Me against UNDP: This photo...

Me against UNDP: This photo...

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,199
Reaction score
8,761
1._village_children_in_africa.jpg

Hivi jamani , picha kama hii kwa kuitazama, ina lengo la kuongelea juu ya umasikini tu wa watu wa Africa?

Mi naona kama vile kuna meseji iliyofichama, ikiandamana na picha hii, nayo ni udhalilishaji wa Waafrica...Wenzangu mnaonaje?

Source: UNDP report on African Poverty.
 
ninapoitazama hiyo picha, naona utajiri wa mali, utamaduni na tabia.

Angalia afya ya watoto pichani; ni njema tu, wamekula na kushiba

Angalia nyuso zao za furaha na confidence ya kaka yao

Angalia utajiri kwa kigezo cha kununua misumari iliyogongelewa kwenye hiyo chanja waliokalia, palipo na uwezo wa kununua misumari, hapakosi wa kununua nguo na sabuni

Angalia nguo, hazijachakaa

Angalia utamaduni wa kujipamba, hizo shanga shingoni, thamani yake ni kubwa mno, kama ni suala la nyumba, huo ndio utamaduni wa watu hao. Kama ni watoto kukaa uchi, well inawezekana ni kutokana na utoto wao na michezo walokuwa wakicheza kabla ya kupigwa picha hiyo, tena michezo yenyewe ndo imewafanya wajae mavumbi. Kimsingi sio wachafu, ndo maana wamenyolewa nywele vizuri sana.

Angalia heshima aliyopewa/alojipa mtoto wa kike; kujisetiri. Hii ni kinyume na tamaduni za magharibi ambapo anayejisetiri ni mwanaume, wanawake uchi uchi (kumradhi)

Kwa ufupi, kama mpiga picha alitaka kuzungumzia umaskini, mwambie sio hivi. Data hazijatosha arudi field.
 
Tatizo liko wapi hapo ?
Are you an alien from the Jupiter?

Umepewa na visual aid kabisa, bado hufanikiwi kutoa hata comment inayosomeka, in connection to hoja ya mleta thread!...are we really together!
 
Kwa ufupi, kama mpiga picha alitaka kuzungumzia umaskini, mwambie sio hivi. Data hazijatosha arudi field.
Alikuwa anawafanyia kazi ma-Bwana wakubwa, akafanya ili apate mshahara!

They're doing these unfair games over our African Continent, am not impressed at all!
 
Are you an alien from the Jupiter?

Umepewa na visual aid kabisa, bado hufanikiwi kutoa hata comment inayosomeka, in connection to hoja ya mleta thread!...are we really together!
Naungana na wewe huu ni udhalilishaji uliokubuhu. Kuna haja ya kuwaandikia na kuwaeleza juu ya hili. Mbona wao wanaheshim sana privacy ya vitoto vya kizungu. This is extreme. PJ chukua hatua otherwise ruhusu wengine tuandike juu ya hali hii. Hata km kunaumasikini kielelezo si uchi wa huyo mtoto
 
Nilikuwa kwenye Debatt moja mwezi November 2009 pale Holand.walikuwa wanajadiri series program inayo onyeshwa kwenye TV ya Kiswedish kila wiki ambapo familia tatu za Kiswedish ziliamua kujigawa na kwenda kuisha na familia tatu tofauti kati ya Afrika, Asia na Latin Amerika. Familia Moja ilipata kwenda Zimbabwe . Actually ilikuwa ni zaidi ya picha hii ya UNDP. na si kwamba ilikuwa ni Afrika tu bali hata wale wenzetu wa Asia na kule Latin Amerika hawakuwa na tofauti kubwa sana kwani ZILICHUKULIWA KULE VIJIJINI KABISA KWENYE TAMADUNI ASILIA. Kwahiyo siwezi kushangaa sana japo kwa tamaduni zetu kuonyesha picha za utupu hata za watoto wadogo ni jambo gumu kabisa..!
 
1._village_children_in_africa.jpg

Hivi jamani , picha kama hii kwa kuitazama, ina lengo la kuongelea juu ya umasikini tu wa watu wa Africa?

Mi naona kama vile kuna meseji iliyofichama, ikiandamana na picha hii, nayo ni udhalilishaji wa Waafrica...Wenzangu mnaonaje?

Source: UNDP report on African Poverty.

Mwenzenu hapa nimechoka...phewwww!!!!!!!
 
Pich haina tatizo, tatizo mni wewe ambaye unadahanihukuwahi kukaa mazingira kama hayo ama hata mwnajamii yako
 
Kwa imani niliyonayo.. hawa watoto walihiaji kusetiriwa kwani kuna siku watakua wakubwa na kushtaki kwa kudhalilishwa!!! Sehemu za siri hata kama ni za mtoto zinahitaji staha na heshima.... Hata maiti husetiriwa sembuse hawa

Shame on UNDP, I am hurt!!
<input id="gwProxy" type="hidden"><!--Session data--><input onclick="jsCall();" id="jsProxy" type="hidden">
 
Piha kama hizi unaweza kuzipata hata bagamoyo yaani Km100 toka capital city achilia mbali mikoa mingine
 
Kama unashangaa hii photo ya vijana (watoto ) wa kiafrika, winter karibu inaisha huko ughaibuni hebu nenda ukaone fikwe za wenzetu zitakavyo jaa watu wa zima bila nepi wala shimizi
 
Ni udhalilishaji kwa Mwafrika. Na sijui ni kwanini wameona ni OK kumweka na/au weka wavulana uchi! Kuna kitu hapo.

Waafrika lazima tuitangaza afrika na tuachane na utegemezi kwa Mzungu anayetuonyesha kama vinyago.
 
Alikuwa anawafanyia kazi ma-Bwana wakubwa, akafanya ili apate mshahara!

They're doing these unfair games over our African Continent, am not impressed at all!

Mkuu unataka kusema huo ni uongo? siamini kama mnataka kubisha kuwa Afrika hakuna watu wanaoishi kwenye mazingira magumu namna hiyo.
 
Hawa jamaa wanatuzalilisha sana, hakuna zuri lolote kutoka Afrika linalozungumziwa nchi nyingine nje ya Afrika hasa kwenye hizi nchi zenye wazungu, kuzungumzia umaskini kwa kuweka picha kama hiyo inaonyesha wazi kuna ubaguzi tena mkubwa sana coz kulikuwa kuna uwezekano wa wahusika kufikisha ujumbe wao kwa kutumia picha ambazo hazionyeshi hali mbaya kama hiyo ya watoto wakiwa hawana hata nguo ya kusitiri miili yao.
Umaskini kweli Afrika upo ila haina maana kwamba maskini huyu asipewe heshima kama walivyo binadamu wengine, kwa mazingira kama hayo hakuna kitu muafrika utasema au kufanya mbele ya mzungu ukaonekana ni mtu, unakuwa kama vile kitakataka flani ambacho hakina thamani...
 
Kama unashangaa hii photo ya vijana (watoto ) wa kiafrika, winter karibu inaisha huko ughaibuni hebu nenda ukaone fikwe za wenzetu zitakavyo jaa watu wa zima bila nepi wala shimizi

Mkuu Gama, hao unaozungumzia wewe wanafanya hivyo kwa starehe zao na bangi zao. Hiyo ni tofauti kabisa na huyu mtoto ambae kwa kuangalia eneo alipo unajua ni hali ngumu ya maisha na sio chaguo lake kuwa hivyo alivyo.
 
Ni wazi kusudio la hii picha ni kwa wale watu wa magharibi kuonyesha umasikini wa Afrika. Ni rahisi watu hao kutoa misada wakiona picha kama hiyo. Hili linasababishwa na viongozi wetu kupenda misada kutoka huko.
 
even in europe there are some childrens living like africans! so, they just feel good when they publicise these kind of pictures!
 
Naungana na wewe huu ni udhalilishaji uliokubuhu. Kuna haja ya kuwaandikia na kuwaeleza juu ya hili. Mbona wao wanaheshim sana privacy ya vitoto vya kizungu. This is extreme. PJ chukua hatua otherwise ruhusu wengine tuandike juu ya hali hii. Hata km kunaumasikini kielelezo si uchi wa huyo mtoto
Jibu unalo mwenyewe. Wanaheshimu na hiyo pamoja na kuwa nguo. Haiwezekani kusema hata suruali ya baba iliyochanika ikaunganishwa kwa sindano ya mkono inashindikana. Watu hawajali wakikumbushwa wanasema wamezlilishwa.

Mkuu unataka kusema huo ni uongo? siamini kama mnataka kubisha kuwa Afrika hakuna watu wanaoishi kwenye mazingira magumu namna hiyo.
Ndugu yandu hapa una deal na Wabongo. Denial ni ugonjwa wao mkuu. Lakini hata mkuu wao wa kaya naye ni yale yale. Alisima huku povu likimtoka eti Watanzania hawali mapanki. Saupper katudhalilisha , na maneno mengine yakuudhi.
 
Back
Top Bottom