Mdau anahoji "kwanini Vitabu vya dini vimetafsiriwa kila lugha, lakini sio vitabu vya maarifa ya dunia"

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Mdau ahoji imekuwaje watu wamefanikiwa kutafsiri vitabu vya dini kuja kwenye lugha mbalimbali hili kila mtu allowe, lakini vitabu vya maarifa ya dunia kama Vya kijeshi, kiuchumi, kimatibabu, kisayansi na viinginevyo vyenye kumsaidia mwanadamu kuishi na mazingira havijatafsiriwa, yani vimebaki kwenye lugha zao za asili... mtu wa kazuramimba au tandahimba anajua vitabu vya dini ila vitabu vya maarifa ya kisayansi hajui chochote.

View: https://youtu.be/E9sJ1gcpB08?si=9AVyNL17JnGaLaQN
 
Mnatakiwa nyinyi wenyewe ndiyo mtafsiri. Nyerere alijua hilo. Yeye mwenyewe alitafsiri vitabu vingi sana. Badala ya kuwa na bodi ya maziwa tungekuwa na idara ya utafsiri ya taifa.

Mzungumzaji ni anaonekana muelewa sana. Tungekuwa tumetafsiri vitabu vya maarifa angeweza kuelewa zaidi kuwa gari haliwezi tumia 'Radio Frequency'😂
 
Elimu lazima iwe na matabaka siyo lazima kila mtu aipate ndiyo maana ipo competitive in nature, kwa hiyo kwa kuweka kwenye lugha fulani tayari ishafanya auto selection, kuna watu hawatoweza kuelewa.

Ila mambo ya DINI hata mkielewa wote haina shida sababu mwisho wa siku sidhani kama yana mchango mkubwa kwenye maisha ya binadamu
 
Toka zamani kulikuwa na Utaratibu wa Tawala kubwa za Kidunia Kutafsiri Maarifa katika Lugha zao ili kukuza maarifa na kuyasambaza kwa Lugha zao mpaka Walatini walivyotafsiri kutoka kwa Waarabu kuja kilatini na kujimlilikisha Maarifa yote mpaka kufikia watu wakiamini Walatini ndio wagunduzi wa Maarifa. Hata hawa waarabu walitafsiri Maarifa kutoka Ugiriki ya Zamani, India , Persia n.k na hiyo ilipelekea Waarabu kuendelea katika kila nyanja katika kipindi cha Mediavel Age hii ni kabla ya Renaissance Age.
 
Elimu ina matabaka ya uelewa kwasababu kamwe hatuwezi kuwa sawa kiufahamu mfano elimu za Dini hakuna neno ambalo halina zaidi ya maana moja na uelewa wa Elimu za Dini inategemea na ukaribu wa Msomaji na Mungu au Imani anayoiamini. Kwa Upande wa Vitabu vya maarifa hata vikitafsiriwa pasina kuvifanyia kazi ni sawa na Bure
 
Elimu lazima iwe na matabaka siyo lazima kila mtu aipate ndiyo maana ipo competitive in nature, kwa hiyo kwa kuweka kwenye lugha fulani tayari ishafanya auto selection, kuna watu hawatoweza kuelewa.

Ila mambo ya DINI hata mkielewa wote haina shida sababu mwisho wa siku sidhani kama yana mchango mkubwa kwenye maisha ya binadamu
Hata biblia kufasiriwa ilikuwa vita kubwa. Unaiona haina maana lakini makasisi waliokuwa wanaweza kuisoma na kuielewa iliwapa nguvu sana.
 
Kwa sababu waandishi wa vitabu vya maarifa wamek0sa maarifa ya kuandika vitabu vyao kwa lugha t0fauti
 
Kwa sababu waandishi wa vitabu vya maarifa wamek0sa maarifa ya kuandika vitabu vyao kwa lugha t0fauti
 
Toka zamani kulikuwa na Utaratibu wa Tawala kubwa za Kidunia Kutafsiri Maarifa katika Lugha zao ili kukuza maarifa na kuyasambaza kwa Lugha zao mpaka Walatini walivyotafsiri kutoka kwa Waarabu kuja kilatini na kujimlilikisha Maarifa yote mpaka kufikia watu wakiamini Walatini ndio wagunduzi wa Maarifa. Hata hawa waarabu walitafsiri Maarifa kutoka Ugiriki ya Zamani, India , Persia n.k na hiyo ilipelekea Waarabu kuendelea katika kila nyanja katika kipindi cha Mediavel Age hii ni kabla ya Renaissance Age.
Na hata Wagiriki wenyewe walitafsiri maarifa ya Misri na kwenda kusoma Misri kwa miaka mingi. Wakayaweka maarifa hayo katika lugha zao. Watu wengi wakayaelewa.
 
Kwasababu watu wakijaa dini ndo wanatawalika ki rahisi sana, ni mbinu ya ku control raia
 
Mwafika akiona maisha makubwa anatafuta sababu au mtu wa kulaumu ...🤣🤣Unaacha kutafuta vya kabila lako unataka vya dunia nzima.
 
Wametafsiri Biblia, Quran kwa lugha ya kiswahili na hadi lugha za Makabila. Ila kutafsiri vitabu vya Sayansi kwa kiswahili wanasema hakuna misamiati.Wasomi?
 
Back
Top Bottom