Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mdau ameshusha andiko lake hili hapa, tulisome tunaweza kupata kitu au ikiwezekana wahusika wachukue hatua...
Japokuwa maonesho yanaelekea mwishoni lakini si vibaya tukipaza sauti changamoto ya huduma mbovu ya vyoo vinavyotumiwa na Wanawake ndani ya maonesho ya Viwanja vya SabaSaba, kwa ufupi vyoo ni vichafu.
Kwanza milango mingi ni mibovu, mingine imeandikwa ‘Usikitumie kibovu, maji hayaendi’.
Imagine 77 ni kila mwaka ila mazingira ya vyoo hayajawahi kuwa mapya kuanzia ndani hadi nje, ni yaleyale ya enzi tunaenda kubembea hadi leo.
Fedha za Tantrade na viingilio vyetu zinaenda wapi kiasi kwamba wanashindwa kujenga kisasa zaidi.
Wabadilike, tunapeana UTI tu, huruma kwa Watoto zaidi wanabeba magonjwa tu humo vyooni.