Mdude Nyangali ni Nelson Mandela wa kizazi hiki

Mdude Nyangali ni Nelson Mandela wa kizazi hiki

DENLSON

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
949
Reaction score
1,260
Wasalaam,

Leo tarehe 28 Juni 2021 Mahakama amemuachia huru aliyekuwa mtuhumiwa wa kosa la kuuza madawa ya kulevya.

Sitagusia juu ya kesi au namna ushahidi ulivyotolewa ila nataka kuongelea msimamo alionao Mdude Nyangali mwanachama mtiifu wa CHADEMA hata akajiita MDUDE CHADEMA.

Taifa linahitaji vijana wengi kama yeye. Ni kijana jeuri mwenye msimamo usioyumba wala kuteteleka labda kama Nelson Mandela.

Leo baada ya kuachiwa moja kwa moja ameongelea suala la Katiba Mpya. Ni watu wachache sana wenye ujasiri wa Mdude ambao bado wanaishi.

Fikiria wale vijana jeuri wa Magufuli leo wanavyo mkana hadharani? Kama wameshindwa kulinda falsafa za Magufuli kwa siku 100 tu wanaweza kusimamia misimamo yao binafsi pasipo mbeleko ya dola?

Mh. Rais unahitaji vijana aina ya Mdude kwenye Serikali yako. Wapime hata kwa moto na njia ni nyepesi tu kama huijui soma kitabu cha Daniel utaelewa ninachosema.

Ukipata vijana 10 kama Mdude unakuwa na uhakika juu ya falsafa ya chama/nchi itakuwa hai hata ukifa, huitaji kutumia fedha au nguvu kulinda legacy ukiwa na watu aina ya Mdude.

Kwa sasa Mdude Nyagali ni Nelson Mandela wa kizazi hiki.
 
Upuuzi mtupu!

Kusikiasikia pekee sifa za Mandela, haitoshi kuelewa jinsi alivyokuwa.

Kumsikia kwako huko Mandela, ndio unataka kumlinganisha na vijana wachache wavuta bangi wa chadema?
Acha wivu wa kike kwa mdude.
 
Uwe unatumia akili yako hata kidogo tu. Utaanzaje kumfananisha Mandela na vitu vya kijingajinga. We do sympathize with Mdude kwa madhila aliyopitia, lakini kumlinganisha na Mandela Ni kejeli kwa Mdude mwenyewe na hivi hata yeye anaona aibu kwa sifa za kejeli mnazompa
 
Back
Top Bottom