Mdomo sungura kwa watoto

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216

Mdomo sungura ni nini?
Mdomo sungura (cleft lip and palate) ni aina ya ulemavu unaosababishwa na sehemu ya uso na mdomo kushindwa kufungwa mtoto anapokuwa akitengenezwa akiwa tumboni. Tatizo la mdomo sungura ni tatizo linalowapata watoto wengi katika jamii. Hali hii hutokea katika wiki ya tano hadi ya nane ya ukuaji wa mtoto anapokua tumboni ambapo sehemu tatu za uso yaani sehemu ya juu, pembeni na chini hushindwa kukutana.

Visababishi vya mdomo sungura.
Kuna visababishi mbalimbali vinavyopelekea mtoto kuzaliwa na ulemavu wa mdomo sungura. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika na wataalamu mbalimbali hali hii husababishwa na muingiliano wa matatizo ya vinasaba na sababu za kimazingira kama;
  • Sababu isiojulikana (idiopathic reason)
  • Unywaji wa pombe uliokithiri kipindi cha ujauzito.
  • Uvutaji wa tumbaku kipindi cha ujauzito.
  • Lishe duni kwa mama mjamzito, kama kukosa virutubisho muhimu kama vile vitamini aina ya asidi ya foliki.
  • Matumizi ya baadhi ya dawa kama dawa za degedege haswa katika kipindi cha ujauzito.
 
Tunashukuru kwa elimu.
Ushauri wako ni nini sasa?
 
Sababu isiyojulikana nadhani inaundugu na watu wasiojulikana.
 
Neema mambo!
 
naomba kuuliza maana nawaonaga ccbrt pale watoto wengi wakienda kupatiwa matibabu huo ugonjwa unapona??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…