Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,207
- 17,674
Wakizungumza leo, Agosti 21 baada ya kuripoti kituoni hapo, Mdude amesisitiza kuwa hawatarajii kurudi tena kituoni hapo hadi jeshi hilo litakapokamilisha upelelezi na kesi yao kwenda mahamakani akieleza kuwa wataendelea na shughuli zao ndani na nje ya Mkoa.
“Tumeambiwa kurudi tena Polisi Agosti 28, lakini tumewapa msimamo wetu kuwa haturudi tena hadi kesi itakapokuwa tayari twende mahakamani, pili tumemwambia RCO hana mamlaka ya kutuzuia kusafiri kwani ni kinyume na sheria na katiba,”
“Hili jambo lililotukuta ilikuwa ni njama za kukutisha kuturudisha nyuma, tuko tayari kwa lolote katika kuipigania nchi, tupo kwenye mazungumzo na Dk Wilbroad Slaa kupanga maandamano kuanzia nje ya nchi,”
“Wale diaspora waliopo nje ya nchi wote watafanya maandamano yasiyo na kikomo zilipo Falme za Kiarabu popote wakati tukijiandaa na ya hapa ndani, kama serikali itasitisha mkataba huu wa DP World tutaachana nalo,” amesema Mdude.
Kwa upande wake Mwabukusi amesema tangu kukamatwa hadi kuachiwa ilikuwa ni kinyume na sheria kwani hata mawakili wao hawakuwashirikisha katika suala la dhamana.
“Kwanza nafikiria kushauri wakili wetu aandike barua kujiondoa kwa sababu hakuna kesi yoyote tumepewa, hata dhamana hatukushirikishwa, hata wanaoshauri nihame nchi sikubali, wa kuhama ni wale DP World,” amesema Mwabukusi.
Gazeti la Mwananchi