Mdogo wa mke wangu (binti) amenidharau na kunitukana mbele ya mke wangu

Utakubaliana na me kwambwa wanawake wakikristo tamaa ya mali zimewajaa san najua fika kama ishu ya kugawan mali ni ya kisheria ata kidini pia ipo ivo ukiachan na mwenza wako zile mali mlizochuma mkiwa pmj baada ya ndoa zinafaa kugaiwa pasu kwa pasu ila hukuti wanawake wa kiislamu kuwa na tamaa iyo ndio maana Bugatti anaoa kila leo 😂😂😂
 
Yes uko sahihi...Baba mkurya hakai kwa mkwewe hata siku 1
 
Ukiona democracy haifanyi kazi Nyumbani kwako,jaribu udikiteta!!
 
Mkuu tatizo hapo ni wewe. Kwa sababu umemjengea shemeji yako kujua kua hapo ni kwa dada yake na sio kwako.

Na ndio maana ana uwezo wa kukutukana na kukwambia umpe dada yake talaka mgawane Mali.

Na ndio maana hata mahamuzi ya baba yao kuja hapo wewe ujashirikishwa.

Kama wewe ndo baba mwenye nyumba hakuna mtu au ndu anaweza kuja hapo bila wewe kukubali. So go back angalia ulipogikwaa upasawazishe.
 
Weka picha ya huyo shemeji yako hapa, ma..ma.e angekula kichapo cha nguvu yeye na dada yake na angelala nje sema mkeo pia inaonekana anatoa profile yako kizembe hii kwangu No staki kukaa na mtu zaidi ya wanangu mkwe apambane huko nililipa mahali/ brideworthy kwisha
 
aliye oa anakwambia mkulya, wewe unaleta ujuaji mwingine kukataa

wapi kasema baba mkwe amekuja kukaa mwaka.

wafundisheni dada zenu wakulya tabia njema, sio kusingizia makabila mengine

ama ndo ile unaambiwa mtoto wako ana tabia chafu unakataa na kusingizia wamemfananisha atakuwa wa jirani
 
W
anadai ila mnawadhulumu, tunaishi nao huku lindi tunayaona
 
Ulishawahi Mpa kipigo Mkeo?.

Kama ni hapana...tatizo Hilo.


Wakurya ninawaelewa sana, Wanawake wao Wana dharau, jeuri, ubabe.

Kadiri unavyowapa kipigo, ndivo wanakuona mwanaume .


Ungekua ushampiga, huyo Mdogo mtu angekua anakuogopa kama ukoma.


Hata Ivo nikupongeze sana, Wewe no mwanaume, Kuna wakati, kua chini hakumaanishi wewe ni Mdhaifu, Sasa basi, MDOGO MTU AONDOKE HIYO JUMATATU

NARUDIA, AONDOKE, AENDE KWAO TARIME
 
Mimi nakataa ,Nishakutana na kesi nyingi za hao jamaa zangu waislam wengine wamestop mpaka kuachana baada ya kuskiaa wake wana mipango ya kugawana mali.

Mzee Ndomana nikasema uoe tu mwanamke asiekua na uelewa wa sheria hizo,lakini hawa wa sasa sio waislam wala wakristo, hivi unajua agenda wanazopush mafeminist kweny groups zao zile?

Bugatti yule ni mtu ambae ana washkaji zake wenye uelewa na sheria, hivyo anajua kufanya protection ya mali zake kabla hajaoa, mwenzangu na mimi utajua hata kufanya cohabitation agreements? Pre nuptials agreement?

Mkeo akikuburuza mahakamani basi hutoboi,Ukisoma vizur family law utaona kabisa sheria inambeba Mwanamke,na baadhi ya nchi anakula 75% ya mali.

Hivyo basi omba tu usikutane na mwanamke anejua haya mambo,hakuna mwanamke asietaka mali ikitokea devorce,sema wengine hawajui hayo mambo,na ndio maana feminism inahubiri hilo kuwapa elimu..Hapo hakuna cha dini ,ni mwanamke mwenyewe tu.

NB nakukumbusha, Mwanamke unae achana nae Sio Mwanamke uliemuoa [emoji2]
 
MKIAMBIWA MSIOE MUWE MNAELEWA

TABU zote za nini hizi
 
ni mtoto mdogo sana kwangu, ni wa mwaka 98. Mwisho akasema bhana eeh kama vipi andika talaka kwa mkeo mgawane mlivyo chuma kila mtu asepe zake (shemeji huyo)! Hata dada yake hakuwahu kutamka maneno kama haya asee.
mkuu, kwanza pole sana!

nahisi haujawahi kupiga mwanamke kwenye maisha yako kwa kijinsi mambo yanavyokustaajabisha... ni jambo jema!

ila nimekuja kugundua dunia hufundisha watu! huyo shemeji atarudi kukuomba msamaha, acha akaolewe na mtu ambaye hataki porojo ndani ya nyumba yake!

na hilo swala la guwana mali na wife inaonekana wameshaliongea ukizingatia kuwa wife anashare mambo ya ndani yenu!

swali ni kwamba, wakisimama pamoja upo tayari kuwa msela tena? kwani kwa spidi ya shemeji yako na mambo kuchukuliwa kwa uwepesi ndani ya nyumba yako, wakati wowote kuna jambo litaibuka!

jikaze, weka mguu chini! ila utakapofanya hili, ujue unaweze kuanzisha mengine!

kama wewe sio mtu mkali, tuliatuli kwani hua dunia ina adabisha watu.

karma husaidia wanyonge!

Unaelewa maana ya karma?
 
Tumia ubabe tu timua wote ndani ya nyumba.

Huyo mkeo mpe muda atarudi kwenye default factory settings
 

Mahakamani talaka na haki zake haziangalii dini.
 
Jitahidi uwe na kipato chako tofauti na hivyo vipodozi vya mkeo
Nahisi hapa ndio chanzo cha yote hayo. Mtu hadi anakaa kijiweni karibu na anapofanya kazi shemeji yake na kuteta na watu wa kijiweni kuhusu shemeji yake, je alikuwa anatafuta nini?
 
Kwanza biashara yenu

Sheme anaendaje kufunga hesabu? Au mkeo kakuzidi Mali?

Kuna mazingira umetengeneza mpaka mwanamke anakua na ujasiri wa kukufanyia vituko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…