- Source #1
- View Source #1
Wakuu
NImekutana na huu ujumbe unaodaiwa kuchapishwa na Halima Mdee kupitia ukurasa wake wa X ingawa sijaiona je uhalisia ni upi?
"tulifanya makosa wengine kwa kujua wengine kwa bahati mbaya, wengine waliondoka kwa sababu ya mifumo iliyo kuwa inalalamikiwa.,,msituhukumu kwa mapito yetu Bali fungueni Milano karibiaheni wakosaji Wanao jutia na kuomba msamaha, haturudi kutafuta vyeo Bali kuongeza Nguvu ya kumuondoa mkoloni mweusi ili tuapte katiba mpya #Free tundu Lissu
Je mtatuhukumu Hadi lini? Kama Kuna adhabu ttupe ili tuitumikie lakini turudi kwenye njia ya Mapambano"

- Tunachokijua
- Halima James Mdee amekuwa mbunge wa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi kadhaa kuanzia mwaka 2005 akihudumu katika jimbo la Kawe hadi mwaka 2020 kabla ya kuteuliwa tena kuwa mbunge wa viti maalumu kuanzia mwaka 2020 hadi 2025.
Mdee alihudumu nafasi hizo akiwa na chama cha demkorasia na maendeleo (CHADEMA) kabla ya kufukuzwa rasmi na chama hicho mwaka baada ya kukata rufaa walipofukuzwa kwa mara ya kwanza.
Madai ya kuomba kurudishwa CHADEMA
Kumekuwa na ujumbe unaosambaa kupitia mitandao ya kijamii ukiwa katika namna ya screenshot na kudaiwa kuwa umechapishwa na Halima Mdee akiomba kurejea CHADEMA na kama kuna adhabu wapewe tu.
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa ujumbe huo haujachapishwa na Mdee kupitia ukurasa wake wa X kama unavyodaiwa.
Kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu JamiiCheck imejirirdhisha pia kuwa ujumbe huo ambaye pia kwa mara ya mwisho hadi kufikia ripoti hii kuandikwa alichapisha Aprili 28, 2026, haujachapishwa katika ukurasa wake rasmi wala chanzo kingine chochote cha kuaminika.
Screenshot hiyo ina dosari kadhaa ikiwemo Screenshot kutumia picha ya utambulisho (DP) tofauti na anayoitumia Mdee kwenye ukurasa wake wa rasmi wa X. Rejea hapa
Pia ina dosari nyingi za kiuandishi mathalani maneno kama "Karibiaheni", "ttupe", kuchanganya herufi kubwa na ndogo ikiwemo kuandika jina la Tundu kwa herufi ndogo (tundu).