SoC02 Mdororo Sekta ya Ngozi: Changamoto za kusadikika na mikakati ya kujinasua

Stories of Change - 2022 Competition

Ottician

Senior Member
Joined
Jul 6, 2019
Posts
103
Reaction score
81
SIKIA HII

Tanzania ni nchi ya pili kwa mifugo mingi barani Afrika nyuma ya Ethiopia.Uwepo wa mifugo mingi ni fursa kubwa ya kuwekeza na kukuza biashara ya ngozi. Tuko wapi? ,Licha ya kuwa na fursa hii Tanzania ni nchi ya kumi na moja kwa uuzaji wa ngozi nje na uwezo wake ukiporomoka kila kukicha. Katika kizazi hiki cha Prada, Dolce& Gabbana na majina makubwa ya bidhaa za thamani zinazotumia ngozi ni dhahiri kuwa tuna fursa tunayoipuuza. Bidhaa za ngozi na ngozi ni kati ya bidhaa zinazouzwa sana na zinazotumiwa ulimwenguni kote ikiwa thamani inayozidi thamani ya biashara ya nyama, kahawa na mchele. Biashara rasmi ya kimataifa ya bidhaa za ngozi na ngozi inakadiriwa kuwa zaidi ya dola za Marekani bilioni 50 kwa mwaka na soko liwa bado na uhitaji mkubwa. Sekta hii iko eneo la kimkakati na dunia inatarajia ukuaji zaidi mpaka kufikia 2028 kulingana na ripoti ya grand view research (Report ID: GVR-3-68038-061-3).Tasnia ya mavazi ikiwa miongoni mwa vichocheo vikubwa zaidi.

TUNAFELI WAPI?
Mdororo wa sekta hii kwa nchi yetu yenye mifugo mingi katika nafasi ya pili Afrika nzima unachangiwa kwa kiasi kikubwa na sababu tunazoweza kutatua wenyewe. Vuta pumzi kidogo tuzizungumze:

Ukosefu wa sera stahiki za kuwezesha uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vya ngozi
Miongoni mwa makala nyingi, tovuti za serikali hata wizara husika hutaja na kusisitiza kwamba hii ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha sekta hii, Kabisa?. Nani wakututungia sera? Tunashindwa nini kutunga sera stahiki?. Sekta ya ngozi imekuwepo kwa muda na kwa nyakati kadhaa imekuwa yenye manufaa kwa nchi yetu. Licha ya hayo ufugaji ikiwa miongoni mwa shughuli kuu za watanzania hivyo kutokuwepo na sera stahiki kunatoa picha ya wazi ni jinsi gani sekta hii imetelekezwa licha ya kutambulika wazi kuwa ina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wetu. Hivyo basi kutumia ukosefu wa sera kama sababu ya kushindwa kufanikiwa ni sawa na kuweka sababu ya kusadikika ili kukwepa majukumu.

Ukosefu wa wataalamu
Kama ndio, basi picha ya wazi hapa ni kuwa mfumo wetu wa utoaji wa wataalamu wa sekta mbalimbali za uchumi ikiwemo sekta ya ngozi hauzingatii uhitaji na maarifa sahihi yanayotakiwa katika kukuza uchumi wetu kwa kutumia elimu kama kichocheo kikuu. Ni aibu kubwa kukosa wataalamu wa ngozi na teknolojia yake kwa miaka sitini sasa huku tukishuhudia ongezeko la mifugo yetu kila kukicha, je uvunaji wa bidhaa zetu utafanika namna gani?. Mpaka sasa licha ya kuwa na ngombe takriban milioni thelathini achilia mbali mbuzi, Je ongezeko hilo limekuwa ghafla? Hapana kwa kawaida sio ghafla, hivyo tulisinzia wakati mmoja. Hivyo twaweza sema taasisi zetu za kuandaa wataalamu ni chache sana hasa kwa elimu mahsusi inayohitajika sekta ya ngozi. Je, ni nani aandae wataalamu wetu, watatoka wapi? Hao wachache waliopo wametumika vipi mpaka sasa?. Basi tutafakari hili ili kujua kama kweli ni tatizo au tumelitengeneza.

Ukosefu wa elimu ya ufugaji bora
Ndio! Ni ukweli usiopingika kwamba ngozi bora hutegemea ufugaji bora , pia ngozi bora ndio huhitajika kwa bidhaa bora kutoboa katika ushindani wa soko la bidhaa la ngozi uliopo katika ulimwengu wa utandawazi sasa. Je, si kweli kwamba ukosefu wa elimu ya ufugaji ni tatizo la kusadikika? Hebu tupitie hizi takwimu japo kwa uchache wake, ukiachana na vyuo binafsi vya mifugo serikali pekee kupitia wakala wa vyuo vya mafunzo ya mifugo (LITA) ina takribani kampasi sita zinazotoa wahitimu kila mwaka katika ngazi ya cheti na astashahada ya afya ya mifugo na uzalishaji.

Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo ni moja kati ya taasisi kubwa inayozalisha wahitimu wa elimu ya mifugo kwa miaka sasa. Tuje hapa sasa, Wako wapi wataalamu wetu? Wametumika vipi?. Ni kweli kwamba anaweza asiwepo kati yetu mwenye jibu sahihi la maswali haya ila pia tutakubaliana kuwa tunaishi na wataalamu wengi miongoni mwetu na thamani ya elimu yao ikiwa kama ndoto. Je, watachangia vipi katika sekta hii mazingira ya kuwatumia kutoa elimu bora ya mifugo sio wezeshi kwa namna moja hadi nyingine na mara nyingi sio kipaumbele cha mamlaka husika.Je, ni wafugaji wetu wameikataa elimu? Basi kiufupi binafsi naweza sema kuwa changamoto hii ni ya kusadikika, sio changamoto halisia.

TUISHI HUMU
Tusisubiri chombo kizame, tuokoe jahazi.Tujaribu kufanya haya, ni tija kwa uchumi wa taifa letu.

Tujifunze sera bora za kisekta kwa wenzetu waliopiga hatua zaidi
Majirani zetu mfano Ethiopia na Kenya zimepiga hatua katika kuthaminisha bidhaa zao za ngozi na ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa usafirishaji wa ngozi ghafi kutoka barani Afrika kwenye soko la Ulaya na Asia.Tusafiri kwao kujifunza, turudi tutekeleze.

Tupitie mfumo wetu wa kutoa wataalamu kama ndio tunaouhitaji
Ile kasumba yakuwa na mitaala ya zamani tena iliyoandaliwa bila kuzingatia mazingira yetu ni ugonjwa unaotutesa. Tunapata wataalamu wasio na elimu inayoshabihiana na mazingira yetu, wasioendani na kasi ya teknolojia na wasioelewa Tanzania yao inahitaji nini kwa miaka ijayo kutokana na elimu na sekta yake. Tuachane na mitaala ya kurithi, tufikiri katika wakati uliopo. Tatizo la kukosa wataalamu haliwezi tatuliwa bila kutafakari mifumo tunayoitumia kuzalisha wataalamu wetu. Ikiwa tunahitaji uchumi wa viwanda kulingana na ukuaji wa teknolojia basi kuandaa mifumo ya kuzalisha wana teknolojia wetu, wanaojua mazingira yetu na wanaojua lengo letu ndani ya miaka kadhaaa basi huo ndio ufunguo wa mafanikio yetu ikiwemo ndani ya sekta hii yenye utajiri wa kufikia

Tusianze upya , Tuanzie tulipoishia
Sekta ya ngozi ilikuwepo toka awali na kuna wakati katika nchi yetu ilifanya vizuri, tuweke akilini pia wakati huo teknolojia ilikuwa bado chini. Sasa ni wakati muafaka wa kurudi nyuma na kufufua vituo vyetu vya kukusanya ngozi kutoka kwa kila mfugaji wetu na kila machinjio yanayotuzunguka maana imekuwa ni kama mizoga iliyokosa thamani, tuipe pia ngozo thamani yake kwa kuinunua kwa bei halali na stahiki inayoendana na thamani yake katika soko la dunia. Hii itawapa nguvu wafugaji ili kujua ni utajiri gani ulio katika bidhaa hii adhimu ya mifugo yao.

Asanteni kwa kunisikiliza!
 
Upvote 19
Hongera kwa kuthubutu. Gharama ya kununua ngozi ni Tsh. ngapi na unafanya nini ili kujua ubora wa ngozi.

Nitajihakikishiaje faida kama nikianza biashara hii?
Gharama ya kununua ngozi ya ng'ombe kwa wafugaji ni kati ya 3000 mpaka 5000.
Kujua ubora wa ngozi unahakikisha yafuatayo :-
1. Imechunwa vizuri bila kukatwa katwa, hasa maeneo ya kati kati ya ngozi ikitandazwa
2. Haina branding ( tattoo) zilizo pigwa na kuchukua asilimia kubwa ya ngozi
3. Ngozi iwe na uzito na iliyonawili ( kutoka ng'ombe mwenye afya)
4. Isiwe iliyoshambuliwa sana na ukurutu na kupe.

Kabla ya kuanza ili ijihakikishia faida ni lazima kutafuta tender ( kiwanda au middleman anayepeleka kiwandani)

Faida inatokana na tofauti kati ya bei unayochukulia na unayouza. Ukiongeza thamani kwa kuiwamba unaongeza gharama kwenye kuiuza. Cha msingi kuchukua ngozi zenye ubora, ukikosea hapa zitakuwa reject.

Mzoefu mwingine aongezee nyama...
 
Hongera sana sana, nilipata deal ya ku-supply Raw Salted Hides kwenye kiwanda kikubwa Sana Egypt ila ngozi zetu zikaonekana price Iko juu sana Sana.... anyway hii kitu ni hot [emoji91] sana sana. Nilijaribu kukusanya taarifa kwa sehemu ila pia Kuna urasimu kwa wauzaji..

Pili, Ngozi zetu nyingi hazina sifa kutokana na ng'ombe kuwekea alama kwa kuchomwa hivyo ngozi kuwa na alama.

Tatu, wachunaji wetu sio professional, wanazikata ngozi na hii hupunguza thamani ya Ngozi husika.

Nne, namna ya kuhifadhi ngozi kwetu Bado ni changamoto Kidogo......

Ngozi zetu nyingi hazina uzito wa 25kg ambazo zingekua rahisi kuuzika, japo Bado hata hizo zenye uzito mdogo Zina hizo changamoto

Tanza-nia ingekua na commitment kwenye mambo yake basi tungefika Mbali saaana.
Asante sana mkuu, umeongea ukweli mtupu. Tunashindwa kusaminisha ngozi zetu, soko lipo huko duniani na halitarajii kujaa leo au kesho.
 
Imekaa poa sana, nakupigia kura sasa. Vijana tuzidi kupambana bila kukata tamaa kwani fulsa ni nyingi lakini changamoto hazikosi.
Gharama ya kununua ngozi ya ng'ombe kwa wafugaji ni kati ya 3000 mpaka 5000.
Kujua ubora wa ngozi unahakikisha yafuatayo :-
1. Imechunwa vizuri bila kukatwa katwa, hasa maeneo ya kati kati ya ngozi ikitandazwa
2. Haina branding ( tattoo) zilizo pigwa na kuchukua asilimia kubwa ya ngozi
3. Ngozi iwe na uzito na iliyonawili ( kutoka ng'ombe mwenye afya)
4. Isiwe iliyoshambuliwa sana na ukurutu na kupe.

Kabla ya kuanza ili ijihakikishia faida ni lazima kutafuta tender ( kiwanda au middleman anayepeleka kiwandani)

Faida inatokana na tofauti kati ya bei unayochukulia na unayouza. Ukiongeza thamani kwa kuiwamba unaongeza gharama kwenye kuiuza. Cha msingi kuchukua ngozi zenye ubora, ukikosea hapa zitakuwa reject.

Mzoefu mwingine aongezee nyama...
 
SIKIA HII

Tanzania ni nchi ya pili kwa mifugo mingi barani Afrika nyuma ya Ethiopia.Uwepo wa mifugo mingi ni fursa kubwa ya kuwekeza na kukuza biashara ya ngozi. Tuko wapi? ,Licha ya kuwa na fursa hii Tanzania ni nchi ya kumi na moja kwa uuzaji wa ngozi nje na uwezo wake ukiporomoka kila kukicha.Katika kizazi hiki cha Prada, Dolce& Gabbana na majina makubwa ya bidhaa za thamani zinazotumia ngozi ni dhahiri kuwa tuna fursa tunayoipuuza.Bidhaa za ngozi na ngozi ni kati ya bidhaa zinazouzwa sana na zinazotumiwa ulimwenguni kote ikiwa thamani inayozidi thamani ya biashara ya nyama, kahawa na mchele. Biashara rasmi ya kimataifa ya bidhaa za ngozi na ngozi inakadiriwa kuwa zaidi ya dola za Marekani bilioni 50 kwa mwaka na soko liwa bado na uhitaji mkubwa. Sekta hii iko eneo la kimkakati na dunia inatarajia ukuaji zaidi mpaka kufikia 2028 kulingana na ripoti ya grand view research (Report ID: GVR-3-68038-061-3).Tasnia ya mavazi ikiwa miongoni mwa vichocheo vikubwa zaidi.

TUNAFELI WAPI?

Mdororo wa sekta hii kwa nchi yetu yenye mifugo mingi katika nafasi ya pili Afrika nzima unachangiwa kwa kiasi kikubwa na sababu tunazoweza kutatua wenyewe. Vuta pumzi kidogo tuzizungumze:

Ukosefu wa sera stahiki za kuwezesha uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vya ngozi

Miongoni mwa makala nyingi, tovuti za serikali hata wizara husika hutaja na kusisitiza kwamba hii ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha sekta hii, Kabisa?. Nani wakututungia sera? Tunashindwa nini kutunga sera stahiki?. Sekta ya ngozi imekuwepo kwa muda na kwa nyakati kadhaa imekuwa yenye manufaa kwa nchi yetu. Licha ya hayo ufugaji ikiwa miongoni mwa shughuli kuu za watanzania hivyo kutokuwepo na sera stahiki kunatoa picha ya wazi ni jinsi gani sekta hii imetelekezwa licha ya kutambulika wazi kuwa ina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wetu. Hivyo basi kutumia ukosefu wa sera kama sababu ya kushindwa kufanikiwa ni sawa na kuweka sababu ya kusadikika ili kukwepa majukumu.

Ukosefu wa wataalamu

Kama ndio, basi picha ya wazi hapa ni kuwa mfumo wetu wa utoaji wa wataalamu wa sekta mbalimbali za uchumi ikiwemo sekta ya ngozi hauzingatii uhitaji na maarifa sahihi yanayotakiwa katika kukuza uchumi wetu kwa kutumia elimu kama kichocheo kikuu. Ni aibu kubwa kukosa wataalamu wa ngozi na teknolojia yake kwa miaka sitini sasa huku tukishuhudia ongezeko la mifugo yetu kila kukicha, je uvunaji wa bidhaa zetu utafanika namna gani?. Mpaka sasa licha ya kuwa na ngombe takriban milioni thelathini achilia mbali mbuzi, Je ongezeko hilo limekuwa ghafla? Hapana kwa kawaida sio ghafla, hivyo tulisinzia wakati mmoja. Hivyo twaweza sema taasisi zetu za kuandaa wataalamu ni chache sana hasa kwa elimu mahsusi inayohitajika sekta ya ngozi. Je, ni nani aandae wataalamu wetu, watatoka wapi? Hao wachache waliopo wametumika vipi mpaka sasa?. Basi tutafakari hili ili kujua kama kweli ni tatizo au tumelitengeneza.

Ukosefu wa elimu ya ufugaji bora

Ndio! Ni ukweli usiopingika kwamba ngozi bora hutegemea ufugaji bora , pia ngozi bora ndio huhitajika kwa bidhaa bora kutoboa katika ushindani wa soko la bidhaa la ngozi uliopo katika ulimwengu wa utandawazi sasa. Je, si kweli kwamba ukosefu wa elimu ya ufugaji ni tatizo la kusadikika? Hebu tupitie hizi takwimu japo kwa uchache wake, ukiachana na vyuo binafsi vya mifugo serikali pekee kupitia wakala wa vyuo vya mafunzo ya mifugo (LITA) ina takribani kampasi sita zinazotoa wahitimu kila mwaka katika ngazi ya cheti na astashahada ya afya ya mifugo na uzalishaji.Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo ni moja kati ya taasisi kubwa inayozalisha wahitimu wa elimu ya mifugo kwa miaka sasa. Tuje hapa sasa, Wako wapi wataalamu wetu? Wametumika vipi?. Ni kweli kwamba anaweza asiwepo kati yetu mwenye jibu sahihi la maswali haya ila pia tutakubaliana kuwa tunaishi na wataalamu wengi miongoni mwetu na thamani ya elimu yao ikiwa kama ndoto. Je, watachangia vipi katika sekta hii mazingira ya kuwatumia kutoa elimu bora ya mifugo sio wezeshi kwa namna moja hadi nyingine na mara nyingi sio kipaumbele cha mamlaka husika.Je, ni wafugaji wetu wameikataa elimu? Basi kiufupi binafsi naweza sema kuwa changamoto hii ni ya kusadikika, sio changamoto halisia.

TUISHI HUMU

Tusisubiri chombo kizame, tuokoe jahazi.Tujaribu kufanya haya, ni tija kwa uchumi wa taifa letu.

Tujifunze sera bora za kisekta kwa wenzetu waliopiga hatua zaidi

Majirani zetu mfano Ethiopia na Kenya zimepiga hatua katika kuthaminisha bidhaa zao za ngozi na ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa usafirishaji wa ngozi ghafi kutoka barani Afrika kwenye soko la Ulaya na Asia.Tusafiri kwao kujifunza, turudi tutekeleze.

Tupitie mfumo wetu wa kutoa wataalamu kama ndio tunaouhitaji.

Ile kasumba yakuwa na mitaala ya zamani tena iliyoandaliwa bila kuzingatia mazingira yetu ni ugonjwa unaotutesa. Tunapata wataalamu wasio na elimu inayoshabihiana na mazingira yetu, wasioendani na kasi ya teknolojia na wasioelewa Tanzania yao inahitaji nini kwa miaka ijayo kutokana na elimu na sekta yake. Tuachane na mitaala ya kurithi, tufikiri katika wakati uliopo. Tatizo la kukosa wataalamu haliwezi tatuliwa bila kutafakari mifumo tunayoitumia kuzalisha wataalamu wetu. Ikiwa tunahitaji uchumi wa viwanda kulingana na ukuaji wa teknolojia basi kuandaa mifumo ya kuzalisha wana teknolojia wetu, wanaojua mazingira yetu na wanaojua lengo letu ndani ya miaka kadhaaa basi huo ndio ufunguo wa mafanikio yetu ikiwemo ndani ya sekta hii yenye utajiri wa kufikia

Tusianze upya , Tuanzie tulipoishia

Sekta ya ngozi ilikuwepo toka awali na kuna wakati katika nchi yetu ilifanya vizuri, tuweke akilini pia wakati huo teknolojia ilikuwa bado chini. Sasa ni wakati muafaka wa kurudi nyuma na kufufua vituo vyetu vya kukusanya ngozi kutoka kwa kila mfugaji wetu na kila machinjio yanayotuzunguka maana imekuwa ni kama mizoga iliyokosa thamani, tuipe pia ngozo thamani yake kwa kuinunua kwa bei halali na stahiki inayoendana na thamani yake katika soko la dunia. Hii itawapa nguvu wafugaji ili kujua ni utajiri gani ulio katika bidhaa hii adhimu ya mifugo yao.

Asanteni kwa kunisikiliza

imekaa poa sana kaka hii
 
Wakati tunaelekea mwisho mwisho mwa stories of change 2022 tupite kidogo kupata madini, kuchangia na kupiga Kura.
 
Back
Top Bottom