Mdudu wa kidole, natamani kukata kidole

Mdudu wa kidole, natamani kukata kidole

MAWEED

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
3,550
Reaction score
12,239
Salaam wanajamvi, natumaini mko salama na kwa wale mliokatika mfungo, Mungu akawaongezee palipo pungua.

Wakuu mwenzenu yamenifika, kidole changu cha kati mkono wa kulia kimevimba hatari. Kinauma mno yaani hakukaliki, hakulaliki. Najihisi mnyonge, nimekosa tumaini.

Nimeweka mafuta ya taa, nimepaka Colgate, maji ya betri, vitunguu swaumu, maji ya moto, lakini wapi? Kuna watu wananiambia nisichokonoe wala nisiende hospitali.

Kama kuna aliewahi kuumwa na akapona, naomba msaada wake. Nimetingwa ndugu zangu. Nauona moto mpaka nmewaza isije kuwa kansa, nka-kate kidole.
 
Soma hapa mkuu. Tafuta ndulele

Basi hiki ni tofauti na changu, hapo kwenye hayo maelezo wanasema ni masaa 24 kinaacha kuuma,mimi nimeweka hiyo ndulele leo siku ya tatu lakn bado kidole kinapwita ah
 
Mbona dawa unayo hapohapo, chukua bangi mbichi majani kama matani hivi kisha yafikiche mpaka yatoe kama mchuzi hivi, mwagia huo mchuzi kwenye kidonda hapo, fanya hivyo kwa siku tatu utaona mabadiliko.
 
Nenda hospital, kafanyiwe check up kuna sindano huwa wanachoma kama uvimbe haujawa na usaha ndani yake na kuondoa hiyo infection ni jamii ya funguses kama sikosei.
Shukran sana, huyu bacteria ataniua
 
Mkuu pole sana. Kuna majani fulani hivi kule moshi unayatafuna ili yalainike halafu unayaweka kidoleni unayafungia na kitambaa kwa huku mjini sijawahi kuyaona zaidi ya kule Moshi. hata jina lake kwa kiswahili sijui
 
Back
Top Bottom