Mdee na Wenzake wawasili mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri lao

Wabunge wa viti maalum akiwemo Halima Mdee na wenzake leo Ijumaa wamefika katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuhudhuria kesi waliyoifungua mahakamani hapo ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mdee na wenzake wamevuliwa uanachama wa chama hicho Novemba 27, 2020 kwa sababu wamekiuka katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila chama hicho kuwapitisha.

Mbali na Mdee, wengine ni Grace Tendega, Esther Matiko, Ester Bulaya, Cecilia Pareso, Hawa Mwaifunga, Jesca Kishoa na Nusrat Hanje.

Shauri hilo bado halijaanza kusikilizwa ambapo mawakili wote wa upande wa Chadema na wa akina Mdee wameitwa kwa Jaji Cyprian Mkeha kwa ajili ya taarifa kwa ufupi.

Hali ilivyo katika Mahakama hiyo kuwa wanachama wamejitokeza kwa wingi kwa pande zote mbili kwa akina Mdee na Chadema wakiwa wako kwenye vikundi mbalimbali

Kwa upande wa wanachama wa Chadema wamejitokeza wengi huku wengine wamevaa sare za chama.

Wakili wa Chadema, Peter Kibatala aliwasilisha ombi mbele ya Jaji Mkeha kuwa atoe hati ya wito kwa wabunge hao ili waje kuwahoji mahakamani hapo kuhusiana na viapo vyao.

Jaji Mkeha alikubaliana na ombi hilo na kueleza hati za wito zitolewe kwa waleta maombi saba (Mdee na wenzake) kwa ajili ya kuhojiwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Wanasiasa bhna, wakiwa jukwaani, wanatuambia tuniajiri,wao inashindikana.
 
Mahakama za Tanzania ni za hovyo sana. Too much political..
Hawaoni aibu majirani zetu wana sikiliza kesi ya uchaguzi wa rais kwa wiki moja. Ila ya wabunge fake ni mwaka sasa!!! Shame!!!
 
Danganya toto itasogezwa sogezwa mbele kesi hadi uchaguzi ufike ill kuwahadaa wafadhili
 
Ndiyo maana Kenya wanatidharau kuwa sisi Ni Bongo fleva. We are insensitive of the environment around su. Tazama Uzi mzima umejaa kejeli, hakuna analysis of what might have transpired today had it not been for the adjournment.
Matusi kejeli,Basi! johnthebaptist
 
Mahakama za Tanzania ni za hovyo sana. Too much political..
Hawaoni aibu majirani zetu wana sikiliza kesi ya uchaguzi wa rais kwa wiki moja. Ila ya wabunge fake ni mwaka sasa!!! Shame!!!
Nchi hii Mungu aiangamize aumbe viumbe wapya
 
Kwani MMM ameunga juhudi?
 
Wakili Pascal Mayalla huu ndio wakati wa kuonyesha uwakili wako na kuosha jina , simama upande wa Mdee na wenzake kwa niaba ya ccm
Mkuu Erythrocyte, kwanza thank you for an invitation kunikaribisha kuosha jina, but its very unfortunately, mimi ni wakili wa kujitegemea kwa kujitolea kutetea kesi za uvunjifu wa haki za binaadamu kwa watu wasio na uwezo, yaani ni human rights lawyer. Issue ya kina Mdee sio human rights violation, hiyo ni political rights, its not something for me!.
P
 
Bora hata wafike wamechoka,mimi naamini hawatafika kabisa Mkuu.
 
Hapana aisee TOZO kitu ingine hiyo mzee, ni meteso bila chuki.
Hili la Tozo likinyamaziwa ntaona kweli wabongo ni misukule ya kwenda πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Siyo mshahara tu, kuna marupurupu, sitting allowance akiwa bungeni na Sasa wanatetewa na mawakili Kwa gharama ya wananchi. Shithole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…