Elections 2010 Mdahalo wa Wagombea vijana Movenpik 25/09/2010

Ni mgombea wa chama chao.
Mbona sisi watu wa Bukoba chadema ndiyo Chama chetu mkuu, na ni chama ambacho kinajenga himaya kubwa sana pande hizi, Bukoba,Mwanza ,Mara,Kigoma,Mbeya na karibu kila pande za nchi hii.
 

Mhe. Bibi Ntilie,

Uchambuzi wako ni sahihi. Niliona ule ushangiliaji nikahisi ni CCM walikuwa wamepachika mamluki wao kushangilia mgombea ubunge yeyote asiyekuwa Chadema, kwa vile Dk. Slaa amemlemea sana huyu mgombea u-Rais wao mgonjwa. Ulisoma kuwa juzi hata aliondoka jukwaani ghafla, bila kuaga?

Katika mdahalo huu wa Movenpik, niliona pia baadhi ya washabiki wa CUF waliokuwa na picha za Prof. Lipumba. Hata Jenerali Ulimwengu alilazimika kukemea washabiki waliokuwa waki-raise hizo picha wakati Mtatiro au Limbu akishangiliwa.

Naungana nawe katika kushauri wagombea vijana wa CHADEMA, nikisisitiza kwamba endapo watashiriki ktk mdahalo mwingine wazingatie ukweli kwamba Dk. Slaa sasa, hasa kukubalika kwake kwa WaTz., ni mtaji mkubwa. Wataje sifa zake na umahiri wake kiuongozi.

Kigeugeu cha J.K. na kukumbatia kwake vigogo wa CCM ambao, yeye mwenyewe na serikali yake imewatuhumu kwa ubadhirifu wa mali ya umma na kwa ufisadi, ni jambo la kuwakumbusha wananchi kila wakati, ili J.K. na ccm wasipewe kura ifikapo Oktoba 31. Kwa maneno mengine, wakumbusheni WaTz. kwamba J.K. ameteua Basil Mramba, Andrew Chenge na Lowassa kugombea ubunge, licha ya yeye mwenyewe na serikali yake, kuwatuhumu kwa makosa ya jinai. Kwa hili kosa tu, hajui na hafai kuendesha nchi. Asichaguliwe tena.
 
Tunahitaji katiba mpya, viraka vimetosha jamani! Wagombea vijana mbona hatuwasikii kuhusu hili? Tofauti yenu na wao isiwe UMRI tu!
 

Na lile bango lilokuwa linalomsifu Slaa lilioshikwa na mtu wa Chadema ambalo lilionyeshwa kwa takriban sekunde kumi kwenye TV hukuliona kabisa au siyo?

Hivi wangeshangiliwa wazungumzaji wa CHADEMA kama walivyokuwa wanashangiliwa wazungumzaji wa CUF, je mngekuja na hoja hizi za kuwa kulikuwa na mamluki wa CCM? Kwanini inawawia vigumu kuamini kuwa wazungumzaji wa CUF walikuwa wanapigilia msumari kwenye issue na kwa muda uliowekwa wakati wale wa kwenu CHADEMA walikuwa wanabaki kujisifu na "rekodi" bungeni. Maswali yalikuwa mtafanya nini kwa issue tofauti, wazungumzaji wenu walibaki kusema walifanya nini huko bungeni. Dakika walizopewa ni mbili kwa kila swali, sasa ukienda kuanza story za nani alisema nini bungeni of course muda utaisha na hautaweza kujibu swali. Matokeo yake muda unaisha swali halijajibiwa na hakuna cha kushangilia. Mbona alishangiliwa pale Zitto alipomuuliza yule kada wa CCM iweje aseme bungeni wapinzani wako kidogo wakati uchaguzi haujafanyika? Je ni nani waliomshangilia? Mamluki wa CCM?

Kubalini yaishe na zingatieni hayo anayoyaambiwa Bibi Ntilie (Mama Ntilie wa zamani) katika paragraph yake ya mwisho alipoamua kusema ukweli na kutoa ushauri wa bure kwa CHADEMA. Hapo utajiuliza hivi kweli mpenzi na mwanachama wa CCM anaweza kutoa ushauri wa bure na pia awe anaogopa kuona mgombea wa CUF kuweza "kumnyang'anya tonge" mgombea wa CHADEMA? Tunadanyanyana kwa sana tu huku tukiwa na agenda zetu za siri. :becky:
 
Mbona sisi watu wa Bukoba chadema ndiyo Chama chetu mkuu, na ni chama ambacho kinajenga himaya kubwa sana pande hizi, Bukoba,Mwanza ,Mara,Kigoma,Mbeya na karibu kila pande za nchi hii.

Niliwahi kusikia kulikuwa na mbunge wa CUF huko Bukoba lakini sijapata kusikia kuna mbunge wa Chadema huko. Sasa kama watu wa Bukoba chama chenu kingekuwa CHADEMA si basi mngelikuwa na japo mbunge mmoja kutoka chama chenu?
 
Wewe hata ujibadilisheje maandiko yako yatabakia ni yale yale...acha kuleta siasa za ukabila.

We sijui ndo Kudadeki, whoever the hell you, are jenga hoja! Myika ni mgombea ubunge kupitia CHADEMA aliyetokea kwa na kabila kama ulivyo wewe..
 
We sijui ndo Kudadeki, whoever the hell you, are jenga hoja! Myika ni mgombea ubunge kupitia CHADEMA aliyetokea kwa na kabila kama ulivyo wewe..

Ngoja pombe za jana ziishe vizuri halafu uandike vizuri. Maana sijaelewa hata kimoja ulichoandika.:glasses-nerdy:
 

Mkapa alishafanya mdahalo 1995 na akawabwaga wote including the perennial candidate Lipumba; sasa 2000 walikuwa ni wale wale na hakukuwa na sababu ya kufanya nao mdahalo kwanii utendaji wake kama Rais haukuwa na dosari!! Sasa Kikwete amewahi kufanya mdahalo na nani toka ameukwaa urais?Ni kweli isiyopingika kuwa ccm ya Mangula ilikuwa bora na mahili kuliko hii ya Ze komedi!!
 

Acheni kuwasingizia CCM. Ni kweli CCM walikuwa na viana wao wasiozidi thelathini ambao walikaa pamoja . Lakini karibia ya robo tatu ya walikuwemo ukumbini pale walikuwa ni wafuasi wa CUF waliokua kwa makundi na wakiwa na viongozi walikuwa wakiwapanga mle ndani hata jinsi ya kusambaa katika ukumbi ule. Wale walikukaa safu za mwisho walikua wakati mdahalo umeshafika robo na sehemu za mbele zilikuwa zimejaa hivyo wakakaa pamoa. Kwa waliofuatilia naamini waliona baadhi ya makundi yakiingia wakati mdahalo unaendelea. Wale haribia wote walikuwa wafuasi wa CUF.

Huo ndio ukweli wenyewe....
 

Yaelekea ndugu yangu unashindwa kutambua tofauti ya MDAHALO na MKUTANO WA KAMPENI. Kama watu wangekuwa wanataka kusikia vibwagizo na vijembe tu bila hata kuelezea sera na ilani za vyama vyao na kuzitolea ufafanuzi wasingefanya mdahala na wangeenda kwenye mikutano ya kampeni, wakarekodi na kurusha katika luninga.
 
Jamani wapenzi mi nilikuwepo kwenye ule mdahalo, kusema ukweli wale waliokuwa wakipiga makofi ni wanachama wa CUF, ndo walioujaza ukumbi walikuja na mabsi yao, sijui waliingiaje wote wale, walikuwa na vipeperushi, bendera za CUF, na picha za wagombea wao Mtatiro na Lipumba, walivaa sare zao za chama wakati kadi hazikuruhusu mavazi hayo. na upigaji makofi yao ilikuwa ni kwa watu wao wa CUF tu, no matter wameongea pumba ama la walipiga makofi but wale wachadema no matter waliongea point gani hawakupigiwa makofi. kwa mtazamo wangu they wre not fair at all, sikuwapenda hata kidogo, hata pale mwenyekiti alipowaomba wazishushe vipeperushi vyao chini si mahala pa kampeni hawakusikia wakidai eti imawauma eee.... nikajifunza kuwa CUF si chama cha amani no mattter wanamgombea mzuri kiasi gani I woul not dare to elect them, ni watu wasioenda shule hata kidogo, sijui ni wapiga debe stendi? hakyanani hawewezi kuchukua nchi hata kidogo. so nawaomba kwa kutazama mdahalo ule msiamue kuwa sijui nani alikuwa bora nani hakuwa bora kwa kuangalia upigaji wa makofi, chukueni zile pointi na sera zao walizokuwa wakisema.
 
Kwa waliofuatilia ule mjadala wa wagombea vijana hivi LIMBU LUKAS - CUF Hivi huyu Jamaa naye ni KIJANA? Maana nahisi anaweza kumzaa Mnyika,
 

Nyie ndiyo wale wale wa CCM mtakaotetea kila pumba za CCM as long as zilikuwa kabla ya Kikwete. CCM kwenu imeanza kuwa mbaya pale Kikwete alipoingia madarakani. Jitu limeua watu, limeiba kura, limekumbwa na kashfa kibao za wizi kuanzia rada, ndege ya rais, Kiwira halafu anakuja jitu lisilokuwa na hata chembe ya aibu anadai Mkapa "utendaji wake kama Rais haukuwa na dosari"? Sasa kama hiyo siyo saratani ya fikra sijui kitu gani.

CCM ya Mangula ilikuwa nzuri? Ile iliyokuwa inaongoza kwa kuiba kura Zanzibar na kuwapeleka watu kuwa wakimbizi kule Shimoni Kenya?

Labda kumbukumbu zako haziko sawasawa lakini baada ya mdahalo BBC walifanyanya opinion poll na Prof. Lipumba alitangazawa mshindi wa mdahalo ule. Isitoshe mdahalo ule ulimtoa Lipumba from nobody to a contestant. 😛layball:
 

Kwenye mkutano wa kampeni ndiyo una muda mwingi wa kupiga soga na kuifafanua sera ya chama chako. Kwenye mdahalo una restriction ya muda and you have to answer the question within the given time limit. Nitakupa mfano wa swali la elimu. Muongeaji wa CUF alienda straight to the point kuwa from chekechea to chuo kikuu, elimu itakuwa bure chini ya uongozi wa Prof. Lipumba. Yule muongeaji wa Chadema akaanza kutoa maelezo ya taaluma ya ualimu kuachwa nyuma na sijui kudharauliwa, matokeo yake muda ukaisha na kashindwa kujibu swali.
 

Utaendelea kujifunza huku roho ikikuuma. Ila ushauri wa bure usije ukajiua tu wakati wa matokeo ya uchaguzi yatakapoanza kutoka baada ya uchaguzi. :becky:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…