Mdude Nyagali aendelea kusota Rumande, Kesi yake dhidi ya RPC wa Songwe kusomwa Jumatatu

Mdude Nyagali aendelea kusota Rumande, Kesi yake dhidi ya RPC wa Songwe kusomwa Jumatatu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Leo, ilikuwa siku ya kusomwa uamuzi wa kesi ya Habeas Corpus inayomhusu Mdude Mpaluka Nyagali dhidi ya RCO Songwe na wenzake wawili.

Hata hivyo, kutokana na kuingiliana kwa usikilizwaji wa kesi nyingine ya mauaji, maandalizi ya hukumu ya shauri hili hayajakamilika.

Soma zaidi: Mdude amburuza kortini RPC Songwe, Mwabukusi kumuwakilisha katika kesi hiyo

Uamuzi sasa utasomwa siku ya Jumatatu, tarehe 2 Desemba 2024, saa tatu kamili asubuhi mbele ya Mheshimiwa Jaji Pomo.
Screenshot 2024-11-29 151319.png
 
Wakuu,

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya, imeahirisha kutoa hukumu ya waleta maombi ambao ni wakili Boniface Mwabukusi na Wakili Philip Mwakilima kuitwa mahakamani kwa Kamanda wa Polisi na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Songwe, kwa madai ya kumshikilia Mdude Nyagali Mpaluka kinyume cha sheria.

Mahakama hiyo imeahirisha kutoa maamuzi ya kuwaita wawili hao mahakamani ikiwa ni maombi ya mawakili Mwabukusi na mwenzake ambapo kesi hiyo sasa itakuja mbele ya mahakama jumatatu ijayo (Desemba 02, 2024) baada ya kumalizika kuandaliwa kwa maamuzi hayo.

Jaji mkazi wa Mahakama kuu Kanda ya Mbeya Musa Pomo ameahirisha shauri hilo hadi mwanzoni mwa juma lijalo


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, Wakili wa kujitegemea Boniface Anyisile Kajunjumele Mwabukusi, amesema ni imani yao (mawakili) kuwa Mdude Nyagali alishikiliwa kinyume cha sheria na kunyimwa haki zake za msingi ikiwemo kuonana na mawakili na kupewa dhamana, hivyo kuiomba mahakama iwaamuru vigogo hao wa Polisi (RPC na RCO Mkoa wa Songwe) kufika mbele ya mahakama kujibu hayo.

Huyu mtu anayeitwa Mdude huwa ni mropokaji sana wa matusi nadhani ni mvuta bangi mkubwa na kichwa kiliishachanganyikiwa,, mimi ningekuwa ndo hakimu ningetafuta kifungu kwa anayetoa maneno machafu nikakitumia kumfunga miaka 30

 
Anavuna alichopanda huyo dude! Mdomo uliopitiliza unaponza. Kuna na yule dogo anaropoka hovyo mitandaoni anatukana matusi ya nguoni kila siku
 
Chadema wako wapi maana hiyo baba yake ndio mwenye chama wanatumia jina la ukoo wao!
 
Back
Top Bottom