Tatizo SIO Dini tatizo ni Rais asiyechukua hatua.
Unakopa matrilion ya pesa halafu unajenga miundo mbinu Ili ukusanye pesa matokeo yake unawatafuta Wageni waje kukusanya pesa . Ni akili kweli? Wewe Umaskini kuwa Waarabu watakusanyia pesa Ili upate maendeleo kweli .?
Ujinga Wa Mwafrika ni mzigo mkubwa sana?
Kwa Sheria Gani itajayowazuia Waarabu na marafiki zao walioweka pesa Kwa mgongo Wa DPW wataacha kuchota pesa na kwenda kujenga majumba Yao ya dhahabu Dubai.?
Hivi huoni kuwa tuna Serikali ya Wezi ndio mana hawajiwekei Sheria Kali.
Kwa Sasa mpaka Spika Wa Bunge hashtakiwi ! Kuna watu wenye maamuzi zaidí ya Kumi hawashatakiwi kutoka MTU mmoja !
Sheria za kiislam Kule Uarabu ni Kali Kwa Wala rushwa na Wezi Wa Mali za umma. Je, Tanzania Sheria zinawachukuliaje Wale wanaokomba Mali za umma?
Huku wale wanaowataja Wezi ndio wanaoshughulikiwa halafu utegemee Mwarabu akupe Hela kwenye nchi yenye Sheria za kipumbavu na za kuwabeba mwawziri na wakurugenzi Wezi Badala ya kuwanyongelea mbali?
Mwarabu na MCHINA ni MTU mkorofi Kwa asili yake bila Sheria atatengeneza mpaka pesa za bandia na atawanunua mahakimu Majaji,mapolisi, mawaziri na wabunge na hakuna pesa itakayoongezeka kwenye mapato zaidí ya Kodi na Tozo Kwa Maskini Wa nchi hii.
Wanasafirisha wanyama usiku na mchana kule Loliondo,wanasafirisha Madini Kwa matani kule Geita . Lakini mikopo Imekua Kwa Kasi Tangu Awamu hii iingie madarakani. Je, tunakosaje pesa za kigeni wakati tunasafirisha Madini ya Kila aina?
Watalii wameongezeka tunakosaje pesa za kigeni. Kiufupi hatuna MTU Wa kuwabana Wezi Wa Mali za umma zaidí ya kupambana na akina mdude na Mwabukusi.
Mungu atasimama . Hakuna Chama kitakachokaa milele madarakani. Hata ikiwa ni CCM lakini Roho ya MAGUFULI itainuka na kuwaingia watu WENGI zaidí kuliko Mwabukusi.
Bahati yenu hakuna wapinzani Wa maana zaidí ya wpinzania WASIOJUA wanataka nini?
Waarabu watachota pesa na hakuna kitakachobadilika Kwa sababu hakuna Sheria Kali ya ndani itakayowabana zaidí ya kushirikiana na watanzania kuiba Kwa Kasi mana hakuna atakayeshtakiwa ndani ya nchi au Hata kufilisiwa !! Utawapata vipi watu usipokuwa na mamlaka juu Yao?
Bora Kwa Sasa akija Rais mwenye Uzalendo na uchungu na watanzania Wa Hali ya Chini anaweza akawafukuza kazi Wezi Wote pale bandarini na kuajiri Wengine Hata kufilisi Mali zao ikawa fundisho Kwa Wengine. Lakini Waarabu wakiiba Nani atawakamata ? Nani atazuia pesa Zao ? Nani atamweka Mwarabu ndani ? Nani atamtisha Mwarabu Ili aheshimu visheria vyetu vinavyowabeba Matajiri na kuwashughulikia Maskini ? Wanatorosha wanyama Kule Loliondo Nani amewahi kusikia Mwarabu kakamatwa Kwa kutorosha wanyama?
Lakini Mtanzania akiua Hata digidigi anafungwa miaka Gerezani? Mtanzania akikamatwa na ngozi ya Nyumbu aliyekufa kibudu anashughulikiwa kweli kweli .
Watauza mpaka Mlima Kilimanjaro mana wakati Wa Ukoloni eneo la Mlima Kilimanjaro lilikua linataka kukabidhiwa Wazungu Ili liwe eneo lao la makazi na wachagga walikua wanataka kuhamishiwa huko kigoma na katavi.
Bahati nzuri alitokea MTU mmoja akaona waraka kwenye ofisi za wakaloni akatoa Siri . Wachagga wakagoma kuwa hawatakua tayari kuhamishwa Kwa Treni kwenda Maeneo mengine Ili kupisha Maeneo Yao ya asili yenye rutuba na Maji ya kutosha na Hali ya hewa nzuri. Haya mambo ya wageni kutaka Maeneo mazuri na miradi mizuri ya wazawa hayakuanza leo. Tukiwa na viongozi legelege Iko Siku Hata Bahari Yote ya Hindi itauzwa .