Mdau aliyeripoti kelele Mtaa wa Alesika shukrani zikufikie huko ulipo, sasa imebaki Kanisa la Angles Ministry kutumia Sound Proof

Mdau aliyeripoti kelele Mtaa wa Alesika shukrani zikufikie huko ulipo, sasa imebaki Kanisa la Angles Ministry kutumia Sound Proof

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu kwema?

Kuna mdau alileta kuhusu suala la Mtaa wa Alesika, Mbezi Beach kwenye baa na Kanisa la Angels Ministry kuwa kero kutokana na kulele kubwa kutoka kwao na walikuwa kikesha usiku kucha.

Upande wa Pub ya Amigos tunashukuru suala hili wamejirekibisha, shida imebaki kwenye kanisa la Angels Ministry. Japokuwa wamepunguza muda wa kufanya shughuli zao; sasa hivi hawakeshi usiku kucha wanaishia saa sita, na hata siku za ibada zimepunguzwa lakini kelele ziko pale.

Pia soma: Kelele usiku kucha Mtaa wa Alesika, Mbezi Beach kutoka Amigos Pub na Kanisa la Angels Ministry ni kero kubwa, tumechoka!

Shida yetu kubwa ni kwenye matumizi ya sound proof, sababu kanisa lipo kwenye makazi ya watu kelele inakuwa too much kiasi cha kuwa kero kubwa.

Kupunguza muda wa kukesha ni kazi bure kama kelele ziko pale pale, nadhani na sheria zinawataka kuwa na sound proof. Hivyo tunaomba mamlaka kama walivyoweza kushughulikia wapunguze muda wa kukesha vivyo hivyo upande wa sound proof wafuate pia sheria.

Za chini chini ni kuwa jamaa kwao mambo safi, na kuhonga kwake ni kitu kidogo tuu ndio maana ilichukua muda sana kufikia hatua hii.

Anayeendesha kanisa hilo anaenda kwa jina la Prophet David Richard, tafadhali mamlaka husika naombeni mfanyie kazi na hili pia tuondokane kabisa na changamoto hii.
 
Back
Top Bottom