Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MDOGO WANGU KANIAMBIA AMENIDHARAU KWA KUSEMA SITAMCHAGUA TUNDU LISU.
Na, Robert Heriel
Unajua mpaka siamini kabisa kwamba mdogo wangu wa kuzaliwa anaweza nambia maneno makali kama yale. Nina hasira, sijui nimfanyeje, bado nafikiri ni adhabu gani itakausha hasira zangu. Hawa madogo wa siku hizi adabu hawana, bila kuwakong'ota watakupanda kichwani.
Kisa kimekaa hivi;
Leo majira ya saa nne asubuhi, mdogo wangu anayenifuata alinipigia simu. Nilifurahi kuona simu yake kwani siku nyingi tulikuwa hatujaongea kama mwezi hivi. Basi baada ya salamu, mdogo wangu akaanza kuongea maneno ambayo yaliniuchafua moyo wangu. Naomba Ninukuu maneno yake hapa chini;
" Kaka, mimi sio mpenzi wa kusoma makala ndefu, ndio maana hata makala zako mara nyingi sio msomaji, japo nina-like tuu iliku-show love kwa Brother. Man wangu huwezi amini rafiki zangu wengi wanakusifu unajua kuandika stori, wengi wanapress stori zako. Hiyo inanifanya niwe proud na wewe Man wangu."
Mpaka kufikia hapo nikawa nafuraha kupewa sifa na dogo. Akaendelea;
" Sasa juzi, nimeona makala yako uliyoandika 'hutomchagua Lisu' Broo umeharibu kichizi, kama makala zako ndio hizo za kiwaki man wangu NIMEKUDHARAU. umejivunjia heshima Broo, pia umeniondolea Nyota ya Ubrigedia kwa washikaji zangu. Wanapiga lumbelele kiwaki. Hawakuheshimu tena"
Hapo nikaingilia mazungumzo baada ya kuona anakosa adabu na lafudhi yake ya Kichaga.
Nikamuuliza; Unataka nimchague Nani?
akanijibu; " Broo ujue nakuheshimu sana, usitake nambia huelewi nikakuona hujielewi. Huyo mgombea wa Kijani acha apite hivi. Akalee wajukuu, huoni pigo zake watu wamechapika, broo tangu nikuite kaka hata mia ya salamu ninayokupa hujawahi nipa. Mimi simaindigi Coz najua kitaa kugumu kisa hawa nyoka wa kijani. Huyu Nyoka wa kijani keshatulia vifaranga hapa kitaa watu wote wanapiga mayowe. Angalia ngeta za watu walivyong'atwa na nyoka wa kijani, then wewe unampa promo as If unaunachokipata"
Hapo ikabidi nimueleweshe kwa upole.
" Dogo sikia, huyo unayemuita Nyoka wa Kijani kafanya makubwa, embu tazama ndege, embu ona Reli ya kisasa, embu ona Bwawa jipya la kufulia umeme huko Rufiji, huoni barabara..." (Ananikatisha)
"Broo unajua wewe umepiga shule, afu mambo unazosema hata siye tusioenda shule tunakushangaa. Huyo Nyoka wa Kijani baada ya kutudonoa akaona haitoshi ndio akaleta hao Mwewe ili wazidi kuchukua vifaranga wetu. Tangu Ndege zinunuliwe huyo Nyoka wa Kijani alikuambia faida zilizoingiza hata kwa mwezi, vipi alikuambia kwa mwaka zimeingiza shilingi ngapi? Broo umekuja kuwaje man wangu"
" Au ndege za mapambo? Broo nilikuwa nakuheshimu lakini kwa hili ninajuta hata kukuheshimu," (Ninamkatisha)
"Embu acha hizo Dogo, Huyo Lisu kwani atafanya nini kumshinda huyo umuitaye Nyoka wa Kijani?"
Nikamuuliza.
" Braza! Braza! Braza! Nimekuita Mara tatu. Lisu ni habari ingine Chalii angu! Sio huyo nyoka mwenye sumu mbaya. Hivi watu wakitekwa wewe ulikuwa wapi Broo? Watu wakiuawa wewe ulikuwa wapi? Brother, hatutaki kuchagua mtu ambaye atashindwa kulinda raia wake asee! Embu ona vijana wanavyosota kisa huyo nyoka wako kukataa kuajiri maskola walio-graduate, Embu ona wafanyakazi walivyochapika mishahara ile ile kisa huyo huyo Nyoka wako wa kijani"
" Broo, hiyo elimu yako nimeidharau asee! Ni bora hata mimi ambaye sijasoma lakini ninauelewa wa mambo. Wewe umesoma na bado humuelewi Tundu Lisu, unamuelewa huyo Nyoka wa kijani. Au unapenda anavyorapu rapu tuu! Broo hujielewi asee!"
Hapo nikamkatisha nikaanza kumfokea, akanikatia simu. Nikampigia hakupokea, nikampigia zaidi na zaidi.
Akanitumia meseji isemayo; "TEMANA NA MIMI"
Kisha baadaye akanitumia sms
"Huna nyumba
Huna kiwanja
huna kazi ya maana
Unasema nyoka kaajiri sijuia ajira milioni ngapi, nawe unakubali kiduwansi, ukoo wako hakuna aliyeajiriwa kwenye hizo ajira milioni na ushee,
Unashindwa hata na sister, yeye ni mwanamke lakini anauelewa kukushinda. Broo Umejishushia heshima"
Nikampigia Mama, bahati nzuri Mama yupo kwenye Miti ya Kijani japo yeye sio nyoka wa kijani. Nikamueleza, sasa nasubiri jioni watakapokuwa wote nyumbani. Mimi niko mbali na home, nyumbani ni Moshi. Dogo yupo moshi.
Sio lazima jamani nimchague Lisu. Ninyi madogo wa siku hizi achaneni na mambo ya kuambiwa.
Huyu dogo nitamalizana naye, kesho napanda gari naelekea Moshi, nitawapa mrejesho nilivyomtia adabu.
Lisu hupati kura yangu, ngoja nikamalizane na huyo dogo. Yupo ndani ya uwezo wangu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300