganyika & Zanzibar?
Khamis Lila (ACT-Wazalendo): ACT-Wazalendo ingependa kuimarisha Muungano na si kuuvunja. Zanzibar na Bara tumeingiliana sana. Muungano una faida nyingi; ukienda kokote Bara na Visiwani huulizwi na mtu umetokea wapi na unafanya nini.
Hamad Rashid (ADC): Watanzania wanauhitaji Muungano. Sisi tunaamini Muundo wa Serikali unatokana na wananchi na kura ya maoni. Maamuzi ya wananchi yaheshimiwe juu ya aina ya Muungano wanaoutaka. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu; Mataifa yote yana nguvu kwakuwa yanakuwa yameungana.
Mohamed Rashid (CHAUMMA): Wananchi wanataka Muungano wa Serikali 3 zisizobagua kokote. Aina ya Muungano ya sasa inawanyonya wazanzibari ndio maana tunataka Muungano wa Serikali 3.
Swali: Vyama vitahakisishaje Zanzibar haiachwi nyuma kwenye maswala ya huduma za kijamii?
ELIMU
Hamad Rashid (ADC): Hakuna mwalimu wa Sayansi anayekaa Zanzibar kwa zaidi ya miezi 3; wengi hukimbilia Bara kutafuta maslahi.
Khamis Lila (ACT): Tuna walimu wa kutosha, wanafunzi wa kutosha lakini shule na vifaa vya kutosha ndiyo changamoto. Walimu hapa Zanzibar wamekosa uzalendo kwa kuwa wamekosa maslahi mazuri, sisi tutaboresha maslahi yao. Tutatoa huduma za jamii bila ubaguzi wowote kwa wananchi wa Zanzibar.
Walimu hapa Zanzibar wamekosa uzalendo kwa kuwa wamekosa maslahi mazuri, sisi tutaboresha maslahi yao. Tutatoa huduma za jamii bila ubaguzi wowote kwa wananchi wa Zanzibar.
Mohamed Rashid(CHAUMA): Nilikosea nikasema mimi ni mgombea kupitia NCCR, naomba nirekebishe kuwa nipo CHAUMA. Sisi tutatoa huduma ya Afya bure; Majengo yatakarabatiwa; Vituo vya Afya hapa Zanzibar vitakuwa wazi masaa 24.
AFYA
Lila(ACT): Tutaboresha huduma ya Afya kwa kuwatenga wajawazito kwenda wodi maalum ya wazazi. Tutaweka utaratibu mzuri wa matibabu.
Hamad Rashid(ADC): Bajeti inayoenda kwenye Sekta ya Afya ni ndogo sana. Ndilo tatizo la msingi kwa sasa!
SUALA LA OIC
Lila(ACT): Kuhusu OIC tutataka kujua wananchi wanataka nini; tukiona kuna uwezekano wa kujiunga OIC tutajiunga, sio suala baya.
Hamad Rashid(ADC): Suala la OIC ni miongoni mwa kero za Muungano... ADC itaanzia hapo!
Mohamed Rashid(CHAUMA): Suala la OIC liko wazi, Zanzibar yenye mamlaka yake kamili hili ni suala dogo sana!
AJIRA
Hamad Rashid(ADC): Zanzibar hakuna viwanda hasa vya kuzalisha ajira kwa vijana. ADC ikichaguliwa itajenga viwanda vya uzalishaji. Tuna tatizo la ajira hapa Zanzibar,tukiingia madarakani tutaitumia rasilimali ya Bahari kutengeneza ajira.
Lila(ACT): Kuna watu wamestaafu wanarudishwa kazini; vijana wengi wanakosa ajira sababu hii. Tutafufua pia viwanda vidogovidogo.
UCHUMI/KILIMO
Mohamed Rashid(CHAUMA): Tutatumia Jeshi la Kujenga Uchumi kuweza kuelimisha wananchi juu ya kilimo bora ili wapate kipato.
Lila(ACT): Tutawasaidia wakulima kuweka Hifadhi ya Jamii ili waweke akiba yao kwa faida ya baadae.
Hamad Rashid(ADC): Tutawafundisha wakulima jinsi ya kuweka akiba na tutahakikisha wanakuwa na bima.
UTALII
Lila(ACT): Tutaondoa vikwazo vidogovidogo kwenye sekta ya Utalii. Tutakuwa na mipango mizuri ili tufanye utalii wa kisasa.
Hamad Rashid(ADC): Sekta ya Utalii inaongoza kwa Zanzibar kwa kuingiza kipato. Watalii wakija wanahitaji Amani na Utulivu. Watalii wakija wanahitaji pia wakute Hoteli zinazoendana na viwango; wanataka walipe malipo kwa njia rahisi.
Tutaboresha njia za malipo kwa watalii ili kuweza kuvutia watalii zaidi. Tunautambua uwepo wa Mwenyezi Mungu. Nchi yetu inazo sheria lakini hazisimamiwi..
NAFASI YA WANAWAKE (JINSIA)
Hamad Rashid(ADC): Tunahitaji usimamizi wa kutosha kwa sheria zilizopo ili unyanyasaji kwa wanawake (wa kijinsia) usiwepo.
Khamis Lila(ACT): Tukiingia madarakani tutaisimamia Wizara ili iweze kufanya kazi zake vema. Tutaweka wanawake viongozi wasomi. Bila wanawake hata sisi tusingekuwepo, ni mama zetu na ni wake zetu.
RUSHWA
Mohamed Rashid(CHAUMA): Kitendo cha Polisi kuwa wanachukua rushwa ni kutokana na Utawala mbovu; tatizo linaanzia juu zaidi.
Khamis Lila(ACT): Rushwa kwa Polisi inasababishwa na vishawishi, ugumu wa maisha... Wakiwezeshwa vema basi Rushwa itapungua!
Hamad Rashid(ADC): Tatizo la Rushwa ni kubwa; tuhuma dhidi ya rushwa zinatakiwa kufanyiwa kazi haraka, wahusika wasilelewe. Tutatumia teknolojia zilizopo kuweza kupambana na rushwa. Tutatumia utaratibu wa manunuzi kwa njia ya mtandao.
MAHAKAMA YA KADHI
Khamis Lila(ACT): Mahakama ya Kadhi ipo Zanzibar, hili halina mjadala; labda tuangalie jinsi ya kuiboresha tu.
Hamad Rashid(ADC): Kenya, Uganda wana Mahakama ya Kadhi. Tanzania Bara kwa bahati mbaya mpaka sasa haijawa nayo. Mahakama ya Kadhi si mbaya, ni jambo la muhimu kwa Waislam na ni suala lililomo kwenye Kitabu Kitakatifu.
Mohamed Rashid(CHAUMA): Zanzibar inayo Mahakama ya Kadhi, kwa Bara napenda kuwambia kuwa ni haki ya msingi ya binadamu.
AMANI BAADA YA UCHAGUZI
Hamad Rashid(ADC): Tutalinda amani; tutaheshimu matokeo, tukidhulumiwa tutafuata taratibu zilizopo.Tunaviheshimu vyombo vya Dola.
Mohamed Rashid(CHAUMA): Amani yetu ikitoweka, itatugharimu zaidi ya miaka 40 kuweza kuirejesha!
Khamis Lila(ACT): Sisi hatupo tayari kusababisha vurugu wala kuivuruga amani iliyopo. Tukishindwa tutakubali matokeo!
WALEMAVU
Mohamed Rashid(CHAUMA): Tukipata madaraka tutawapa walemavu haki zao kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.
Khamis Lila(ACT): Tutawashughulikia walemavu kama tutakavyowashughulikia wananchi wengine. Tutawapa huduma wanazostahili.
Hamad Rashid(ADC): Bila mfumo mzuri wa Kisheria hata huduma nzuri kwa walemavu ni ngumu kutolewa. Tunatambua vipaji vya walemavu. Sisi kwetu walemavu wana nafasi ya kipekee, ni tofauti na kwa wenzangu walivyosema
MADAWA YA KULEVYA
Lila(ACT): Tukipata madaraka, tutapambana na wanaoingiza madawa ya kulevya; baadhi wanajulikana! Tutawafunga maisha hata kuwaua. Madawa ya Kulevya hapa Zanzibar yanaingia kwa kupitia Uwanja wa Ndege na Bandarini; tutayadhibiti maeneo haya.
Hamad Rashid(ADC): Zanzibar ni sehemu ndogo sana, ni rahisi kudhibiti wauza madawa. Tatizo ni Law Enforcement
Mohamed Rashid(CHAUMA): Kwa miaka 3 iliyopita kuna maendeleo mazuri kiasi ya upambanaji na madawa ya kulevya hapa Zanzibar. Sijawahi hata siku moja kusikia mtu kashtakiwa hapa Zanzibar wala kunyongwa kwa madawa ya kulevya.
SANAA NA MICHEZO
Hamad Rashid(ADC): Tunaamini Michezo na Sanaa ni soko linaloweza kuingiza kipato hapa Zanzibar. Tutatumia wataalam kuinua soko.
Mohamed Rashid(CHAUMA): Mimi ni kiongozi wa mpira wa miguu. Ni wachezaji wangapi hapa Zanzibar wamesajiliwa Simba na Yanga?
Khamis Lila(ACT): Sanaa zetu lazima ziangalie mila zetu hapa Zanzibar, sio tunaiga tamaduni za magharibi..
MAFUTA NA GESI
Mohamed Rashid(CHAUMA): Tukipata madaraka, tutaharakisha ndani ya miaka 2 tuanze kuchimba mafuta.
Khamis Lila(ACT): Tukiingia madarakani tutafanya utafiti kwanza kuhakikisha kama kweli mafuta yapo Zanzibar.
Hamad Rashid(ADC): Tayari Zanzibar imeshaanza kuongea na SHELL juu ya uchimbaji mafuta; tukiingia madarakani tutaendeleza juhudi.
UMASIKINI
Mohamed Rashid(CHAUMA): Ili kupunguza umaskini, tutawashirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo
Hamad Rashid(ADC): Kaya maskini sehemu kubwa zipo kwa wakulima. Ni kwa kuwa uzalishaji wao haujaboreshwa. Tutawapa pembejeo bure. Tutawalipa wafanyakazi kwa wanavyofanya kazi... Kwa taaluma zao, kazi wanazofanya na kuangalia mfumuko wa bei.
Hamad Rashid(ADC): Tutawalipa wafanyakazi kwa wanavyofanya kazi... Kwa taaluma zao, kazi wanazofanya na kuangalia mfumuko wa bei.
Mohamed Rashid(CHAUMA): Tutawalipa wafanyakazi wa kima cha chini USD 300, kwakuwa pesa yetu haina thamani.
SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA
Hamad Rashid(ADC): Wananchi wa Zanzibar waliamua wenyewe kuwa Chama chochote kitakachoshinda kitashirikiana na kilichofuatia. Nadhani kuna haja tutoe uhuru kwa chama kinachoshinda kuchagua chama cha kushirikiana nacho hapa Zanzibar. Nadhani si jambo sahihi kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutekeleza sera/ilani za chama kilichoshinda.
Mohamed Rashida(CHAUMA): Tukipata madaraka tutaunda serikali itakayoshirikisha vyama vyote, dini zote na makabila yote.
Khamis Lila(ACT): Tukishinda, tutaomba tubadilishe Katiba ya Zanzibar ili kurekebisha Muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Mdahalo UMEKWISHA, tunawashukuru wote waliofuatilia; unaweza kufuatilia yaliyojiri kwa kina hapa...
==========
Kwa 'LIVE' updates zaidi tembelea JF Twitter account - https://twitter.com/JamiiForums

Attachments
Last edited by a moderator: