Kudadeki
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 859
- 52
Mkuu umetumwa nini? Mbona wamesahau kukutuma kwenye mdahalo ukawawakilishe???
Sasa jaribu kupinga hoja kwa hoja badala ya kuleta habari za kilevi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu umetumwa nini? Mbona wamesahau kukutuma kwenye mdahalo ukawawakilishe???
Kwa maana hiyo unataka kusema nini? John mnyika ni mchaga?Huko Kimara na Mbezi si ndiyo walipojazana Wachagga? :becky:
Wewe hata ujibadilisheje maandiko yako yatabakia ni yale yale...acha kuleta siasa za ukabila.Huko Kimara na Mbezi si ndiyo walipojazana Wachagga? :becky:
Kwa maana hiyo unataka kusema nini? John mnyika ni mchaga?
Wewe hata ujibadilisheje maandiko yako yatabakia ni yale yale...acha kuleta siasa za ukabila.
Mbona sisi watu wa Bukoba chadema ndiyo Chama chetu mkuu, na ni chama ambacho kinajenga himaya kubwa sana pande hizi, Bukoba,Mwanza ,Mara,Kigoma,Mbeya na karibu kila pande za nchi hii.Ni mgombea wa chama chao.
Na mie Bibi Ntilie nimekuja mjini toka kijijini (ambako hakuna umeme kwa hiyo hakuna TV) na nimeweza kuuona mdahalo wa vijana wanaowania kuchaguliwa kuwa Wabunge kutoka vyama vya CUF na CHADEMA. Naweza kudiriki kusema kwamba vijana wote (pamoja na wale walioonekana kama wazee!) wamejieleza vizuri lakini wa CHADEMA wameonekana kujieleza vizuri zaidi wakielewa nini chama chao kinasimamia na wakaeleza na kujibu kiufundi na kisomi zaidi kuliko wagombea wa CUF. Hata hivyo, waliokuwa wakipigiwa makofi zaidi ni CUF, hususan Mtatiro ambaye baadhi ya mambo aliyokuwa akieleza yalikuwa ni yaleyale ya CHADEMA lakini akayaeleza kwa namna tofauti na akapigiwa makofi hayo.
Pengine swali la kujiuliza ni kwa nini vijana wa CHADEMA - Halima Mdee, Zitto Kabwe, John Mnyika, Regina na Mrema hawakupigiwa makofi ya kutosha ingawa ndio walioeleza sera zao vizuri zaidi? Kwa nini hawakuweza kupata makofi ya nguvu hata pale walipojaribu kuwaeleza wasikilizaji jinsi wabunge wa CHADEMA wa bunge lililopita walivyofanya kazi kubwa ya kuichachafya serikali ya CCM bungeni? Yawezekana pia huenda wapiga makofi wale walikuwa ni wana CCM wenzangu ambao kwa kuwa hakuna mgombea wetu aliyejitokeza basi wakaamua ama walipangwa kuingia kwenye mdahalo kuwadhoofisha CHADEMA kwa kutowapigia makofi waliyostahili. Naambiwa eti Chama chetu CCM siku hizi hakiaminiki tena!
Lakini, upo upande mwingine wa shilingi kwamba huenda katika wakati huu tulionao wa joto la uchaguzi kupanda, kwenye kampeni ama midahalo ya aina hii wananchi wanapenda kusikia maneno ya kishabiki zaidi kuliko yale ambayo yanaweza yakawa na uzito mkubwa lakini hayagusi hisia za kishabiki!
Nawashauri vijana mnaowania kuchaguliwa mkiwa kwenye majukwaa mbalimbali muangalie aina ya wasikilizaji wenu, muwe makini mgundue haraka wasikilizaji wale wanataka kusikia nini kutoka kwenu na kwa lugha ya aina gani. Muwe tayari kubadilisha mbinu haraka pale mnapoona makofi hayawi mengi ipasavyo! Mnyika amchunge Mtatiro asijempoka tonge mdomoni.
Mhe. Bibi Ntilie,
Uchambuzi wako ni sahihi. Niliona ule ushangiliaji nikahisi ni CCM walikuwa wamepachika mamluki wao kushangilia mgombea ubunge yeyote asiyekuwa Chadema, kwa vile Dk. Slaa amemlemea sana huyu mgombea u-Rais wao mgonjwa. Ulisoma kuwa juzi hata aliondoka jukwaani ghafla, bila kuaga?
Katika mdahalo huu wa Movenpik, niliona pia baadhi ya washabiki wa CUF waliokuwa na picha za Prof. Lipumba. Hata Jenerali Ulimwengu alilazimika kukemea washabiki waliokuwa waki-raise hizo picha wakati Mtatiro au Limbu akishangiliwa.
Naungana nawe katika kushauri wagombea vijana wa CHADEMA, nikisisitiza kwamba endapo watashiriki ktk mdahalo mwingine wazingatie ukweli kwamba Dk. Slaa sasa, hasa kukubalika kwake kwa WaTz., ni mtaji mkubwa. Wataje sifa zake na umahiri wake kiuongozi.
Kigeugeu cha J.K. na kukumbatia kwake vigogo wa CCM ambao, yeye mwenyewe na serikali yake imewatuhumu kwa ubadhirifu wa mali ya umma na kwa ufisadi, ni jambo la kuwakumbusha wananchi kila wakati, ili J.K. na ccm wasipewe kura ifikapo Oktoba 31. Kwa maneno mengine, wakumbusheni WaTz. kwamba J.K. ameteua Basil Mramba, Andrew Chenge na Lowassa kugombea ubunge, licha ya yeye mwenyewe na serikali yake, kuwatuhumu kwa makosa ya jinai. Kwa hili kosa tu, hajui na hafai kuendesha nchi. Asichaguliwe tena.
Mbona sisi watu wa Bukoba chadema ndiyo Chama chetu mkuu, na ni chama ambacho kinajenga himaya kubwa sana pande hizi, Bukoba,Mwanza ,Mara,Kigoma,Mbeya na karibu kila pande za nchi hii.
Wewe hata ujibadilisheje maandiko yako yatabakia ni yale yale...acha kuleta siasa za ukabila.
We sijui ndo Kudadeki, whoever the hell you, are jenga hoja! Myika ni mgombea ubunge kupitia CHADEMA aliyetokea kwa na kabila kama ulivyo wewe..
Punguza uongo. Mkapa alikubali kuingia mdahalo kwenye uchaguzi wa 1995 lakini ule wa 2000 aliukacha. Sasa mwaka 2000 katibu mkuu wa CCM alikuwa nani kama siyo Mangula? Hizo agenda zenu za kuwa CCM ilikuwa nzuri kabla ya kuingia Kikwete na Makamba ndiyo tunazozipiga vita hapa.
Mhe. Bibi Ntilie,
Uchambuzi wako ni sahihi. Niliona ule ushangiliaji nikahisi ni CCM walikuwa wamepachika mamluki wao kushangilia mgombea ubunge yeyote asiyekuwa Chadema, kwa vile Dk. Slaa amemlemea sana huyu mgombea u-Rais wao mgonjwa. Ulisoma kuwa juzi hata aliondoka jukwaani ghafla, bila kuaga?.
Mtatiro anajibu ndani ya muda. Sasa nyinyi kama mnaona hao wengine waakina Mrema wanaotoa maelezo mengi bila ya kujibu swali huku muda ukuiisha ndiyo utaratibu mzuri wa "kupeana zamu" na "siyo kubebana", bora muendelee na utaratibu huo. Wakati huo huo Mtatiro wa CUF anaenda right to the point na kumaliza kujibu swali within the given time frame.
Mkapa alishafanya mdahalo 1995 na akawabwaga wote including the perennial candidate Lipumba; sasa 2000 walikuwa ni wale wale na hakukuwa na sababu ya kufanya nao mdahalo kwanii utendaji wake kama Rais haukuwa na dosari!! Sasa Kikwete amewahi kufanya mdahalo na nani toka ameukwaa urais?Ni kweli isiyopingika kuwa ccm ya Mangula ilikuwa bora na mahili kuliko hii ya Ze komedi!!
Yaelekea ndugu yangu unashindwa kutambua tofauti ya MDAHALO na MKUTANO WA KAMPENI. Kama watu wangekuwa wanataka kusikia vibwagizo na vijembe tu bila hata kuelezea sera na ilani za vyama vyao na kuzitolea ufafanuzi wasingefanya mdahala na wangeenda kwenye mikutano ya kampeni, wakarekodi na kurusha katika luninga.
Jamani wapenzi mi nilikuwepo kwenye ule mdahalo, kusema ukweli wale waliokuwa wakipiga makofi ni wanachama wa CUF, ndo walioujaza ukumbi walikuja na mabsi yao, sijui waliingiaje wote wale, walikuwa na vipeperushi, bendera za CUF, na picha za wagombea wao Mtatiro na Lipumba, walivaa sare zao za chama wakati kadi hazikuruhusu mavazi hayo. na upigaji makofi yao ilikuwa ni kwa watu wao wa CUF tu, no matter wameongea pumba ama la walipiga makofi but wale wachadema no matter waliongea point gani hawakupigiwa makofi. kwa mtazamo wangu they wre not fair at all, sikuwapenda hata kidogo, hata pale mwenyekiti alipowaomba wazishushe vipeperushi vyao chini si mahala pa kampeni hawakusikia wakidai eti imawauma eee.... nikajifunza kuwa CUF si chama cha amani no mattter wanamgombea mzuri kiasi gani I woul not dare to elect them, ni watu wasioenda shule hata kidogo, sijui ni wapiga debe stendi? hakyanani hawewezi kuchukua nchi hata kidogo. so nawaomba kwa kutazama mdahalo ule msiamue kuwa sijui nani alikuwa bora nani hakuwa bora kwa kuangalia upigaji wa makofi, chukueni zile pointi na sera zao walizokuwa wakisema.