neema shamuhenya
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 312
- 216
Mdomo sungura ni nini?
Mdomo sungura (cleft lip and palate) ni aina ya ulemavu unaosababishwa na sehemu ya uso na mdomo kushindwa kufungwa mtoto anapokuwa akitengenezwa akiwa tumboni. Tatizo la mdomo sungura ni tatizo linalowapata watoto wengi katika jamii. Hali hii hutokea katika wiki ya tano hadi ya nane ya ukuaji wa mtoto anapokua tumboni ambapo sehemu tatu za uso yaani sehemu ya juu, pembeni na chini hushindwa kukutana.
Visababishi vya mdomo sungura.
Kuna visababishi mbalimbali vinavyopelekea mtoto kuzaliwa na ulemavu wa mdomo sungura. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika na wataalamu mbalimbali hali hii husababishwa na muingiliano wa matatizo ya vinasaba na sababu za kimazingira kama;
- Sababu isiojulikana (idiopathic reason)
- Unywaji wa pombe uliokithiri kipindi cha ujauzito.
- Uvutaji wa tumbaku kipindi cha ujauzito.
- Lishe duni kwa mama mjamzito, kama kukosa virutubisho muhimu kama vile vitamini aina ya asidi ya foliki.
- Matumizi ya baadhi ya dawa kama dawa za degedege haswa katika kipindi cha ujauzito.