Mbwichichi
JF-Expert Member
- Dec 19, 2018
- 297
- 1,687
Habarini wakubwa wa kazi,maandalizi ya watani kunyoana kesho nadhani yanaenda kwa kasi nzuri….Rada za huku kwangu zinasoma kwamba bado tabu iko palepale,ila mwishoni mwa ligi watakaoteseka kesho watafurahia.
Binafsi ninapenda sana kushare mambo mbalimbali kuhusu maisha ya kila siku katika mfumo wa kuhadithia….
Leo nikiwa nasoma post ya anko “jemedari” mchambuzi mtata akipost kuhusu mabinti zake kupanda ndege kwa mara ya kwanza nikakumbuka visa vya baba yangu mzee Bwacha…Kwanza apumzike kwa amani sana huyu mzee,natamani kidogo ninachokipata leo angepata japo kipande chake lakini hayupo tena.
Wakati nakua mzee wangu alikua kauzu sana,yaani kauzu mno…Kabla sijaelezea mambo yake naomba nitoe kwanza wasifu wake.
Mzee alikua mstaafu wa jeshi la polisi ambaye kwa stori zake ambazo alikua akiamua anatusimulia kwamba alipelekwa kupigana vita ya kagera.Kule vitani mzee anadai aliwahi pigwa risasi ikamlamba puani lakini horizontally,na kweli mzee pua yake ilikua imekatika…angekua na uwezo angekua anavaa ile mask ile 🎭
Sasa shida yake ikawa hivi….ni kama alikua mwathirika wa ile vita,sababu hata saikolojia yake inaonekana haikukaa vizuri.
1. Kuna kipindi nikiwa darasa la sita naanza balehe ndio niligundua kumbe watoto wengine kama mimi wanavaa chupi,siku moja tukiwa kama familia tu ndio nikaropoka baba naomba ninunulie chupi……lahaula lakwata!!!,mzee alinizaba bonge la kofi la kijeshi,kwa wakati ule nilipoteza kumbukumbu zote nadhani maana ndio ikawa mwisho wa maongezi,nikawa nalia kwa kwikwi nikiamini nimeonewa.Kumbe mzee ile kitu ilikua serious sana kwake….akaniitia kikao na kesi ikageuzwa,akamwambia bi mkubwa kwamba mimi nimeanza dalili za kutaka kuwa “Shoga” 😳,kipindi kile sikuipa uzito sana,anasema inakuaje mtoto wa kiume naomba kununuliwa chupi,kwanini niombe kuvaa chupi,yaani uvae chupi ya kazi gani….mzee alisema yeye chupi yake ya kwanza alijinunulia baada ya kuwa ameajiriwa polisi😀😀😀…..na kuanzia hapo alisema hataki kabisa kusikia habari za mimi kuomba kuvaa chupi.Ilibidi bi mkubwa kwa siri aninunulie….Sikuwahi tena kumwambia mzee habari ya kuomba chupi na haijawahi kuwa kwenye bajeti zake hata siku moja.
2. Mzee wangu alikua anavuta sana sigara,lakini mtaani walikua wanakutana na masela pia alikua anavuta ganja….kuna siku moja sasa bahati mbaya katiza katiza nikakutana naye anamalizia kuvuta,kwa kipindi kile ilikua ni sigara ya Sporti…sijui kama ipo hadi leo,sasa mzee sigara alikua anavuta kwa kujificha,basi nikajifanya kumshauri kwamba baba sigara hizo siyo nzuri kwa afya yako….mimi sijui nilikosea nini,mzee alinikamata,aliniwasha sana makofi….akasema sasa leo ndio nakudundisha kuacha fatilia mambo ya watu….aliwasha sigara yake nikiwa chini ya ulinzi akaanza kuvuta na ananipulizia moshi usoni kama vile wanafanya maninja kwenye muvi wakimkamata jambazi….basi anavuta ananipulizia,na akabakisha nusu akasema leo utavuta sigara tuone kama utakufa,alisema nyerere anavuta sigara…basi kwa vitisho nikavuta ile sigara na alisema somo ni kuacha kumfuatilia….na kikweli sikuwahi kumfuatilia tena.
Alikuja kufa kwa kansa ya mapafu ila mpaka anakata kauli alikua anakataa kwamba sawa alikua anakosea lakini mimi sikupaswa kumshauri baba yangu hasa katika umri ule,narudia hadi anakufa hakukubali abadan kwamba ile kansa ilikua sababu ya sigara.